Uchaguzi 2020 Waajiri wamuonya Lissu kupotosha kuhusu ajira

Uchaguzi 2020 Waajiri wamuonya Lissu kupotosha kuhusu ajira

Aibu tupu kwa andiko la kinjaa njaa kama hili.
Mtu katoa hoja kemkem. Hakuna hata moja unayothubutu kuikosoa. Unaishia kusema andiko la kinjaa njaa. Tupe basi hizo hoja za wewe uliyeshiba tulinganishe na za huyu mwenye njaa. Si lazima kupinga kitu kama huwezi kutoa hoja zinazotetea maoni yako, eti tu kwa kuwa uko upinzani.
 
Hata hujui kuwa humu JF karibu kila member ni mtumishi/mwajiriwa na wengi wakiwa wa umma....

Kwa lugha rahisi ni kuwa huwezi kudanganya humu halafu ukabaki salama...

Tangu baba yenu Magufuli awe Rais, kwa miaka mitano yote amezuia "STATUTORY ANNUAL SALARY INCREMENT" ambayo ipo kisheria kwa kila mtumishi achilia mbali kuongeza mishahara halisi (Gross Net Pay) pamoja na KIMA CHA CHINI kwa kuzingatia hali ya uchumi wa nchi....!!

Sasa mbona mnatudanganya mchana kweupe kana kwamba sisi ni wajinga???
Umepata wapi ujasiri wa kuongea na wakupuuzwa?
 
Watumishi gani waliolipwa madai mbalimbali ya mishahara au nyongeza za mishahara,ni watumishi wa mwaka gani,maana wapo watumishi mbalimbali wanaodai malimbikizo kibao ya mishahara yaliyosababishwa na serikali wakati wa zoezi la uhakiki wa watumishi miaka ya 2017/2018,2018/2019 ambao hawajalipwa mpaka sasa
 
Kuna haja ya lazima watumishi nao watoe waraka manake uma unapotoshwa na njaaaaaa, hashim rungwe ameliona hili, ubwabwa na kuku kuanzia mashuleni mpaka mtaani ili akili ziwarudie hawa binaadamu.
 
Ila hii nchi bana.

Huyo Mchange naye anachotea mabilioni ya pesa kutoka hazina kwaajili ya kuendeshea propanda kama hizi.Aisee.

So hii makala kesho itakuwa Jamvi la habari?

CCM wamewekeza na wanatumia mabilioni na nguvu kuubwaa kwenye mambo ya kpuuzi halafu utegemee eti kuna siku Tanzania itapata maendeleo, aisee
 
Akili ukielekezea tumboni ni kubaya huyo ni mchumia tumbo lake anatetea ugali wake na familia yake ila sisi wafanyakazi tunajuwa mbivu na mbichi ya awamu ya tano ilichotufanyia katika stahili zetu ambazo ziko kisheria
 
Nilipo ona habari leo na habib mchange nkajua basiii hakuna kitu hapa
 
Mchange Ni Kama musiba Kama akupata teuzi asahau jamaa yake akajiajiri October sisi sio mifugo tunachagua mtanzania mwenzetu this time
 
Huwa nashangaa Sana kukuta mtumishi mfano polisi au mkurugenzi wa tume akisaidia kuurudisha udhalimu Hali hanufaiki nao huku wameambiwa kabisa wasitegemee nyongeza au maboresho yeyeto. Kipi Cha kunufaika wamepigika 5 yrs wanataka msoto Tena 5 yrs.
 
Hii issue ya mishahara, naona inajaribu kuzimwa, lakini ukweli kwamba ndio huo wa Tundu Lissu, wamwache apambane na hali yake, yeye alijiona mjanja kwa kunyima haki za watumishi Leo anaomba msaaada, wamwache apambane na hali yake
 
Mbona sisi wafanyakazi hela tunaiyona.....,Huu Uzi ni propaganda.
 
Mimi ni mtumishi wa umma sijawahi sijawahi kupandishwa cheo wala mshahara tangu huyu MNYAPARA AINGIE MADARAKANI.
Acha ukasuku.
Wakati nasoma nilitamani kutukana ila nikamezea. Huyu jamaa ni mtumishi wa umma kuzimu labda
 
Back
Top Bottom