Waandishi wa habari wa Tanzania, baadhi wasivyojua namna ya kusimamia maudhui ya taarifa za viongozi wa juu kama Raisi

Mkuu,

Ni kweli 5 W hazijakamikishwa.

Lakini huoni kwamba hii ni habari ya awali kabisa baada ya tukio, na tunaambiwa wataalamu wa miamba watatafiti, na hivyo labda tunatakiwa kushukuru tu hata kwa Millard Ayo kuwapo sehemu ya tukio na kutupa tukio lilivyotokea tu, na sasa wengine wanaweza kutumia video hii kufanya uchambuzi zaidi?

Yani angalau tumepata hata video ya first account kutoka kwa wanakijiji, viongozinwa kijiji na mkuu wa wilaya.

Huoni kwamba hapa huwezi kukamilisha 5W, take what for example, huwezi kusema what really happenned zaidi ya walivyosema hao wananchi ku describe mlipuko, kwa sababu hata uchunguzi wa kitaalamu haujakamilika, na hicho ndicho pretty much alichosema Mkuu wa Wilaya?
 
I'm going meta.

Uzi huu unaonesha matatizo kadhaa ya kiutamaduni ya Watanzania wengi.

1. Kupenda usiri usio na sababu nzuri za kimantiki.

2. Kupenda ku defer to na ku protect the powerful.

3. Kupenda kuficha tatizo, badala ya kutatua tatizo.

4. Kupenda kulaumu mtu mdogo, hata pale mkubwa anapokuwa kakosea.

5. Kupenda kutafuta majibu rahisi kwenye maswali magumu.

6. Kutofikiri kwa kina na kidhahania.

7. Kupenda jeshi kwa hisia bila kufuata mantiki.

8. Kudogosha haki ya watu kujua habari muhimu za jinsi nchi yao inavyokwenda.

9. Kupenda kwenda kwa matukio badala ya kufikiri kimfumo.

10. Kutothamini nguvu ya uwazi katika kuanika matatizo na kubadili mambo kimfumo.
 
Bongo kuna waandishi wa habari??Au kuna vilaza wa habari?? Mie uwa nacheka sana nikiwaangalia akina zembwela, kitenge na vilaza wenzao. Hii sector kwa kifupi imekosa watu wa ukweli, wengi ni wababaishaji tu waganga njaa sasa hiki ulichokiongea watakijulia wapi???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…