Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...

Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...

Mkuu asante kwa kuwakumbuka mashujaa wa habari. Sisi (mimi na wewe) tunajua nini maana ya kuwa mwandishi wa habari. Nakusihi bado kuwa mwandishi kwa maana ya mwandishi wa habari kuliko kuwa mtumwa wa nafsi yako. Tumkumbuke pia Marini Hassan. Mungu tu ndiye anayejua sababu za kifo chake.
 
Mtu yeyeto aliyeelimika na kustaarabika hawezi uwa mtu ili akamilike hii uleta Sana shaka juu ya elimu ya mtu.
Killing ufanywa na barbarian, uncivilized society.

Ukijua maana ya universe kila mmoja ni maiti mtarajiwa, Ingekuwa killing ni kinga ya kifo kina moi,Banda,bokasa,mobutu,nguema, Saddam, mobutu ,Abacha nk wangeishi.Lkn nao hawapo wamekimbiza upepo wameacha vyote duniani.Ukifika miaka ya 80 ndo utajua maisha ya dunia ni kuukimbiza upepo,unasumbukia nn.
 
Paskali umenikumbusha mbali, 2015 japo sio zamani sana wakati JPM, PM Kasim Majaliwa na aliekuwa Chief Secretary Amb. Sefue wakiendesha serikali pasi kuwepo baraza la mawaziri kwa ziara za kushtukiza.

Haya mahojiano niliyaona na najiuliza, Anganieli Mpendu kaenda wapi? (Kastaafu au..??) Niwapo pole tena wanahabari kwa kuondoka kwa Joseph Isango. Sisi (waandishi tusio rasmi) tunaishi kwa tahadhari kwasababu uoga nao ni akili. Misaafu inasema "The prudent (sensible person) sees the evil and hides himself, But the naive go on, and are punished for it." Prov 22:3

Tanzania ndiyo hatutimiza hata miaka 60 ya kujitawala. Martin Luther King ameuwawa miaka 192 tokea Uhuru wa Marekani uliopatikana 1776. Nini nataka kusema, uhai wa mwanadamu ikijumuisha wanahabari ni mkubwa kuliko kuwachokonoa wakubwa. Jamal Khashoggi ameuwawa baada ya kuwaudhi wakubwa wa Saudia

In principle, itachukuwa muda sio mfupi huenda kizazi chetu kikaisha ndipo uhuru wa wanahabari ambao watu wa Marekani wanao ukawepo.

Kwasasa ni busara kuishi in the name of "Hail is the King" tuishi kwanza na "kukosoa kwa staha". Ila kama kuna mwanahabari ambae ana wito kama wa akina Martin Luther King wa kusema, kuandika hata mambo ya chumbani, unaweza kuishia kupanda juu ya mlima ukaiona nchi ya ahadi na ukashindwa kufika kama Musa.

Tuendeelee kuishi kwa tahadhari (kwa kutumia "satnaizer" nyakati hizi za kuandika) maana kuna watu wako trained "kuondoa" watu wengine wakiwa na hisia tu umewaudhi wakubwa hata kama wakubwa bila shaka hawajaudhika na habari iliyotoka.
 
Usiogope kifo ni sehemu ya maisha,kuuliwa awajaanza leo Wala killing haijawahi zuia Siri zisifikie jamii,maana kuna third eyes watching every step Kama satellite ifanyavo kazi.

Wawezafanya siri kumbe upo uchi.Hakuna mwanadamu yeyeto duniani aliyeweza kuwa juu ya dunia.Atafanywa mbwembwe zote maringo yote kujimwambafy kote nk at the end atajiona yupo uchi.

Dunia imejengwa kwenye misingi yake ambayo ukiikiuka ni lzm ikuadhibu bila kujali who are you laws of nature inatambua mtu as mtu na si cheo , umaarufu, utajiri, madaraka, maana kila mtu amebeba laana na baraka ya maisha yake
 
Duh umeandika kwamasikitiko sana mpaka huruma hasa Aya mbili zamwisho.

Kwani mkuu nawewe nimwandishi wahabari zakiuchunguzi? Kwanini sasa usiache tu mkuu?

Maana wabongo niwanafki sana..... Wanamisemo yao eti 'kila mchuma janga hula nanduguze' mara utasikia 'sumu haijaribiwi kwaulimi' mara 'mtoto akililia wembe mpatie'.

Mda huo walishasahau kama walikuwa wanafurahia machapisho/interview zako.

Mda huo wewe upo jera au udongoni. Familia yako ipo kwenye majonzi mazito, wapo njia panda tena mbaya zaidi uwe umepotea bila hata mwili wako kuonekana ndio kabisa unawaacha njia panda ya barabara 24 kama ipo.

