Waandishi wa habari Tanzania hamjitambui

Waandishi wa habari Tanzania hamjitambui

Alipotea Azory Gwanda mpaka leo hamjachukua hatua yeyote

Kwanini msichukue hatua kwa vitendo kusitisha kutangaza habari yeyote inayohusu Serikali mpaka mwenzenu apatikane?

Angalia reaction yenu mbovu kukamatwa kwa Kabendera mmeshindwa hata kumchangia pesa ya matibabu mama yake mpaka amekufa?

Kutwa kujipendekeza kwa madicteta. waandishi wa habari hamjitambui najua mtakuja kunishambulia ila ukweli unauma.

Majanga ni ya kila mtu hata wewe unajipendekeza kwa mtu uenda kesho ukakutana na majanga unafikiri nani atakusikia?

"Goes Around Come Around"
Wanabodi,
Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, kila mwaka sisi waandishi huwa tunakutana mahali kwa siku 2 na kujadili mambo mbalimbali kuhusu uhuru wa habari, na katika mkusanyiko huo, serikali, vyama vya habari na Taasisi za habari hutoa matamko kede kede kuhusu uhuru wa habari, lakini kwa mwaka huu, kufuatia janga la Corona, hakuna maadhimisho yoyote rasmi ya kukutana, ila nilitegemea wizara ya habari, vyama vya habari na mashirika na Taasisi za habari zitoe matamko mbalimbali.

Bado sijabahatika kuona tamko lolote!, ila usikute zile speech huwa zinaandaliwa kwa ajili ya presentations kwenye kongamano hotelini, safari na per diem!, leo hakuna safari, no trip, no per diem, no hotel gathering, hivyo this time hata speech tuu hakuna?!.

Nawatakia waandishi wenzangu, maadhimisho haya ya kimya kimya, nawashauri wale wafadhili mbalimbali wa tukio hili, kwa vile hatukusafiri, wala kula na kulala hotelini, then naomba hao wafadhili watutumie tuu hizo per diem, tutahama majumbani mwetu na kuhamia hotelini 3 days kisha tutatoa matamko.

Paskali
 
Back
Top Bottom