Wabongo kwa kujiita C.E.O mitandaoni utafikiri hata wanajua maana na kirefu cha herufi hizi. Sio mbaya kujiinua ila huu ni ulimbukeni.

Wabongo kwa kujiita C.E.O mitandaoni utafikiri hata wanajua maana na kirefu cha herufi hizi. Sio mbaya kujiinua ila huu ni ulimbukeni.

Utakuta mtu ana genge lake,kijiwe chake eti anajiita CEO, ma meneja, mara bosi. Mbaya zaidi bodaboda nao wameanza kuitwa maofisa, eti maofisa usafirishaji, tena media kubwa zinang'ang'ana kuwaita hivyo wahuni hao wakati wao hawajiiti hivyo. Sasa wafanyakazi wa LATRA wataitwaje?
Haahhahah c.e.o anapitisha kapu achangiwe wakacheze ndondo mbagala
 
Mara utasoma " The cute baby mama"
C.E.O wa Ze Cute Outfits za warembo

Mara "Juma aka Simba mkali"
C.E.O wa simba fanicha kunduchi"

Maana halisi na ya kawaida ya C.EO ni mtu mkuu mwenye jukumu la kusimamia kampuni, ambaye wakati mwingine pia ni rais wa kampuni au mwenyekiti wa bodi. Tena hapo bado vile vitengo vya kuuza na utawala vinaongozwa na Makamu wa Rais Mwandamizi ambao huripoti moja kwa moja Mkurugenzi mtendaji.

Sasa wewe ndio C.E.O lakini wewe ndio mfagia ofisi, una zamu za kusafisha choo ulipopanga fremu, wewe ndio mteja akinunua bidhaa online unafunga ofisi kukimbia stendi kumtumia mzigo.

Wewe jiite mmiliki wa duka [Shop Owner], acha sifa, uongo na ulimbukeni.

Ishi kwa level yako, sasa ukijiitaa C.E.O sasa hivi what is next for you sasa, will you dare to dream for more.
Mkuu,

Inaonekana kama wanakuumiza sana wakipost hivyo eeh?

Watu wamenyimwa u CEO wa kweli, wewe unawanyima mpaka u CEO wa kujifurahisha wenyewe?

Mbona unakuwa mnoko hivyo?
 
Mkuu,

Inaonekana kama wanakuumiza sana wakipost hivyp eeh?

Watu wamenyimwa u CEO wa kweli, wewe unawanyima mpaka u CEO wa kujifurahisha wenyewe?

Mbona unakuwa mnoko hivyo?
Haha mimi ni mnoko ila sio mnonko zaidi ya C.E.O feki.

Unajiita ceo wakati una jiko unajipikia dukani kwa kuogopa gharama za mama ntilie haha
 
Chief Executive Officer ndie yeye na akiwa hayupo biashara itafungwa huenda ana ndoto kubwa ila kaanza kidogo
Sasa hapo unaleta maana yako pekee na una i-force iwe utakavyo. Goodluck.

YOU ARE A SHOP OWNER NOT A C.E.O

ACHENI MAZINGAOMBWE.
 
Mara utasoma " The cute baby mama"
C.E.O wa Ze Cute Outfits za warembo

Mara "Juma aka Simba mkali"
C.E.O wa simba fanicha kunduchi"

Maana halisi na ya kawaida ya C.EO ni mtu mkuu mwenye jukumu la kusimamia kampuni, ambaye wakati mwingine pia ni rais wa kampuni au mwenyekiti wa bodi. Tena hapo bado vile vitengo vya kuuza na utawala vinaongozwa na Makamu wa Rais Mwandamizi ambao huripoti moja kwa moja Mkurugenzi mtendaji.

Sasa wewe ndio C.E.O lakini wewe ndio mfagia ofisi, una zamu za kusafisha choo ulipopanga fremu, wewe ndio mteja akinunua bidhaa online unafunga ofisi kukimbia stendi kumtumia mzigo.

Wewe jiite mmiliki wa duka [Shop Owner], acha sifa, uongo na ulimbukeni.

Ishi kwa level yako, sasa ukijiitaa C.E.O sasa hivi what is next for you sasa, will you dare to dream for more.
Wanajitabiria.
 
Kabisa mkuu, udeal na TRA, Halmashauri na matawi yake, na ulipie fremu bado na wewe ubakiwe na ya kula halafu usiwe CEO?
Na u deal na wakopaji na wateja wanaosusa mara bidhaa kuadimika sokoni mara kupanda bei mara friji haligandishi mara umeme haupo siku nzima
Yani sio tu CEO ni Champion kabisa🙌🙌🙌
 
Back
Top Bottom