Waarabu wa Afrika ni Waarabu au Waafrika?

Waarabu wa Afrika ni Waarabu au Waafrika?

Kwa mujibu wa takwimu, nchi za Kiarabu zipo 22. Kumi na mbili zipo bara la Asia na kumi zipo Afrika.

Zilizopo Afrika ni Algeria, Comoro, Djibouti, Misri, Libya, Mauritania, Morocco, Somalia, Sudan, na Tunisia.

Kwa kuwa inafahamika kuwa Afrika ina jumla ya nchi 54, waliopo kwenye hizo nchi 10 za Kiarabu wanajitambulisha kama Waafrika au Waarabu?

Kukitokea mgongano wa kimaslahi kati ya nchi za Kiafrika na Kiarabu, nchi kumi za Kiarabu zilizopo Afrika zitaegemea upande gani?
Wamasai wa Kenya ni wamasai au wakenya?? Ongeza akili japo kidogo basi swali lako halina maana!!
 
Hivi thongeee ukweli tu,
Wale jamaa ni mapandikizi,sio waafrika kabisa,mfano Tunisia.

Na sisi kama africans inabidi tuwakatae,

ukishawakataa wewe ndio watakua sio waafrica? acha ubaguzi ndugu
 
Kuwa Mwarabu ni mila na tamaduni, siyo wa kutokea bara lipi wala siyo wa rangi ipi au dini ipi.

Ni sawa na kusema Mswahili.
Kwa hiyo unataka kusema Mtu yoyote anayefuata mila na tamaduni za waarabu basi ni mwarabu?
 
Mkuu sijui kwa nini watu wanadhani umeuliza swali la kijinga,but naona swali lako lina hoja ndani yake.
Na issue kama hizi ndio zinafanya watu tuhoji ilikuwa kuwa vipi Waisrael (whites) a.k.a Wazungu wakawa katikati ya nchi za kiarabu ambapo watu wake ni waarabu??

Mabara yaligawiwa kwa kufuta ethnic za watu,Waarabu waliopo Afrika asili yao ni Asia ambapo inajumuisha wachina,Indians,Korean,Japanese,Nepal, Mongolia na hawa watu ukiwaona wanendana kwa kila kitu.Huku Afrika walihamia tu-hivyo kuhamia huku hakuwafanyi wao kupoteza asili yao na kuwa Waarabu.

Wanaitwa Waafrika kwa kuwa wanaishi ndani ya bara la Afrika na hiyo ni kutokana na mgawanyo wa maeneo ya kiutawala but always watakuwa Waarabu.
 
Kabla ya mwaka 1948 kulikuwa hakuna nchi inayoitwa Israel.
 
Wamasai wa Kenya ni wamasai au wakenya?? Ongeza akili japo kidogo basi swali lako halina maana!!
Mkuu, umeshawahi kuhudhuria vikao vya mahakama? Hakuna swali la kipumbavu bali kunaweza kuwepo na majibu ya kipumbavu.

Swali unaloliona ni jepesi linaweza likawa ni humu sana kwa mwenzako, na like lililo gumu kwako linaweza likawa rahisi kwake.

Muhimu ni kuwa mkarimu vya kutosha na kujaribu kuvivaa viatu vya mwuliza swali ili uweze kumpa jibu sahihi.
 
Sijakuelewa mkuu hapo mwisho! Wahindi ni wahindi na muda huo huo ni Waasia,
Wachina pia ni wachina na muda huo ni Waasia
Libya ni waarabu na muda huo ni waafrika!
Kwanini Libya wasiwe WaLibya na wawe waafrika?
unanipa mashaka degree yako ulisomea kijiwe cha breakpoint pale posta?
 
WAAFRIKA WA UARABUNI NI WAARABU AU WAAFRIKA?
Ushaambiwa muafrika siyo rangi bali asili ndiyo maana kuna waafrika wa rangi zote

Mfano Mmarekani mwenye asili ya Afrika
Kwahiyo kuna muafrika mwenye asili ya uarabu

Arabu ni asili siyo nchi kwa hiyo tutasema
M.Iran mwenye asili ya Afrika
M.Iraq mwenye asili ya Afrika
Msaud Arabia mwenye asili ya Afrika

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom