Waandamanaji 10 wanaripotiwa kuuawa na polisi baada ya kuvamia jengo la Bunge la nchi hiyo na kuwashinda nguvu polisi.
Hali kwa sasa ni shwari kidogo baada ya polisi kuongeza nguvu ya idadi katika eneo hilo.
Sehemu moja ya jengo hilo la Bunge imeshika moto na moto huo bado waendelea.
Tukio hilo limetokea mara tu baada ya Bunge hilo kupitisha mswada wa sheria ya kodi inoongeza kodi katika bidhaa mbalimbali nchini huo.
Raisi Ruto amesema kuongeza kodi huko kutathibiti kukopa mikopo ambayo itaiathiri nchi hiyo kiuchumi.
Yadaiwa kuwa wabunge wengi walopitisha mswada huo wamepokea mlungula ili kurahisisha kupitishwa kwa muswaada huo ambao utaathiri wakenya wengi walo na kipato cha chini, wafanyabiashara na wachuuzi.
Kuna majeruhi wengi ambao wamejeruhiwa kwa risasi ambapo polisi waliamua kutumia nguvu na risasi halisi badala ya risasi za bandia au "rubber bullets".