Waalimu hawataki kufundisha shule za vijijini

Waalimu hawataki kufundisha shule za vijijini

Kule hupangwa walimu wa kiume wagumuwagumu, wa kike hupangwa mjini au vijiji vilivyochangamka na vina barabara za kwenda mjini kwa urahisi. Kama mdada naye kakamaa sura kama kaonja limu naye hupangwa kijijini ila panapofikika kwa urahisi. Hawa wenzangu na mimi wao ni vijijini penye mazingira magumu, urafiri kwenda mjini ni shughuli pevu, hakuna nyumba nzuri za walimu, kule utakutana wasomi wengine ambao ni afisa mtendaji wa kijiji na daktari wa zahanati ya kijiji na manesi wawili watatu wenye sura kauzu zilizokomaa waliopangiwa kazi huko ndani kijijini. Wenzao pisi kali hupangiwa mjini, ni vituko kwa kweli upangaji watumishi wa umma vijijini
 
We mwalimu kijana ndio kwanza unapangwa kazi kijijini utakutana na walimu wazee wanaohesabu miezi kustaafu, Utaambiwa kijana umeletwa huku kijijini usopoongeza elimu utazeekea hukuhuku na kustaafia hapa. Mwanzo utapokelewa vizuri sana na wanafunzi pamoja na wanakijiji. utalishwa mayai, maziwa, nyama, mbogamboga. matunda na ofa zingine kwa kuwa ni mwalimu mpya. Ukizoeleka hutaona ofa tena. Ni daktari wa kijiji tu ataendelea kupata ofa za wanakijiji kwa kuwa anawatibu magonjwa yao. Kuna 'shule za adhabu' kama mwalimu ni mtovu wa nidhamu kwa mabosi wake wa wilayani hutupwa huko interial akapambane na mazingira magumu, na wakiona una enjoy maisha ya huko unalima, unafuga wanakuhamisha tena kukupelea sehemu usiyoweza kuwekeza miradi yako. Kuna walimu wakipangwa kijijini hufurahia huko kwa kuwa wanaona wamepata fursa za kilimo na ufugaji
 
Kituko kingine cha walimu wanaopangiwa kijijini hasa vijiji vya ndani ndani, walimu wa kike huishia kuolewa na wakulima, wavuvi, wafugaji. Mwenyekiti wa kijiji hupewa kipaumbele kuoa mwalimu. Ni bahati sana wasomi wawili daktari wa kijiji, nesi, mwalimu, mtendaji wa kijiji kuoana wasomi kwa wasomi waliokutana huko kijijini na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na hatimaye kuoana
 
Back
Top Bottom