Waarabu kushangilia huku wakipeperusha bendera ya Tanzania inatuma ujumbe gani?

Unamdanganya nani Pascali ?!. Lini hivi vitu vikawekwa wazi kwa waTanganyika ?!. Wasomi wa kibongo mmeiangusha sana nchi hii kwa njaa na uoga wenu. Bora hata wanasiasa na wanaharakati baadhi wanatuamsha.
 
Wanahamia kweye maeneo yao waliyogewa muda si murefu
Wamechoka kuka tende na mikate waja kula wali ndondo za malofa
 
🤣🤣 wanazigiri🤣🤣

Sijui mlitoka wapi na hawa watu.

Mungu usinyamaze.
 
Hao ni Watanzania walio kwenye mji mtakatifu Iraq walipokwenda kuhiji katika miji mitakatifu ya madhehebu ya Shia ya Najaf kulipo msikiti maarufu mtakatifu na Karbala kulipo kaburi la Imam Husayn .
Ulisikia wapi mtu anarnda kuhiji na bendera ya nchi yake?
 
Huwa naandika mara nyingi sana kuwa adui mkubwa wa Watanzania ni ujinga, wewe umeendelea kudhihirisha hilo, wajinga wenzako wengi watafata ujinga wako.

Sasa ulitaka wasishangilie kuuziwa bandari zote, wakati wewe umelala na ujinga wako?
Huu muungano na Tito Okello umetuletea matatizo makubwa sana. Na ambayo yaelekea hayarekebishiki.
 
Aile post hii thread alitakiwa afanye uchunguzi yakinifu halafu aje na majibu juu ya hicho kinachoendelea kwenye video.
La sivyo ni kuchanganya watanzania waone kama wanawindwa na waarabu.
 
Shia ni dhehebu hivyo haina lugha!

Shia kuwa ni dhehebu haizuii kuwa na lugha.

Wanatumia lugha kuu ya Iran kama lugha yao rasmi; Kifursi.

Kama ambavyo waislamu wote wasiokua Shia wanatumia Kiarabu kama lugha yao rasmi.
 
Ningekuwa nafahamu kiarabu ningetia neno ila sifahamu wacha nikae kwa kutulia.
 
Kitambo, huoni kila baada ya mda flan anasubmit report anatua Kwanza anaacha ndege yake pale anachukua nyngn kuelekea ujombani
dah inawezekana lakini. Kuna factors ukijaribu kuzi combine kwa jicho la tatu unajua kuna jambo
 
Jamani tuepuke propaganda hao ni waislamu wa kishia wako kwenye ibaada uko Iraqi, hapa Tanzania kuna jamii ya kishia waismailia wapatao zaidi ya 200k, na wengi wao ni watanzania wenye asili ya waarabu Persians na Africa wachache.
 
Hao ni Watanzania walio kwenye mji mtakatifu Iraq walipokwenda kuhiji katika miji mitakatifu ya madhehebu ya Shia ya Najaf kulipo msikiti maarufu mtakatifu na Karbala kulipo kaburi la Imam Husayn .
Mji na msikiti mtakatifu kwa mujibu wa nani!?
 
Aile post hii thread alitakiwa afanye uchunguzi yakinifu halafu aje na majibu juu ya hicho kinachoendelea kwenye video.
La sivyo ni kuchanganya watanzania waone kama wanawindwa na waarabu.
DP World ndio imeleta haya yote
 
Kuna kosa Waarabu kupeperusha bendera ya Tz? Mbona Watanzania kibao huvaa nguo zenye bendera ya Marekani au kuweka bendera ya Israel kwenye magari yao na hujawahi kukemea hilo?
 
Umemjibu vizuri sana. Kaandika upumbavu tu kutokana na chuki na husda dhidi ya Waarabu na Waislamu.
 
hiyo ni majlis (religious gathering) ya mjukuu wa Mtume (S A W), aitwaye Hussein (A.S) ambaye alikufa Karbala kutetea uislam dhidi ya utawala dharim wa Yazid Bin Muhawia

so tusipotoshe umma ikiwezekana hii post yako uombe mods warekebishe heading, hii ni kuleta taharuki kwa mihemko yako.

hiyo bendera unayoiona ni baadhi ya watanzania walioenda huko iran na ikumbukwe uraia sio rangi ya ngozi.
na pia inaweza kuwa ni heshima kwa Tanzania kwani kiongozi wa mashia Afrika mashariki na kati makao makuu yake yapo Tanzania anaitwa Shkh.Hemed Jalala kama sijakosea.
 
Kuna tofauti gani kati ya washia na Qadiani/Ahmadiyya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…