Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Basi ndio umwambie hayo ili akusaidie, mimi huwa ninapata nafasi za kazi za gulf countries na watu kadhaa nimewaunganisha huko, pia huwa napata za Canada ila gharama zake huwa kubwa.Mkuu mimi elimu yangu ni form six ingawaje nilifeli.Nina leseni ya udereva class C hivyo kwenye suala la udereva niko vizuri.
Kuhusu passport ninayo,hiyo kadi ya chanjo ya covid pia ninayo,cheti ya chanjo ya homa ya manjano ninayo.
Kuhusu pesa siwezi kosa milioni 10.Hivyo ni yeye tu kunifanyia mpango niweze kufika huko
Hii kwa kiasi kikubwa inatokana na watu kuishi kwa mafungu kwa kutaka kupunguza gharama za maisha.kuchomeshana kisa umemzidi kipato kawaida ila kinachowagharimu watanzania ni kujuana sana kila mtanzania unayekutana nae ni ndugu
Sasa mtu unamuuliza qualifications, or lack of, ujue ana fit wapi, hata kukujibu hilo mgogoro.Basi ndio umwambie hayo ili akusaidie, mimi huwa ninapata nafasi za kazi za gulf countries na watu kadhaa nimewaunganisha huko, pia huwa napata za Canada ila gharama zake huwa kubwa.
Mkuu Kiranga mimi nina elimu ya kawaida,nilifika form 6 lakini nilifeli kwa ishu zilizosababishwa na mapenzi(Haya hayana umuhimu).Wewe ni sawa na yule mtu aliyeota ndoto.
Halafu akaenda kwa mtafsiri wa ndoto, akitaka atafsiriwe ndoto yake.
Mtafsiri wa ndoto akamuuliza, sawa, niambie ndoto yako nikutafsirie.
Badala ya kumwambia mtafsiri wa ndoto ndoto yako akutafsirie, unampa kazi ya ziada, unamwambia mtafsiri wa ndoto kwanza akuambie umeota nini, halafu aitafsiri hiyo ndoto.
Nakupa kanuni muhimu ya kusaidiwa.
Msaidie anayetaka kukusaidia, fanya kazi yake ya kukusaidia iwe rahisi, usimuongezee mzigo wa kufanya kazi ya ziada ya kutafuta akusaidiaje. Nenda kuomba msaada ukiwa unajua unataka kusaidiwa wapi.
Juzi nilikuwa katika kikao na Profesa mmoja Mtanzania yuko US anatoa michongo ya scholarship. Tuna network ya kusaidia wanafunzi kuja kusoma US.
Alisema kitu kimoja ambacho hapendi ni mtu kuja kumwambia anataka scholarship, bila detail.
That is too general, too vague.
Alisema anataka mtu amwambie kasoma nini, kafanya mitihani gani, kakwama wapi, anahitaji msaada wapi, yani mtu fulani ambaye yeye mwenyewe kashaonesha initiative, anajua anataka kufanya nini, anahitaji msaada kufika anapotaka kufika.
Sasa, hata tukiondoa mambo ya scholarships na usomi, wewe hujaonesha initiative, uko too vague, too general, yani, hata kwa mtu ambaye hana qualification yoyote, akiniambia hivyo anakuwa kanisaidia kujua anaingia kwenye michongo gani. Kuna safari zinafanywa na watu wenye uzito mkubwa Tanzania unaweza kupata.
Tatizo wewe hata initiative ya kuniambia una kipi, au huna kipi, hujafanya.
Unakuwa kama wale wanafunzi ambao huyo rafiki yangu profesa amesema hapendi kuwasikia, wanaosema "nitafutie scholarship" tu, bila detail.
Kwa mentality hii unaweza kufika Marekani ukatamani kurudi Tanzania tu. Marekani ni nchi inayotaka specificity.
Mimi ni muongo.Umesema mwenyewe. Hivyo siwezi kukusaidia.Mkuu Kiranga mimi nina elimu ya kawaida,nilifika form 6 lakini nilifeli kwa ishu zilizosababishwa na mapenzi(Haya hayana umuhimu).
Mimi ni dereva mzuri tu na nina miliki leseni daraja C,pia nina passport,kadi ya chanjo ya korona,kadi ya chanjo ya yellow fever.
Nahitaji kufika nje kwa fursa kama udereva lakini pia fursa yeyote ya unskilled mimi napiga,ishu ya pesa ya nauli kwangu siyo ishu.
Wewe niambie nifanye nini mimi nitafanya ili niweze kufika hapo
Safi hapo sasa umejieleza vizuri, now tumsikie mkuu Kiranga atajibu nini, itakuwa msaada kwa wengine pia.Mkuu Kiranga mimi nina elimu ya kawaida,nilifika form 6 lakini nilifeli kwa ishu zilizosababishwa na mapenzi(Haya hayana umuhimu).
Mimi ni dereva mzuri tu na nina miliki leseni daraja C,pia nina passport,kadi ya chanjo ya korona,kadi ya chanjo ya yellow fever.
Nahitaji kufika nje kwa fursa kama udereva lakini pia fursa yeyote ya unskilled mimi napiga,ishu ya pesa ya nauli kwangu siyo ishu.
