Tetesi: 'Waandishi wa Makonda' kwenda Ziarani Koromije

Tetesi: 'Waandishi wa Makonda' kwenda Ziarani Koromije

Hivi huwa kuna ugumu gani wa mtu kuuliza source ya habari?,mtu anakaa nyuma ya keyboard au anapitiwa na usingizi baada ya saa moja anazinduka na ndoto na kuileta humu na nyie mnaanza kujibizana,hivi hamjiulizi hii habari inatoka wapi?,hawa watunzi wa story na uzushi ndo wanazingua hapa JF.Kama gazeti kubwa kama TZ daima limetuongopea Makonda yupo likizo SA miezi miwili,bado mnawaamini hawa manyumbu wanaoleta tetesi za kuota humu?
 
Hivi haiwezekani mtu binafsi kufungua kesi dhidi ya mtu aliyeghushi vyeti ni mpaka jamhuri tu ndiyo inayoweza kumfungulia mashitaka?

Wataalam wa sheria hebu nisaidieni hili
 
Kiongozi wa Mkoa anayesemekana kutumia jina lisilo lake ameandaa ziara ya Waandishi 10 watakaondoka kesho kuelekea Mkoani Mwanza. Waandishi hawa watakuwa na kazi maalumu Jijini Mwanza, katika Sekondari ya Pamba na Kijijini Koromije.

Kulingana na hadidu za rejea za ziara hii, waandishi watakutanishwa na kuongea na ndugu pamoja na walezi wa Kiongozi wa Mkoa na watatembelea Sekondari ya Pamba—Mwanza. Katika Sekondari hii watapata wasaha wa kupewa taarifa mbalimbali kuhusu Kiongozi wa Mkoa na kuongea na uongozi wa Sekondari.

Baadaye waandishi wataelekea Kijijini Koromije ambako watatakiwa kuwahoji watu kulingana na orodha iliyotolewa na Kiongozi wa Mkoa.

Kazi itakamilika kwa kuandaa taarifa katika mifumo mbalimbali ya kieletroniki (maandishi, sauti na video) zitakazolenga kuonyesha kuwa yote yaliyosemwa na kushuhudiwa juu ya Kiongozi wa Mkoa ni uongo. Taarifa kamili kutoka katika ziara hii zitarushwa mitandaoni na kupelekwa kwenye vyombo vya habari.

Lengo la ziara hii si kuibua ukweli bali kutaka kuufanya ukweli uchanganyikiwe kama njia ya kufifisha sakata la “BASHITE” Ifahamike kwamba huu ni muendelezo wa mikakati ya Mwana Kipenzi cha Mfalme baada ya kufurahia keki ya mwaka mmoja madarakani. Nakuuliza; hivi mawaziri waliambiwa wakibainika kufanya sherehe baada ya kuteuliwa watafanywa nini?
Watapewa pipi na maji na kama wanakisukari mwafaa
 
Washaandika script sasa wanaenda location kushoot picha, sawa tutasubiri tuone jinsi editor alivyofanya yake.
La saba oyeeee!
Nalog off
 
Hakika huyu ni mwana kipenzi wa mfalme.

Kwahiyo ameandaa list ya watu wa kwenda kuhojiwa.
Na watu hao 'wameshajiandaa' kuhojiwa.
Hawa watu waache kutufanyia maigizo,huu ni upotevu wa rasilimali.
La saba oyeeee
Nalog off
 
Kasumba yote hii ya nini ? Unatoa vyeti mpaka cha ubatizo kelele zote unazimaliza kiulaini kama unanawa
 
Yote hayo ya nini siaweke vyeti mezani
Mmeanza kumwambia atoe vyeti lini? Kwahiyo mpk atoe vyeti ndio mthibitishe? Hivi mnategemea ajichome kisu mwenyewe kama kweli amefoji? Akili yenu ndogo sana.
 
La saba oyeeee
Nalog off

Tatizo lilopo ni sifa nyingi alizomwagiliwa na Rais sasa hapo inampa Rais kazi kubwa kumuondoa mara moja baada ya uchunguzi wa TISS, Criminal investigation department. TAKUKURU na Prof Ndalichako na mama Kairuki kutoa repoti zao kuhusu mr Bashite Daudi kutumia cheti cha mtu! Hii itakuwa ndo mwanzo wa downfall wa kiongozi mkuu kama atafumbia macho mambo ya forgery ya elimu na kazi kwa (presidential appointments)wateule wake!mbon Kitwanga ni wa kabila moja lakini hakusita kumtumbua!
 
kaka yupo anaogopa kujitokeza, inawezekana alishapigwa beat, yupo tabora ni mtangazaji wa redio 1, anajua akijitokeza bado vibano vitawageuka wote wa2
Kwahiyo mnategemea makonda atajichoma kisu mwenyewe kama kweli amefoji?
 
Njaa itakuponza ww! Kifupi mimi nimesoma Azania Sec O' mpaka A' level mwaka naujua mwenyewe na baadaye UDSM leo ukiniuliza Walimu wa pale Azania kuanzia Mchwampaka, Christian, Kwayu (Head Master), Matrey, Sanga, Amrani,na yule Refa aliyekula mpunga wa Azam waifunge Yanga, Primus, na Wanafunzi Sebastian Ndege, Bob Leo, Chief wengine wengi. Sasa muulize Bashite Akutajie angalau Walimu wanne wa shule anakodai alisoma kama hajaanza kupiga yowe la kilio kama mtoto anayelilia ziwa la mama yake
Umewahi kumuuliza?
 
Back
Top Bottom