Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
- #81
Leo nimewakumbuka waandishi wa habari na kupotea/vifo vya kutatanisha, toka kwa Stan Katabalo, Ben Saanane, Azory Gwanda, Daudi Mwangosi, Josephat Isango, maajaliwa ya hatma za maisha yao, ni ama tuombe Mungu atunusuru na dhahama hizo, ama...
RIP Wanahabari wote waliotangulia mbele ya haki na Mungu uwanusuru wale waliopotea bila sisi kujua hatma zao, na naamini kabisa bila shaka yoyote kuwa karma Itawashughulikia wahusika wa matukio hayo, huku sisi ambao bado tuko kwenye fani kiugumu ugumu, and we are still surviving, Mungu atajaalie moyo wa uvumilivu, ustahimilivu, na ufuatiliaji, tuwatembelee kujua majaaliwa ya familia zao.
Paskali
Mkuu Mwanamageuko , karibu pande hizi, ili ushuhudie utetezi wa haki, sikuanza leo!.Je Mkuu wadhani Mungu halipi? Ama wadhani uhalifu au udhalimu unaolindwa na wanadamu huwa haulipwi? Sihitaji kukumbusha mengi ila jiweke kwenye familia za Azory Gwanda, Ben Saanane, na wengineo wengi ambao tunawajua na tusiowajua ambao walinyanyaswa na walinyanyasika huku 'media na raia wakitazama na wengine kushangilia madhila"
P.