Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Hahaha ebana umenikumbusha mbali saa
 
Jamani Kiranga UMUGHAKA yaishe msije shia pata ban bure. Kila mtu afanye anachoweza. Unaye omba kusaidiwa kama kiranga hawez kukusaidia usilaumu, ukute sio mlango wako huo. Watatokea wengine watakusaidia.
Msije kosana hata sura hamfahamiani.
Mkuu mimi sina shida na huyo jamaa bali nilikuwa natolea tu mfano wa wabongo wengi waishio majuu walivyo na roho za visokorosokwinyo!
 
Ukiishi nje ya Tanzania ukitaka mafanikio usifanye mazowea na Watanzania, juwana nao lakini jiweke mbali nao kabisa.

Fanya mazowea na wenyeji wenye maana, siyo wale wa hovyo hovyo.

Natumai umenielewa.
 
Unaweza kudhani mtu wa hivyo hawezi kuchomwa ila wabongo wanaweza mkuu.

Kuna mtanzania ana kikampuni chake nchi fulani huko mamtoni.Ana maisha mazuri kuliko watanzania wengi wa huko na kampani yake ilikua wabongo.Siku ya siku kawaalika kwake kwa chakula ila mwezi mmoja baadae anashangaa polisi wanamjia nyumbani.Wanaomba kupekua na wanakuta vifuko vya madawa ya kulevya vimefichwa kwenye heater.
Hakufungwa ila ilimletea changamoto nyingi na mpaka leo anaogopa wabongo kuliko ukoma.
Ninachojua sio wabongo tu wanaooneana wivu bali ni kawaida watu kutoka taifa moja kuoneana wivu.
Ni rahis mim kukuonea wivu wewe ukijenga ghorofa nyumban wakati mim sina cha maana nilichofanya nyumbani ila rafiki yangu wa kinegeria au wa ki Iran hawezi kunionea wivu mim kujenga ghorofa Tz bali atamuonea wivu rafiki yake aliyefanya ya maana Iran.

Wakati naishi mamtoni rafiki zangu walikua ni wazungu na watu wa mataifa mengine.Wakati mm nilikua nawaona wabongo wenzangu ni wabaya wao walikua wakisifia kuwa watanzania ni watu wazuri wapole na wenye upendo na waliniona mim ni rafiki yao mtanzania ni bora huku muiran akiniambia hapendi kujichanganya na wairan wenzake sbb wana wivu na majungu.Mserbia na mnigeria nae anasema hivyo hivyo kasoro mzungu yeye malalamiko yake juu ya wazungu wenzie yanakua tofauti na sisi wageni.
 

Muraaa mbona umeiandika kwa hasira sana...
 
Kinachokuwa ni shida ni kujuana sana, hata maisha ya Tz tunaishi kwa kujuana sana, Kenyans hata UGs naona wana mipaka flani, kila mtu na mambo yake na inasaidia, dawa ni kuwa na mipaka tu.
Boundaries is a foreign concept.

Si ndiyo unaona mpaka hapa JF mtu hakujui anajipa uhuru kwamba anakujua sana mpaka kukuita muongo.

Kwa watu wanaojua kufikiri hilo ni tusi kubwa sana.

Halafu kituko, huyo anayekuita muongo kiholela ndiye anayelalamika kuwa Watanzania hawana msaada.

Ninaweza kuelewa kwa nini watu hawamsaidii mtu asiye na adabu hivi. Mtu mwenye a false sense of entitlement hivi. Mtu mwenye mawazo negative hivi.

Achague moja, kuomba msaada au kufanya ujeuri.

Viwili hivi haviendi pamoja.
 
Wewe mwenyeji wa Taifa gani, mbina wengine waliokutangulia kuishi hatusikii wakilalamika hicho, Jambo la mtu mmoja usilifanye la kitaifa.

Nawe kuwa huko basi usjione msafi saaana kuliko Watanzania wote acha ujinga.
 
Kwa hivyo hayo madawa walimpandikizia?

Siku hizi kukutana nyumbani na watu usiowajua vizuri ni risk kubwa.

Sasa hapo huoni kila mtu analaumu watu wa jamii yake kwa sababu anawajua sana?
 
Sasa mjinga ni mimi au wewe?

Wewe kukaa nje unadhani watu wote ni wajinga kama wewe.

Wewe ni limbukeni na zwazwa wa maisha na ndiyo maana unadhani kuishi nje ndiyo kuyapatia maisha kumbe ni uzumbukuku tu ulionao kichwani.
Huyu ndiye mtu anayeomba msaada.

Hapo anaomba msaada afanikiwe.

Akifanikiwa si atatuua huyu?

Siwezi kushangaa watu wakikataa kukusaidia.
 
Ungejibu Kiranga siyo muongozo ungepungukiwa na nini?

At least kama ni mtego angenasa, lakini umeshindwa kufanya reasoning ya vitu vidogo kama hivi sijui kama mziki wa consular utauweza?
Hivi anajua kuna wakati ili upate permit wazungu wanaweza kukuuliza maswali ya kipuuzi kama vile'Mara ya mwisho kulala na mkeo ulifunga goli ngapi'.
Sasa kwa jazba hizi si ataishia kuwatukana tu🤣
 
Huyu ndiye mtu anayeomba msaada.

Hapo anaomba msaada afanikiwe.

Akifanikiwa si atatuua huyu?

Siwezi kushangaa watu wakikataa kukusaidia.
Watu kama wakina nani?

Hivi kwa akili yako unadhani nategemea msaada?Huo msaada wapelekee ndugu zako.

Mimi Marekani lazima nije kwa juhudi zangu na uwezo wangu binafsi,nyie endeleeni na roho mbaya zenu na uzwazwa wenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…