Waarabuni wa Dubai waomba zabuni ya kuendesha Mabasi ya Mwendokasi

Hiyo sio mbaya, ila Cha muhimu wazawa wapate engagement Yao, umeona wapi nchi inaendeshwa na wageni tu wazawa wanaonekana hamnazo!? Government share 49% Locals 15, operator in power kama ni foreign company 36% tufike mahali tujione hata wazawa tunaweza, na kweli tunaweza!! Wenye biashara ya Dala Dala wawe first priority
 
Je ujenzi wa BRT ni PPP au PPP inaanzia kwenye uendeshaji tuu.
 
Sio rahisi ivyo kama unavyoongea ukifahamu masharti ya kuendesha miradi ya public transport huko unapotaja.

US njia za reli ya serikali ni hasara na mabasi ni hivyo hivyo.

U.K. faida ni ndogo sana na hayo masharti inataka mtu anaejiamini kweli kweli kuomba tender. Unalipia gharama za upkeep ya bus lane, unalipia pension ya wafanyakazi wote, mishahara mazuri na hizo hesabu zinatoka kwanza, unalipa kodi faida, kilichobaki bado unagawana na serikali.

Ukishindwa kutimiza masharti unakula fines za kuuwa biashara si ajabu ikazidi £100m+ ukishindwa wizara ina team ya wataalamu tayari kuichukua biashara na kuiendesha huku wakitafuta mwekezaji mwingine na wewe ulieshindwa utawakuta mahakamani wakidai chao.

Sio rahisi kama mnavyoongea ulaya wanaingia tu PPP masharti yake sikia ni balaa hasa UK na mlaji analindwa usijipangie tu nauli.

Tanzania sisi PPP zetu ni kugawa kama sandakalawe miradi ya serikali.
 
Hapa nimekuelewa. Ila wengine wanaongea bila ushahidi. Inaonesha kidogo we upita pita shule
 
Watz nionavyo wengi ni vichaa, takwimu zinasema ukiona kundi la watu kumi, sita kati yao ni hamnazo. Nashawishika kuungana na jaamaa anaedai shida ni kula ugali.

Unakuta mtu anacoster 2 marejesho analipa, anajenga nyumba, dereva anapata chake, konda, mpiga debe bila kusahau kodi inalipwa na gari service inapelekwa km kawa.

Kwanini tuamini hawa wapuuzi kila ki2 wamewekewa still wanafeli. Inafikirisha sana ktk watz 60mln tukose watu wa kuendesha hii kitu mpaka tuwape wageni haiingii akilini.
 
Saizi vimelegea kila kona?
 
Kwani unafikiri hao watanzania wenye uwezo wa kuendesha hiyo biashara hawapo huko serikalini.

Shida ni CCM, mamlaka ya teuzi na vyombo vya ulinzi.

Ukimsikiliza yule Dr aliengozo jopo la kupanga vitita vya NHIF. Hesabu alizokuwa anaongelea kwenye kupanga bei ndio hizo hizo za biashara ya mabasi (services costing).

Sasa yule sio mtu wa finance atakuwa kajifunza yale mambo kwenye management course ya udaktari, kama anajua hesabu za services costing ina maana anajua kutengeneza strategy na mifumo yote ya usimamizi wa biashara ya huduma ya afya.

Unataka kuniambia huko serikalini hakuna mtu mwingine mwenye skills hizo aliesoma business management akaendesha huduma ya mabasi kwa ufanisi.

I always say ukitaka kujua huko serikalini kuna waelevu sikiliza wataalamu wao au wakurugenzi wa wizara wengi ni very technical.

Shida ni watu wanao wąsimamia CCM hawana uwezo wala akili ya kujua mtu mwenye sifa zipi apewe shirika lipi na wala hawana uwezo wa kusimamia taasisi zao (mawaziri wanaopewa wizara husika) jumlisha na report za CAG ambazo awazifanyi kazi.

Ni kwamba kuna watu hawataki maendeleo tu si kwamba hakuna watu huko serikalini wakuendesha miradi ya serikali kwa ufanisi.
 
Binafsi kwangu mimi Huduma zote ziwe mali ya UMMA ingawa na watu binafsi ruksa kufanya wanachofanya haya mambo ya privatization kwenye Commanding Height za Country economy ni kupotoka hata UK nadhani waliokwenda huko kabla.... the results leaves a lot to be desired...;

Kwenye huduma ukimpa mtu Binafsi bado asipopata faida ni Kodi za wananchi ndio zitampa ruzuku aendelee kupata chake na shareholders wake...

 
Wapewe tu maana hakuna aliyejitokeza anayeweza ,vilevile kamahatuwez kujitawala wenyewe heri tutawaliwe
 

Kuna muarabu keshaandaliwa hapo.
 
Umenena vyema mkuu. Ok; Sasa walioko huko Serikalini hawasikilizwi, wakitoa ushauri wa Kitaalam , ushauri hauzingatiwi unatupiliwa mbali (ref CAG report) na wanasiasa walijiingiza humo wengine huwa na genda zao za siri za kuangushana. Kwa mantiki hiyo, ni bora kuwakwepa mazima. Inafikirisha sana kwamba maprofesa/PHd na wasomi nguli wengine wapo lakini ni kama wametulia vile na kuangalia game linakwendaje na mti utaangukia wapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…