Waandishi wahabari, wanasiasa nawanaharakati wengine ndugu zenu tunawapenda sana ila msije kuhatarisha maisha yenu kwasababu yetu, msije kuhatarisha maisha yenu kwaugali mnaotutafutia sisi maana kuna hatari mbeleni mkatuachia majonzi mazito kuliko hii furaha mnayotupatia kipindi hiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mayalla tumekuelewa !! Uhai ni zawadi pekee ambayo ukipokonywa hakuna anayeweza kukurudishia.

Ila usiache kunawa mikono na maji tiririka mara kwa mara ili kujikinga na Corona.
 
Aisee... inasikitisha sana, mimi nakaa karibu sana na Isango na ni jirani yangu, nikimkumbuka alivyokua anatutetea hapa kisasida aisee Mungu ndio anajua, kifo chake kimetuacha na mswali mengi, tumebaki wanyonge hapa, tulimtegemea kwenye vitu vingi sana, alikua ni jicho letu na mkombozi wetu, hua naumia sana nikisoma mabandiko yake humu, Mungu amuondolelee dhambi huyu alikua ni shujaa!
asante pascal kwa kuwakumbuka hawa mashujaa!
 
Mbona ni kama unawatisha wengine.

Ila nijuavyo mimi kazi nyingine ni kama kujitoa muhanga, na kila anayechagua upande huo basi "ameshaagana na nyonga" na yupo tayari kwa lolote.

Aliwahi kuimba Marijani Rajabu "kila mtenda wema atakumbukwa kwa wema" na mstari mwingine akasema "afadhali ya kufa kuliko kunyanyaswa"

(hivyo ikitokea mtu aliyekuwa very critical on the status quo, ghafla akageuka na kuanza kuunga mkono juhudi, nawaombezi sana muwaelewe watu wa aina hii ambao hawaangalii leo au sasa bali wanaangalia mbali.)

Hapo kwenye red unanikumbusha 'nguli' mmoja wa habari ambaye sasa hivi ni Mtumishi kiongozi wa Uma kwenye moja ya Wilaya za huko Kaskazini...kwa jina ni somebody Mura (sina uhakika kama nimepatia hilo jina lake la ukoo) alivyokuwa machachari mpaka alivyowafotoa Maafande wanavyopokea pesa za kubrashia viatu barabarani..kilichomkuta hakuna hata aliyesimama naye, matokeo yake akapotea kabisa kwenye anga zile za 'habari za kiuchunguzi'
 
Ni kweli ulichoandika hapo kinasikitisha sana,hasa watu wanapokuwa wanatumia taaluma yao ili kutoa habari zenye ukweli ili kufichua madudu. Mfano umekumbusha Kifo Stan Katabalo ambae wakati anajitoa mhanga ili kuibua madudu kwa manufaa ya taifa letu. Ila pia nimefuatilia nyuzi nyingi za mikasa iliyompata mwandishi wa habari Josephat Isango(Rip) ilikuwa ni kipindi cha awamu ya nne. Yaani kipindi cha awamu ya Jakaya Kikwete.

Lakini kwa nia njema tu mtoa mada pamoja na kuwa kweli zipo tawala dhalimu ambazo huwa zinakandamiza waandishi wa habari. Lakini pia tusiangalie sarafu upande mmoja.Wapo waandishi wa habari ambao hutumia taaluma yao vibaya kwa manufaa ya kikundi flani au wanasiasa flani hivyo kupelekea kujikuta wanaingia kwenye matatizo na wenye mamlaka.

Nafikiri ni wazi.kabisa taaluma yenu inataka msiwe bias. Kama unaandika habari usiwe mtu wa kulalia upande mmoja ili kuepukana na kadhia zisizo za lazima. Naandika hivi sio kwamba nafurahia mabaya yawakute waandiahi wa habari. Bali wafanye kazi kwa maadili ili kuepuka ushabiki wa kisiasa ambao unaweza kuharibu kazi zao.

Pia kuhusu waandishi wa habari kutokuwa na weredi wa kuandika habari za masuala ya kisheria nakubaliana na wewe kabisa. Amepotea Azory Gwanda na Ben Saanane. Habari kubwa ni kulaumu watu wasiojulikana ambao moja kwa moja wanahusishwa na serikali. Lakini huwezi kuona mwandishi wa habari akimhoji mwanasheria yoyote kwamba kuna hatua gani ambazo zinaweza kuchukuliwa kisheria? Kama kweli serikali na vyombo vyake ina husika kwa nini wanahabari hawataki kwenda mahakamani na kuweka writ ya Habeas Corpus ili kama vyombo vya dola vina hawa watu viwalete toka huko waliko? Kuliko kuwa na malalamiko ambayo hata maswali yake yapo gizani tu.
 
Back
Top Bottom