Waarabu wanatuharibia mpira wa Ulaya

Waarabu wanatuharibia mpira wa Ulaya

Ruben Neves katika umri wa miaka 26 huku Barcelona wakiwa wanamuhitaji amechagua kwenda zake Uarabuni.

Huko Chelsea lundo la wachezaji wako mbioni kuelekea Uarabuni. Alianza Ngolo Kante, na sasa Koulibaly na golikipa Mendy muda wowote wataelekea Uarabuni.

Waarabu wamedhamiria kweli nina mashaka baada ya misimu michache wachezaji wengi wa daraja la juu watakuwa wanacheza huko uarabuni
Mwarabu amechukua nafasi ya mchina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saudia Arabia wameiga kile walichofanya china miaka michache iliyopita. Lundo la mastaa walikimbilia huko kufuata pesa. Watu kama Osca, Carrasco, Ramirez, Paulinho, nk wote walienda wakiwa bado vijana. Ila huko saudia wanaenda ambao umri ushawatupa.
Paulinho alirudi tena ulaya akakipiga pale barca. Carrasco akarudi tena Atletico Madrid. Ambopo mpaka sasa anakipiga pale. Osca inasemekana anataka kurudi ulaya.

hivyo basi wengi wa wanaoenda saudia ni wale ambao umri umeenda au viwango vimeshuka.
 
Mbona ligi na timu ya taifa ya Saudi imejaa watu weusi acha kukalili.

Kwanza nawashangaaga nyinyi mnao sema waarabu wanawadharau watu weusi hali ya kuwa waarabu ndo jamii pekee ya watu weupe wenye muingiliano mkubwa wa kimahusiano na watu weusi kuliko jamii nyingine.

watanzania wengi ni wabaguzi sana
 
Kwahiyo mafuta yanatumika kwenye Magari tu?

😀😀😀😀
Inatumika pia kama mali ghafi ya kutengenezea bidhaa mbalimbali lakini nchi mbalimbali zinazo zalisha mafuta tayari zimeshaanza kufanya "Diversification," hivyo usifikiri wenyewe ni wajinga na eti wewe wa hapo Tandika kwa Mchambia Chupa ndio una akili kuwazidi.
 
Binti mbona povu kama mgonjwa wa kifafa?

Halafu wewe unajua kila mwanaJF anaishi wapi sio?
 
Ruben neves tetesi za kutakwa na Barca kaanzisha wakala wake tu, Hana kiwango chochote acha aende uarabuni tu
Sio hana kiwango yule ni mtu na nusu ila kwa falasafa za barca haendani na mpira wa barca
 
Sio hana kiwango yule ni mtu na nusu ila kwa falasafa za barca haendani na mpira wa barca
Angekua Mtu na nusu miaka yote SITA Hio asingekaa wolves, hakuna mchezaji hapendi kua club kubwa na kucheza ucl... Lakini pale wolves ndo palikua saizi yake
 
Ruben Neves katika umri wa miaka 26 huku Barcelona wakiwa wanamuhitaji amechagua kwenda zake Uarabuni.

Huko Chelsea lundo la wachezaji wako mbioni kuelekea Uarabuni. Alianza Ngolo Kante, na sasa Koulibaly na golikipa Mendy muda wowote wataelekea Uarabuni.

Waarabu wamedhamiria kweli nina mashaka baada ya misimu michache wachezaji wengi wa daraja la juu watakuwa wanacheza huko uarabuni
Mwana Mfalme wa Saudia ameagiza vilabu viandae bajeti ya kuhakikisha wachezaji nyota 300 wa dunia wanaenda kucheza Ligi ya Saudia.
Kitakachofuata waafrika wote wataelekea Saudia
 
Watu wanataka pesa kijana hii ni dunia ya kibepari na ubepari unakulazimisha kuwa mbinafsi ulitaka neves abaki ulaya kukufurahisha ww tu?

Kumbuka ajira ya mpira ni ya muda mfupi tu na unapofikisha miaka 30 unaonekana umezeeka kwahyo zinapokuja pesa kama hizo hamna haja kuzikataa kwasababu mwisho wa siku pesa ni muhimu zaidi.

Alafu pia kwani wachezaji wanaotoka Africa, America na Asia wanapambana waende kucheza ulaya kwasababu ya nn kama sio kufata malisho mazuri kutoka ulaya ?
 
China na Marekani walishindwa
China hawajashindwa mbona mkuu, wao China wana project ya muda mrefu wakilenga kuanzia 2050 watawale soka sasa hapa wame fail vp?

Nchi kama China sio Africa wao wana mipango ya muda mrefu, sisi Africa hatuna dira hata maendeleo tu ya nchi. Lengo lao kwanza lilikua ni kuwavutia watu hasa watoto waupende mpira na ndiomana wakapeleka wachezaji maarufu kutoka ulaya
 
Ruben Neves katika umri wa miaka 26 huku Barcelona wakiwa wanamuhitaji amechagua kwenda zake Uarabuni.

Huko Chelsea lundo la wachezaji wako mbioni kuelekea Uarabuni. Alianza Ngolo Kante, na sasa Koulibaly na golikipa Mendy muda wowote wataelekea Uarabuni.

Waarabu wamedhamiria kweli nina mashaka baada ya misimu michache wachezaji wengi wa daraja la juu watakuwa wanacheza huko uarabuni
Pesa inaongea
 
Back
Top Bottom