Waandishi wa habari mnapata wapi ugumu wa kumuhoji Abdul juu ya sakata la fedha za mama Abdul?

Kiukweli umeandika upuuzi tu haujaeleweka kabisa kwasababu lissu kamtaja abdul na wenje nae kamtaja abdul sasa hapo uzushi unatokea wapi?
 
Kiukweli umeandika upuuzi tu haujaeleweka kabisa kwasababu lissu kamtaja abdul na wenje nae kamtaja abdul sasa hapo uzushi unatokea wapi?
Naomba twende mdogo mdogo。
  1. Umewasikia wewe mwenyewe kwa masikio yako au umehadithiwa tuu?
  2. Lissu amesema nini?
  3. Wenje amesema nini?
  4. Kati ya hao wawili kuna mmoja ni mkweli na mmoja ni muongo!。
  5. Mkweli ni yupi na kwa nini?
  6. Muongo ni yupi na kwanini?
  7. Abdul atafutwe ili aseme nini?.
P
 
Naomba twende mdogo mdogo。
  1. Umewasikia wewe mwenyewe kwa masikio yako au umehadithiwa tuu?
  2. Lissu amesema nini?
  3. Wenje amesema nini?
  4. Kati ya hao wawili kuna mmoja ni mkweli na mmoja ni muongo!。
  5. Mkweli ni yupi na kwa nini?
  6. Muongo ni yupi na kwanini?
  7. Abdul atafutwe ili aseme nini?.
P
 
Unataka Watekwe?
 

Abdul atafutwe aseme kipi sahihi kati ya vitu vifuatavyo.
i/ je, ni kweli alipelekwa kwa Tundu Lissu ili akamuhonge kama alivyosema Lissu mwenyewe?

Au alipelekwa kwa Tundu Lissu ili akamsaidie ili apate fedha zake ambazo alikuwa hajalipwa kama alivyosemwa Wenje?

Au hakuna tukio la Abdul kupelekwa kwa Tundu Lissu kama anavyosema Freeman Mbowe?
 
Thubutuu,hili nimelijifunza kwenye siasa za amerika tangu 2020 hadi 2024.Ujue hii habari ya vyombo vya habari vinavyoweza kutumika vibaya.Ilimlazimu Mzee Trumpet aanzishe Truth social media,Tweeter inunuliwe na Elon Musk,bbc,voa,dw,france intl na upuuzi mwingi kupuuzwa.Hata rfa leo anajua alivyopoteza wasikilizaji waliokuwa na imani na zile intenational media walivyo zipuuza.
 
Mtu kama Deodatus Balile ambaye kila leo yuko kwenye trip za mama, anakula mema ya nchi, ataanzaje kumhoji Abdul kuhusu pesa chafu anazopenyeza kuua upinzani? Unataka akate tawi alilolikalia? Hii haiwezekani kamwe! Kwa sasa hakuna waandishi Tanzania wanaoweza kuhoji masuala mazito yanayohusu ufisadi. Hakuna kaliba ya waandishi wa jamii ya Johnson Mbwambo, Jenerali Ulimwengu, Joseph Mihangwa, Profesa Bwenge nk. Mtu kama Maggid Mjengwa utegemee ahoji masuala manene kaa haya wakati ni kada mtiifu wa CCM?
 
Nakuunga mkono kaka. Baada ya media kubwa kubeba propaganda za kumponda Trump, Elon aliinunua Twitter na kugeuza upepo. The same happened kwa JK, alipoona magazeti ya Mtanzania na Rai yanatoa habari ambazo hazipendi ama hapendi kuzisikia, akaweka deal na Rostam, Rostam akainunua kampuni nzima ya Habari Corporation na kuyaua magazeti husika. Kupata independent media house Tanzania kwa sasa ni ngumu sana, ni kama kusaka mwanamke bikra ndani ya wadi ya wazazi.
 
TAKUKURU
 

Acha kujifanya uko Marekani au Uingereza. Hivi unadhani huyo Abdul ni Masha Love kwamba kwa simu moja tu unampata unafanya nae interview?

Kabla hujatukana taaluma za watu angalia na context ya nchi yako.

Kumpata tu Waziri kwenda kushiriki kwenye space zinazoandaliwa na LHRC huko X ni mtihani sembuse huyo Abdul ambaye ana tuhuma nzito hivyo?

Hii sio Marekani
 

Jiwe na Nape waliua kabisa ethical journalism ya nchi hii
 

Hukuwahi kumsikia Lissu akisema kuhusu hili, au kwa sababu siyo kada?

Nakumbuka moja ya mabandiko yako enzi za jiwe kutaka kukanusha vyombo vya habari vya nje kuhusu mapungufu yaliyokuwa yanatolewa ya jiwe. Au Lissu ni mzushi pia ambaye habari zake ni za uzushi kama wapinzani walivyo wazushi?
 
Unamaanusha nchi imetengeneza chawa wengi kiasi kwamba ufanisi wa watanzania na taaluma zao umepotea.
 
P Kwangu mimi nafikiri huo utakuwa uoga,kawaida na jua mwanahabari anasikiliza pande zote kisha anaunda habari.Vipi iweje usikilize akina TL na Wenje pekee kwanini na Ankolee asipewe haki ya kusikilizwa?
 
Fanya wewe tuone au ethics za kazi yako kule zinaku limit?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…