Wewe niambie nifanye nini mimi nitafanya ili niweze kufika hapo
Wapi nimesema nataka urafiki na wewe?Kaa utulie mzee mimi si size yako wala sihitaji urafiki na wewe
Ebu toa hints za nini kifanyike ili uweze kutoa msaada kwa muhusika mwingineMimi ni muongo.Umesema mwenyewe. Hivyo siwezi kukusaidia.
Sasa mkuu mtu kashatoa hint Zote muhim anataka msaada afu unamlet down unataka abembelezwe wabongo au nyie ndo mnaopenda kusujudiwa..umughaka mbele utaend km ulivyoenda kongoEbu toa hints za nini kifanyike ili uweze kutoa msaada kwa muhusika mwingine
WaTz wachilia wa nje, hata wa ndani, ni jambo gani wanafanikisha kwa umoja wao? Chuki, husda, wizi na kuendekeza rushwa, mtindo mmoja, hakuna tofauti!Community za Wabongo nje hazina tija, ndio maana pamoja na wao kutaka uraia pacha, huoni umoja wao kwenye hilo.
Kwanza kabisa yeye mwenyewe ajue ana kipi, hana kipi, anataka kusaidiwa wapi.Ebu toa hints za nini kifanyike ili uweze kutoa msaada kwa muhusika mwingine
Wabongo wa mamtoni sio wa ku socialize nao.Siyo vizuri kuwa kisiwa. Ni vizuri kushosolaiz na kujichanganya kigumu hivyo hivyo.
Kuna nature kama kifo na kuuguwa. Japo mibongo mingi ni mitambo ya umbea hivyo hivyo tu itasaidia.
Lakini tabia zetu mtoni ni mbofumbofu na kukera.
Naona ni mchakato uanaohitaji ujitambue na ufahamu unachokitaka haswa. Kwa kunufaisha audience, ikiwa ulishaweka uzi wa mambo haya. Unaweza ku attach hapa ili tufahamu kwa undani baada ya hizi insights. ShukhuraniKwanza kabisa yeye mwenyewe ajue ana kipi, hana kipi, anataka kusaidiwa wapi.
Mfano.
Kuna watu wana degree ya kwanza, wanataka kusoma zaidi nje kwa njia ya scholarships, wanajua wamesoma field gani, wanajua wamefanya mitihani gani, au hata kama hawajui, hawa tunaweza kushauriana nao. Kuna network ya safari za mambo ya vyuo, scholarships, grants, loans etc.
Kuna watu hawana pa kufikia wala barua ya mualiko, wana safari za kijamii/kitalii wanahitaji barua ya mualiko itakayoonesha wana sehemu ya kufikia.
Kuna watu wana qualifications za kutafuta kazi zenye soko sana kimataifa, wanahitaji kujua jinsi ya kuunganishwa na makampuni ya kimataifa kufanya kazi.
Kitu muhimu ni mtu mwenyewe awe na idea ana kipi, anataka kufanya kipi, anataka msaada wapi, ana kipaji gani, mtu aanze kufanya homework yeye mwenyewe, si anataka kuja nje tu wakati hata yeye mwenyewe hajui anataka kufanya nini huko nje.
Sent from my SM-S908U1 using JamiiForums mobile app
Majungu hayo utakua huna tofauti naeKuna dogo flani nimeshawahi kuletaga uzi humu kitambo kidogo nadhani 2015 au 2016.
Dogo aliletwa mtoni akiwa mdogo kutoka bongo. Anapendaga kushindana na mimi hadi leo. Nampango wa kumuanzishia uzi humu jinsi nilivyomuwin kisaikolojia.
2009 nilipokuwa bado mgeni hapa dogo aliniudhi kichiz. Aliniambia sasa wote mkija huku nani atabaki bongo? Nilimaindi kichiz
Hadi akinunua kitanda ananiringia nabaki kushangaa kitanda tu mtoni jamani.
Kaeni mkao wa kula ntaleta uzi mwengine kumhusu karibuninilivyomuwin kisaikolojia nakumnyamazisha
Kutawaliwa ni matokeo ya wazee wliokuwa ma snitch, zile meli za arabs zilikuwa zikitia nanga pwani vijana wa kibantu wanaenda kuwatafuta na kuwawinda vijana wenzao kuwauza kwa arabs na whites, wanapewa fedha,hovyo kabisa.Ktk historia wazee wetu walioongoza mapigano au aina yoyote ya kukataa udhalimu kutoka kwa wakoloni walisalitiwa na baadhi ya wazee wetu mfano mdogo tu ni mfanyabiashara maarufu wa pwani BWANA HERI ambae alikua mstari wa mbele kupinga wakoloni wa kijerumani alinyongwa ktk mwembe uitwao mwembe kinyonga pale korogwe baada ya kukamatwa akiwa mafichoni huko Dodoma hivyo majungu na kusalitiana hapa bongo ni sehemu ya maisha.
Wabongo wengi wana matatizo ya ego na mashindano.Majungu hayo utakua huna tofauti nae
Jibu yale maswali yake mkuu.Hiyo visa unaweza kunyimwa vilevile hata kama ukimuelewesha consular,jambo la msingi ni kuwsshirikisha watanzania namna gani ya kupata visa kwa urahisi na siyo blah blah.
Huu ujuaji ndiyo jamaa anaouzungumzia hapo,mkikaa huko nje huwa mnaonaga watanzania wenzenu ni wajinga na hawana akili.
Kwa kifupi watanzania muishio nje mna roho mbaya sana