Waandishi Wa Habari Mmetia Aibu Kwenye Press Baada Ya Mchezo Wa Young Africans Na Mamelod Sundowns

Waandishi Wa Habari Mmetia Aibu Kwenye Press Baada Ya Mchezo Wa Young Africans Na Mamelod Sundowns

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari.

Nimeamgalia Press Iliyofanyika Baadae Ya Mechi Ya Young Africans Na Mamelod Sundowns Hapa Kupitia Azamsports 2.
Ukweli Waandishi Wa Habari Wa Hizi Blog Na Media Nyingi Imeonesha Wanauwezo Mdogo Na Elimu Ndogo Katika Sector Hiyo Ya Habari.

Ukiachana Na Lugha Ya Kiingereza Kuwa Tatizo Kwao Pia Elimu Ni Ndogo Kwa Maoni Yangu Naona Wanaufinyu Wa Maarifa Kwenye Upande Wa Habari.


Hizi Press Waandishi Wa Habari Nawapa Rai Ya Kupitia Interview Za Walioendelea Kujifunza Kuuliza Maswali, Kila Kitu Kina Template Za Hizi Press Za Michezo Na Mashindano.


Watanzania Tuache Uvivu Wa Kusoma Maana Ni Aibu, Pale Tunapoonesha Ujinga Wetu Mbele Za Watu.


Kuboresha Sector Ya Habari Ianze Kwa Waandishi Wa Habari Wenyewe, Kwanza Kuongeza Maarifa Na Mambo Mengine Yatafata.

Ila Ukweli Kwa Press Ya Leo Ya Baada Ya Mechi Ya Young Africans Na Mamelod Sundowns, Waandishi Wa Habari Mmetutia Aibu.

Baadhi Ya Maswali Ambayo Waandishi Wa Habari Waliyotutia Aibu Ni Hivi:-

1. Kukosa Mpangilio Mzuri Wa Swali Husika (Swali Kukosa Maana) Hata Kama Limeulizwa Katika Lugha Ya Kiingereza. Maswali Karibu Yote Hayakuleta Dhima Halisi Ya Press Baada Ya Mchezo Ni Kama Waandishi Wa Habari Hawakujiandaa Kabisa.

2. Waandishi Wa Habari Kuuliza Maswali Yanayoleta Bias Kwa Kocha Na Wachezaji. Mfano Mwandishi Wa Kituo Kimoja (Blog) Ameuliza Kwanini Unamuamini Mzinze Kucheza Mchezo Wa Young Africans Dhidi Ya Mamelod Sundowns? Gamondi Ikabidi Amjibu Huku Akimshangaa Na Kumwambia Ni Mchezaji Mdogo Ambae Ni Future Ya Taifa La Tanzania Na Amefanya Attempt Nyingi Kuliko Shalulile.

3. Mwandishi Wa Habari Anaulizia Leg 2 Utakayochezwa South Africa Next Week Wakati Press Ni Summary Ya Mchezo Wa Leg 1 Uliochezwa Muda Mchache Uliopita.

4. Mwandishi Wa Habari Alipewa Nafasi Ya Kuuliza Maswali Sasa Wakati Anauliza Akauliza Swali Moja Pekee Kumbe Ana Maswali Zaidi Ya Moja Sasa Kocha Anamaliza Kumjibu Yule Mwandishi Akataka Kuuliza Swali Jingine Kama Interview Na Kuleta Mkanganyiko Kwa Waandishi Wa Habari Wengine.

5. Mambo Ni Mengi Ila Nitajitahidi Kutafuta Video Ila Sidhani Kama Itapatikana Maana Waandishi Wa Habari Watabebana Kuficha Hii Aibu.

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu
 
Aibu tupu, halafu wakikaa kwenye viredio vyao kujifanya wajuwaji sasa.

TASWA na TFF tafadhali waandalieni semina na mafunzo hawa waandishi uchwara wamelitia aibu Taifa.

Ni Bora hata wawe wanaandaa maswali Kwa kuandika ili waulize Kwa kusoma kuondowa hizi aibu Kwa kujifanya wajuwaji kumbe zero kabisa.

Cc: GENTAMYCINE piga spana hizi tutusa.
 
Aibu tupu kaka, mpaka Gamond anamuuliza mwandishi wewe ni journalist?

Tena issue ya Mzinze amwambie hiyo ni kijana mdogo NI hazina Kwa Tanzania na faida Kwa Tanzania ndio maana anampa nafasi.
duh sijaona aliuliza swali gani to get Gamond scorched kumuuliza mwandishi?
 
Hahahahaha sasa usikute aliyeuliza akajiona yeye ndio yeye
Leo wameaibika, labda Kwa watu wasiojuwa kingereza ndio hawaelewi aibu waliotuletea leo.

Halafu kumbe Manara naye ana TV? ndio najuwa Leo no wonder.

Mwakyembe alikuwa sahihi Sana kuweka regulations za waandishi lazima awe na elimu kuanzia Diploma Leo ndio nimemuelewa Mwakyembe.
 
......mbona malalamiko, kwani wameulizaje, wengine hatujafuatilia mahojiano, tuwekeeni video tushee hiyo fedhea, au lugha imekuwa changamoto hadi wametukana, anyway kingereza wengi wetu kinatushinda hata tuliobahatika kwenda shule.......
 
Leo wameaibika, labda Kwa watu wasiojuwa kingereza ndio hawaelewi aibu waliotuletea leo.

Halafu kumbe Manara naye ana TV? ndio najuwa Leo no wonder.

Mwakyembe alikuwa sahihi Sana kuweka regulations za waandishi lazima awe na elimu kuanzia Diploma Leo ndio nimemuelewa Mwakyembe.
Hahahahaha..Manara Tv ni TV ya mtandaoni tu ..anarekodi ana edit kisha ana upload YouTube, anaita Online TV 😆😆 sio diploma ilikua degreee kabisa na hii nakumbuka mtu aliyekua anaipinga ni marehemu RG kuwalinda vijana wake pale mjengoni kuwa vijana kweli hawana vyeti ila wana vipaji , ila sasa hawa TBC ambao wengi ni graduate ndio wanaandika na kutangaza hivyo..
 
Back
Top Bottom