Waalimu hawataki kufundisha shule za vijijini

Waalimu hawataki kufundisha shule za vijijini

Si walimu tu, professional yoyote hawezi kufanya kazi vijijini aache mijini, tena Dar kwanza. Ndio ukweli.
Wengi tu hawaipendi hiyo dar..

Kikubwa ni kuweka huduma za jamii na miundombinu rafiki.
Hayo mengine ya ulozi, mila za ajabu na kasumba mbalimbali yatajiondokea mwingiliano wa watu ukiwa mkubwa.
 
Kunq vijana wakati nawafanyia maombi ya Ajira za ualimu. Kauli zao zilikuwa " Bro nijazie shule zq ndani ndani huko vijijini ili nipate kazi, na ntaenda kukomaa" Few Moment later baada ya kupata Ajira. Wakaanza kupiga sim " Bro ukitaka kuhama unafanyaje??? Maana huku bro sio kabisa"
Serikal ina haja ya kuajili wazawa sehem hzo za Vijijin maana wao angalau wanaweza pambanq na changamoto zote za huko.
Pili Kila Wilaya ianishe maeneo ambayo ni Changamoto sana kwa watumishi , na baada ya kuyabaini maeneo hayo basi kuwe na Motishq kwa watumishi wanaopelekwa huko
Mwisho, Jamiii na serikal ihakikishe inakomesha uanzishwaji wa makazi holela holela. Yaani kuna sehem unapita mpaka unajiuliza hawa walifuata nini huk? Maana eneo la makazi ni changamoto kwa kupeleka huduma yoyote ya Kijamii kma maji na Umeme
 
Wanaofundisha vijijini wapewe mshahara mkubwa kuliko wa mjini gap liwe walau laki moja hii itasaidia Sana

Shida nchi yetu ukiweka hivyo utakuta anaongezewa mtu asiyestahili kabisa kama zilivyo pesa za mkopo wa asilimia kumi
 
Wanaokubali kwenda kufundisha huko Serikali iwape special allowance kufidia ugumu wa mazingira magumu
 
Kijijini maisha mserereko ,watumishi wa mjini ndiyo wale hata kodi kulipa kuna muda inawashinda maana matymizi ni makubwa na mshahara ni kiduchu ni hapo wanaenda kwa akina bwana MABOTO MICROFINANCE siku si nyingi mara mwalimu kanyang'anywa TV kisa deni la laki moja 😂😂

Kijijini huwezi lala njaa hata kama hulimi ,unaweza kumpigia simu mkulima ukamwambia umemiss kula kwake na akachinja kuku kabisa maana anaona ufahari kutembelewa na kula na mwalimu /daktari/mtendaji hapo sijazungumzia mgambo wa kijiji .

Njooni kijijini mjini kugumu wazee huko mtaishia kuforsi kununua usafiri kama passo alafu mnauendesha usafiri wenyewe siku nne toka tarehe 23_28 hapo kamshahara kwisha habari yake wakati wa kijijini ni mwendo wa ugali na maharagwe hakuna cha chipsi wala burger sasa mshahara utaishaje kizembe hivyo .


Solution :kuwe na special allowance kwa watumishi wote wa vijiji sumbufu .

Samahani nimewananga sana watumishi wa mjini ila nyie ndiyo wajanja wa maisha bwana asikudanganye mtu au mnasemaje ?
 
Back
Top Bottom