Waasi wa M23 sasa waelekea mji wa Bukavu

Waasi wa M23 sasa waelekea mji wa Bukavu

31 January 2025
Goma, DR Congo

Exclusive mahojiano : Corneille Nangaa kiongozi wa M23 walipotekwa Goma, azungumzia kuhusu FDLR na kitakachofuata...tunaelekea Bukavu hadi Kinshasa...

View: https://m.youtube.com/watch?v=7gHSPju7orY
Corneille Nangaa, kiongozi wa kisiasa wa waasi wa AFC / M23, aliketi na timu ya The New Times mjini Goma, kwa mazungumzo kuhusu mafanikio na shabaha walioitimiza ya kuuteka kwao mji huo wa kimkakati wa Goma , ufisadi nchini DR Congo na hatua ya mwelekeo mwingine katika mapigano yao... baada ya kuitia kibindoni mji wa Goma sasa vuguvungu (movement) inaelekezwa ..

TOKA MAKTABA :

17 December 2023

Tamko la Bw. Corneille Nangaa aliyepata kuwa mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya nchini kwake DR Congo



View: https://m.youtube.com/watch?v=l-UKfwrc2lI

Bw. Corneille Nangaa wa muungano wa the Congo River Alliance akiwa mjini Nairobi, Kenya ametoa tamko zito kwa WaCongolee, Jumuiya ya Ukanda huu, Bara la Afrika na ulimwenguni kwa ujumla lililotikisa serikali Kinshasa Congo hadi ikaamua kuwaita mabalozi wake waliopo Kenya na Tanzania kurudi nyumbani.

Ni tuhuma za serikali ya Kinshasa kufadhili na kutumia rasilimali za dola kuendesha mauaji, ufisadi, kunyakua ardhi za raia, ukabila, uhujumu uchumi na kutumia vita kama nyezo ya kujinufaisha kiuchumi wa binafsi na kuuteka nyara uchaguzi mzima wa December 2023.
1703436179969.png

Tumeamua kuja pamoja kama muungano wa the Congo River Alliance kusimama kupinga mambo haya maovu yanayoratibiwa kutoka Kinshasa chini ya utawala wa rais Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo uliopo Kinshasa.

Kenya ilinawa mikono na kukataa kukamata viongozi wa upinzani wa DR Congo na kusisitiza mazungumzo baina ya makundi na serikali ya Kinshasa ndiyo suluhisho la amani kupatikana Congo

TOKA MAKTABA:

December 16, 2023
Fukuto la kidiplomasia ndani ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki
Nchi kongwe za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki yaani Kenya na Tanzania zasema nchi ngeni kabla ya kuingia katika Jumuiya ya EAC zipigwe msasa kupitia semina ndefu

16 December 2023
DR Congo yawaita mabalozi wake waliopo Kenya na Tanzania nyumbani

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliwaita mabalozi wake kutoka Kenya na Tanzania kwa mashauriano siku ya Jumamosi, baada ya muungano mpya wa kijeshi wa Kongo unaojumuisha waasi kuzinduliwa katika mji mkuu wa Kenya.

Alain Tshibanda, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Kongo, alitoa tangazo hilo kwenye mtandao wa kijamii wa X, uliokuwa ukiitwa Twitter.

Balozi huyo nchini Tanzania aliitwa tena kwa sababu Tanzania ni mwenyeji wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo Kongo ni mwanachama hai pia mdau wa Jumuiya hiyo katika kutoa michango na rasilimali fedha.

Mapema siku ya Jumamosi, mkuu wa ubalozi wa Kenya alikuwa ameitwa kwa wizara ya mambo ya nje mjini Kinshasa. Serikali ya Kenya haikuweza kupatikana mara moja kutoa maoni yake.

Siku ya Ijumaa, wanasiasa na makundi ya Kongo wakiwemo waasi wa M23, ambao wameteka eneo la mashariki mwa Kongo, na Bw. Corneille Nangaa, mkuu wa zamani wa tume ya uchaguzi ya Kongo, walizindua Muungano wa Mto Kongo mjini Nairobi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Nangaa, ambaye aliidhinishwa na Marekani kwa rushwa na kukwamisha uchaguzi wa 2018, alisema muungano huo utaleta pamoja makundi mbalimbali ya watu wenye silaha, wanamgambo, mashirika ya kijamii na kisiasa ya Kongo.

"Natafuta suluhu la kudumu; jumuiya zote lazima ziishi pamoja nchini Kongo," Nangaa aliiambia Reuters siku ya Jumamosi.

Kongo inatazamiwa kufanya uchaguzi wa rais na wabunge tarehe 20 Disemba.
Muungano huo mpya ni wasiwasi wa ziada katika eneo ambalo ukosefu wa usalama umeendelea kwa miongo kadhaa, ukichochewa na uhasama wa kikabila na mzozo wa ardhi na rasilimali na athari za kikanda.

Bintou Keita, mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Kongo, alisema katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba "anatiwa wasiwasi sana na kuundwa kwa jukwaa jipya la kisiasa na kijeshi.

