Bob Marley alijibu hili swali kwenye ule wimbo wake wenye maneno aliyokuwa anatuambia sisi weusi. Baadhi ya hayo maneno ni:-
"EMANCIPATE YOURSELVES FROM MENTAL SLAVERY..."
Sisi kweli ni WATUMWA kwenye namna yetu ya kufikiri.
1. Africa (na weusi kwa ujumla), tuna watu wenye IQ kubwa sana, na wana uwezo mkubwa pia katika fani mbalimbali ikiwepo mpira, muziki, n.k.
2. MATATIZO MAKUU ya Waafrika ni MATATU
a) KUFURAHIA KUTAWALIWA
b) UBINAFSI WA KUTISHA
C) KUAMINI UCHAWI KWENYE KILA JAMBO
Tunafurahia
kutawaliwa kisiasa, na kiuchumi. Akija mzungu au mhindi au mwarabu akisema anataka kuwekeza, anatetemekewa na wahusika wote, japo amekuja na pesa kidogo tu. Anaenda ardhi, anapewa eneo la kuwekeza. Anaenda benki, anakopa, kwa kuweka dhamana ardhi yetu tuliyompa.
Anatoa rushwa kidogo anapewa vibali vyote. Anakopa mpaka mashine za kuchimbia madini.
Wewe mwananchi KAMWE HUTAPEWA FURSA KAMA HIZO. Upewe halafu "kesho utajirike"? Hakuna !! Utumwa wa akili (mental slaver) aliouimba Bob Marley.
Baya zaidi, mchimba madini anadaiwa ASILIA NNE TU (just 4%) ya thamani ya madini YETU !!
Kama sio UTUMWA WA AKILI kukubali kupokea 4% ya madini yaliyochimbwa (badala basi hata kugawana nusu) ni nini? Mbona Botwsana wanapata nusu ya kile kilichovunwa ?
Yaani KIUKWELI tunafurahia wageni WATUTAWALE (hata kama sio kisiasa) KIMAPATO.
Hilo la UCHAWI nadhani linaeleweka. Miaka kadhaa iliyopita, mbunge Msukuma Kasheku ALISEMA BUNGENI (na kwenye hansard rekodi ipo) kwamba anaamini HAKUNA MBUNGE ambae hajaenda kwa mganga wakati wa kusaka ubunge. (Kumbuka mawaziri wanatokana na wabunge). HAKUNA MBUNGE YEYOTE ALIYETOA TAARIFA YA KUPINGA MANENO HAYO.
Kwa misimamo kama hiyo, unadhani tutakaa tuendelee?