Kwanza kabisa yeye mwenyewe ajue ana kipi, hana kipi, anataka kusaidiwa wapi.
Mfano.
Kuna watu wana degree ya kwanza, wanataka kusoma zaidi nje kwa njia ya scholarships, wanajua wamesoma field gani, wanajua wamefanya mitihani gani, au hata kama hawajui, hawa tunaweza kushauriana nao. Kuna network ya safari za mambo ya vyuo, scholarships, grants, loans etc.
Kuna watu hawana pa kufikia wala barua ya mualiko, wana safari za kijamii/kitalii wanahitaji barua ya mualiko itakayoonesha wana sehemu ya kufikia.
Kuna watu wana qualifications za kutafuta kazi zenye soko sana kimataifa, wanahitaji kujua jinsi ya kuunganishwa na makampuni ya kimataifa kufanya kazi.
Kitu muhimu ni mtu mwenyewe awe na idea ana kipi, anataka kufanya kipi, anataka msaada wapi, ana kipaji gani, mtu aanze kufanya homework yeye mwenyewe, si anataka kuja nje tu wakati hata yeye mwenyewe hajui anataka kufanya nini huko nje.