Congo Recalls Envoys to Kenya and Tanzania Over Alliance Launch in Nairobi​

December 16, 2023 8:05 PM
Democratic Republic of Congo
KINSHASA, CONGO —
Democratic Republic of Congo recalled its ambassadors from Kenya and Tanzania for consultations on Saturday, after a new Congolese military alliance that includes rebels was launched in the Kenyan capital.
Alain Tshibanda, spokesperson for Congo's foreign ministry, made the announcement on the X social media platform, formerly called Twitter.
The envoy to Tanzania was recalled because Tanzania hosts the headquarters of the East African Community, which Congo also belongs to.
Earlier on Saturday, the Kenyan embassy's head of mission had been summoned to the foreign ministry in Kinshasa. The Kenyan government could not immediately be reached for comment.
On Friday, Congolese politicians and groups including the M23 rebels, who have seized territory in eastern Congo, and Corneille Nangaa, a former Congo election commission chief, launched the Congo River Alliance in Nairobi.
Speaking at the launch, Nangaa, who was sanctioned by the U.S. for corruption and obstructing the 2018 election, said the alliance would bring together various Congolese armed groups, militias, social and political organizations.
"I am looking for a lasting solution; all communities must live together in Congo," Nangaa told Reuters on Saturday.
Congo is due to hold presidential and legislative elections on December 20.
The new alliance is an additional concern in a region where insecurity has persisted for decades, fueled by ethnic rivalries and a tussle over land and resources with regional implications.
Bintou Keita, head of the United Nations peacekeeping mission in Congo, said in a post on social media platform X that she was "extremely concerned by the creation of a new political-military platform


View: https://m.youtube.com/watch?v=N7qW0ltxRc4
 
Binafsi ninhependa wachukue Nchi hiyo iwe KIVu Ili kuweka na stability japo suala hili ni gumu haliungwi mkono Kimataifa ila wanaweza jitemga kama Somaliland na maisha yakaenda.
Democratic Republic of Kivu inawezekana lakini kwanza wakamate Kinshasa halafu mpango upelekwe Bungeni ili Referendum ifanyike watu wa Kivu waulizwe kama wanaona Kinshasa ni mbali kiAdministration nina imani wengi watapiga kura kujitenga na ghasia za Kongo.

Au wapewe full Autonomy.
 
Kipindi hiki tutawajua wengi sana wanaojiita watanzania kumbe mioyo yao ipo Rwanda.

Ikiwemo wewe mleta Uzi.
 
Inasemekana Majeshi ya Burundi yameungana na FLDR na Interahamwe wanawasaka Watutsi wa Kongo kwa lengo la kumalizia kazi ya Hutu Power walioianza 1994.
 
Mbona wewe uko Tanzania lakini moyo wako uko na magaidi ya Hamas.
Hilo halihusishi taifa langu.

Lingehusisha taifa langu ningekuwa upande wa taifa langu.

Haiwezekani uharamia anaoufanya Rwanda ambao ni hatari kwa usalama wa nchi ya Tanzania ambayo unasema yako kisha wewe ukabaki ukamuunga mkono mhuni wa nchi nyengine anayetishia usalama wa taifa lako. Hilo halipo!

Na hukuanza leo wala jana! Nimekuona kwa muda mrefu tu. Alikuwa mrwanda mwenzako aliyeitwa wa kupuliza sasa umebaki wewe.

Wewe siyo Mtanzani, wewe ni Mrwanda. Na kama ukisema wewe ni mtanzania basi wa asili ya Rwanda. Kwa ufupi wewe ni mhaini wa taifa hili!

Na kwa tabia zenu mnazozionyesha humu hamfai kuaminiwa nyinyi. Kama ningekuwa na mamlaka ningewafuta wote uraia watanzania wenye asili ya Rwanda.
 
Hilo halihusishi taifa langu.

Lingehusisha taifa langu ningekuwa upande wa taifa langu.

Haiwezekani uharamia anaoufanya Rwanda ambao ni hatari kwa usalama wa nchi ya Tanzania ambayo unasema yako kisha wewe ukabaki ukamuunga mkono mhuni wa nchi nyengine anayetishia usalama wa taifa lako. Hilo halipo!

Na hukuanza leo wala jana! Nimekuona kwa muda mrefu tu. Alikuwa mrwanda mwenzako aliyeitwa wa kupuliza sasa umebaki wewe.

Wewe siyo Mtanzani, wewe ni Mrwanda. Na kama ukisema wewe ni mtanzania basi wa asili ya Rwanda. Kwa ufupi wewe ni mhaini wa taifa hili!

Na kwa tabia zenu mnazozionyesha humu hamfai kuaminiwa nyinyi. Kama ningekuwa na mamlaka ningewafuta wote uraia watanzania wenye asili ya Rwanda.
Unauhakika gani ni hatari kwa Tanzania??
 
Baada ya kujua kuwa M23 wako na Cornele Nangaa ,basi Felix Tshishekedi ana kazi nzito, hao waasi wanafika Lubumbashi muda si mrefu ,hii vita ishakua ngumu Kwa Felix
 
Baada ya kujua kuwa M23 wako na Cornele Nangaa ,basi Felix Tshishekedi ana kazi nzito, hao waasi wanafika Lubumbashi muda si mrefu ,hii vita ishakua ngumu Kwa Felix
Au yeye alidhani kama ya siku zote? Kumbe wenzake kwa sasa wamedhamiria?
 
Au yeye alidhani kama ya siku zote? Kumbe wenzake kwa sasa wamedhamiria?
Nadhani lile shambulio la kupindua lilikua jaribio tu ,Sasa wameona kuingia Kwa style Ile ni ngumu

Waamua kuja Kwa style hii ya kuasi na mbaya zaidi huko waliko anzia ndio siku zote ni njia rahisi kufika Lubumbashi
 
Back
Top Bottom