LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 29,814
- 47,414
Kule kijijini utakuta shule haina mwalimu wa kike, ni wanaume watupu. Kuhusu masuala ya wanafunzi wa kike inabidi mmpate mama mtu mzima mwanakijiji mmfanye ndio matroni kwa ajili ya wanafunzi wa kike japo huyo mama hapati posho anajitolea tu ila mtampa kipaumbele kuwa mpishi mkuu shuleni nyakati za mitihani ya kitaifa. Kuna shule za vijijini kumpanga mwalimu wa kike ni shughuli pevu labda uumpe adhabu umtupe huko mpaka ashike adabu ndio umtoe huko ndani kijijini kusiko na barabara ya kueleweka mbali na mjini