Wabongo Hawatumii Consultants vizuri ndio maana wengi wanafeli kwenye biashara

In case hujui Guardiola alicheza Barcelona na alikuwa ni mkata umeme hatari miaka ya 90 inawezekana ulikuwa mdogo sana ila Guardiola mpira anaujua kuucheza vizuri namba 6 mzee wa dimba
 

Mkuu,

Mifano unayotoa kwenye hii mada ni irrelevant.

Wewe kama ni consultant basi JUKUMU lako ni kuhakikisha unashawishi wateja waone umuhimu wako.

Si ndivyo?

Ukishindwa hilo na kuanza kulalamikia watanzania wewe ndiyo una shida kubwa.

Wafanyabiashara wa hapa Tz au nchi yoyote ile hawapo kwaajili yakukuonea wewe huruma au kwasababu eti wafanyabiashara wa America na Europe wanatumia consultation services.

Mfanyabiashara anachotaka ni results.

Kumbuka, money is attracted to value.

Kama watu hawaoni value haijalishi kiasi gani utawalaumu kamwe hawatahitaji huduma yako na hawatokupatia pesa [emoji383]

Ni rahisi tu kufahamu hili.
 
So hapa naona kwa nchi yetu Consultant ni kama Kishoka fulani ambaye TRA wakikuzingua yeye anaenda

Na hii ni kwamba hii nchi mfumo wa kodi bado unakuwa sio rasmi mfano leo TRA wanaweza amka na kuja kukujambisha tu ilkmradi
 


Wako wanaofanya biashara mradi kuche ..na wako wengine wanaelewa techniques za kufika level ya mbali...mie naongelea Hawa wakati na wadogo...!...means sijaona umuhimu wa wao kutafuta consultants
 
So hapa naona kwa nchi yetu Consultant ni kama Kishoka fulani ambaye TRA wakikuzingua yeye anaenda

Na hii ni kwamba hii nchi mfumo wa kodi bado unakuwa sio rasmi mfano leo TRA wanaweza amka na kuja kukujambisha tu ilkmradi

Tra wanajambisha vibaya Sana..esp huko interior .
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Hii ndio JF kuna wajuaji kama milioni hv
Wew kama consultant wa biashara je umewahi kuwatumi consultant wa kielimu,saikolojia ili waiongoze familia yako katika mafanikio ya kielimu, au wewe unataka utumiwe tu wakati wewe huwatumii wataalamu wa nyanja isio kuhusu.
 
Ni kweli mkuu wafanyabiashara wengi ni darasa la 7 ila wana tathmini za mbali ndio maana wanafikia hadi kumiliki viwanda au malori na mabasi kwa hyo sio vilaza.
Kutokana na hilo huwa hawapendi kusikiliza maneno mengi sana ya kumpanga bali wanataka vitendo(practical oriented things) hapo ndio mtapatana.
 
Umeshauri vema mkuu, naomba kukazia hapo uliposema ukiwa na mtaji chini ya 100m si lazima sana kuwa na consultant(s).

Kama unafanya biashara (nasisitiza biashara) sio umejiajiri, ni muhimu kuwa na consultant kuanzia level ya chini kwa sababu hizi:

1. Biashara inatazamiwa baada ya muda flani itakuwa na kufika level ya kati ama juu (Going concern concept).

2. Kama biashara haikujengwa kwenye misingi thabiti inaweza kushindwa kuzipokea na kuziishi idea mbalimbali zinazotolewa na Consultants hivyo kutofanikiwa na kisha watu kuona hakuna umuhimu wa consultation kumbe shida ni misingi ya biashara yako.

3. Consultation itakusaidia sana kwenye kukuza biashara kwa kuwa inakusaidia kujenga mifumo ya uendeshaji kuliko kufanya kila kitu wewe mwenyewe hivyo itakubidi uzuie biashara isikue ili uweze kuisimamia (kutaka kukumbatia kila kitu).

4. Biashara iliyojengwa kwenye consultation inalandana kimifumo na biashara zingine (mifumo ya uzalishaji, usambazaji, malipo, ordering, sales & marketing etc) hivyo kukuwezesha kutrade na partners wa kitaifa na kimataifa.
 
Matendo
Matendo yenye matokeo makubwa lazima yapitie kwenye maneno kwanza au maandishi...unapoona idea ya Azam ukwaju na Ballcone kuna mtu alianza kutoa maneno au maandishi.
 
Ndio mtaendelea kukaa benchi na kulaumu kila siku maana mmekaririshwa hamtaki kubadilika na kutumia mbinu mpya.
Huyo Azam hata kama anatumia,ameanza kutumia wakati ameshakuwa bilionea tayari.
Sidhani kwamba hayo makaratasi yenu ndio yalimfanya afanikiwe na kuwa bilionea
Matendo

Matendo yenye matokeo makubwa lazima yapitie kwenye maneno kwanza au maandishi...unapoona idea ya Azam ukwaju na Ballcone kuna mtu alianza kutoa maneno au maandishi.
 
