Aliyekwambia nina negativity nani?
Mimi nataka nifike Marekani na nataka wewe
Kiranga unisaidie.
Ishu ni kufika huko tu mambo mengine utaniachia mimi.
Haya twende kazi
Wewe ni sawa na yule mtu aliyeota ndoto.
Halafu akaenda kwa mtafsiri wa ndoto, akitaka atafsiriwe ndoto yake.
Mtafsiri wa ndoto akamuuliza, sawa, niambie ndoto yako nikutafsirie.
Badala ya kumwambia mtafsiri wa ndoto ndoto yako akutafsirie, unampa kazi ya ziada, unamwambia mtafsiri wa ndoto kwanza akuambie umeota nini, halafu aitafsiri hiyo ndoto.
Nakupa kanuni muhimu ya kusaidiwa.
Msaidie anayetaka kukusaidia, fanya kazi yake ya kukusaidia iwe rahisi, usimuongezee mzigo wa kufanya kazi ya ziada ya kutafuta akusaidiaje. Nenda kuomba msaada ukiwa unajua unataka kusaidiwa wapi.
Juzi nilikuwa katika kikao na Profesa mmoja Mtanzania yuko US anatoa michongo ya scholarship. Tuna network ya kusaidia wanafunzi kuja kusoma US.
Alisema kitu kimoja ambacho hapendi ni mtu kuja kumwambia anataka scholarship, bila detail.
That is too general, too vague.
Alisema anataka mtu amwambie kasoma nini, kafanya mitihani gani, kakwama wapi, anahitaji msaada wapi, yani mtu fulani ambaye yeye mwenyewe kashaonesha initiative, anajua anataka kufanya nini, anahitaji msaada kufika anapotaka kufika.
Sasa, hata tukiondoa mambo ya scholarships na usomi, wewe hujaonesha initiative, uko too vague, too general, yani, hata kwa mtu ambaye hana qualification yoyote, akiniambia hivyo anakuwa kanisaidia kujua anaingia kwenye michongo gani. Kuna safari zinafanywa na watu wenye uzito mkubwa Tanzania unaweza kupata.
Tatizo wewe hata initiative ya kuniambia una kipi, au huna kipi, hujafanya.
Unakuwa kama wale wanafunzi ambao huyo rafiki yangu profesa amesema hapendi kuwasikia, wanaosema "nitafutie scholarship" tu, bila detail.
Kwa mentality hii unaweza kufika Marekani ukatamani kurudi Tanzania tu. Marekani ni nchi inayotaka specificity.