In case hujui Guardiola alicheza Barcelona na alikuwa ni mkata umeme hatari miaka ya 90 inawezekana ulikuwa mdogo sana ila Guardiola mpira anaujua kuucheza vizuri namba 6 mzee wa dimba
Nimemtolea mfano sababu namjua Guardiola kama mchezaji na sasa kama kocha. In his playing days, he was regarded as the best midfielder of his geration by football legend Johan Cruyff.

Hata hivyo ni ukweli kwamba dunia ya mpira inamtambua Guardiola leo kwa kile alicho achieve as a coach na si akiwa mchezaji.

Maana yangu ni kuwa unaweza ukafanya jambo moja katika ngazi/nafasi fulani usifanikiwe kama ukifanya jambo hilo hilo katika ngazi/nafasi nyingine. Kwa hiyo mtoa mada anaweza asifanye maajabu sana kama mfanyabiashara lakini bado akafanya vema sana kama consultant.
 
So hapa naona kwa nchi yetu Consultant ni kama Kishoka fulani ambaye TRA wakikuzingua yeye anaenda

Na hii ni kwamba hii nchi mfumo wa kodi bado unakuwa sio rasmi mfano leo TRA wanaweza amka na kuja kukujambisha tu ilkmradi

Ni kwa kesi chache sana TRA wanaweza wakakutia kiwewe kwa makusudi either wajipatie chochote kutoka kwako au kwa kutumwa (huku mitaani kunakuwaga na uhasama wa kibiashara wakati mwengine) ila nyingi ni za mfanyabiashara mwenyewe kujisababishia,unakuta mimi kama mfanyabiashara nakwepa amma kwa kujua au kutojua adhabu zake najilimbikizia madeni siku wakiamka deni limekuwa kubwa so inabidi kukaa mezani kama sina point za maana nalipishwa ila consultant ana uwezo wa kuniwakilisha akatoa sababu mbili tatu atakazoona zinafaa ambazo mimi sizijui nikaambiwa nilipe bila fine na bado deni nikapunguziwa.

Yupo jamaa yangu kijana wake alitoa receipt ya Tsh 32,000,000 kwa mara moja asiambiwe lile kosa kwa wakati akaja kujua kupitia Z report ya EFD baada ya week na sheria inataka mistakenly report iwasilishwe TRA ndani ya 24 hrs kwenda yeye kama yeye wakasema ni sahihi as long as hawajui mtaji wake umeongezeka kwa kiwango gani labda asubiri mwaka wa makadirio unaofuata akate rufaa, akashauriwa awatafute consultants alisaidiwa akai-punch ile ngoma ila ilikuwa tayari inakula kwake.

Nadhani kinachomata ni kujua namna ya kupangilia maneno,wapo watu wakiingia TRA hata awe mchafu kiasi gani anasikilizwa na bil ilikuwa kubwa anapunguziwa anaandikiwa hela ndogo anaenda kulipa maisha yanaendelea so siyo kila mtu atamuhitaji consultant wanaowahitaji hawa watu ni wale waoga waoga.
 

Ndiyo ukweli wenyewe huo mkuu.

Wewe ukimwendea mfanyabiashara kwa maneno matupu atakupuuza tu hata kama utamwambia wewe ni graduate wa Harvard School of Business.

Tatizo hawa ndugu wanashindwa kutazama mambo kwa uhalisia wake.

Point muhimu yakutia kwenye kikapu na kwenda nayo home ni hii...

Wateja wanapenda kununua/kumpatia pesa mtu/consultant wanayemwamini anaweledi na amedhibitisha hivyo
 
Inawezekana unaona mfano wangu hauhusiani na mada kwa kuwa hujafatilia nilichokuwa namjibu muhusika.

Nilichokuwa namjibu muhusika ambaye alimtaka mtoa mada afanye biashara badala ya kufanya consultation ndipo nikamtolea mfano wa kocha huyo ambaye alikuwa mchezaji kabla na dunia haikumfahamu sana kwa mafanikio aliyopata in his playing days lakini alicho achieve leo kama kocha dunia nzima inamtambua.
 

Sawa mkuu,

Tupo pamoja.

Ni mjadala tu [emoji1674]
 
Sikupingi mkuu,hasa hiyo #3 kwa jicho la tatu nimeielewa sana.

Shukrani!
 
Nna kampuni nataka fungua.

Hii kampuni itasajiliwa tz na itakua inatoa huduma hasa nje ya nchi.

Je nikipata faida ya dola 1000 ni kodi gani nitatakiwa lipa kwa mwezi au kota?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…