Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

Kwanza wanalala Nje na kwenye vistoo ndio maana pamoja na kukaa huko USA Bado wako busy humu jf wanatamani kurudi.

Hao hao eti nao Huwa wanaenda kuwasikiliza kina Lisu,Mbowe na watu dizaini yao eti wanahutubiwa mambo ya maisha mazuri 😁😁😁😁
 
Mkuu kuna mmoja juzi katoka Marekani ni mshikaji wetu kitaani yaani jamaa kachoka utadhani alikuwa gerezani,Amefika kuona nina drive Bima(BMW) anabaki kunishangaa na kunipa masifa kibao!

hiki ndo kimefanya nimeandika uzi!
Bongo supu kuku wa buku 5 ni supu hasa,hao wa huko full mabroila harafu bei mbaya 🤣🤣
 
Hakuna sehemu yenye maisha rahisi. Narudia tena hakuna sehemu rahisi yenye maisha rahisi... Labda ubaki Bongo uwe chawa wa mama Samia ila ujue nako kuna ugumu wake. Inabidi uwe mpiga kelele kweli kweli na ujitoe akili zako.
Urahisi wa Maisha Cha kwanza ni chakula na pili nyumba.

Sasa Kwa hizo parameta 2 kipi Bora uende huko ukateseke urudi zero au ubakie bongo uwe na uhakika wa vyote?

Utapata nyumba au Ardhi huko Marekani? Eti unaenda kutafuta harafu 3/4 ya kipato kinaishia kwenye Kuendesha maisha huo si utaahira Sasa.
 
Lazima nikudharau mkuu kwasababu pamoja na kuwa nje lakini hadi Maisha nakuzidi!🤣
Usipopata maisha Afrika,huko kwingine ni Mtihani maana gharama za maisha ziko Juu.

Leo hii Lita ya mafuta ya gari ni nafuu Tanzania kuliko Nchi nyingi za Ulaya.
 
Mkuu hilo nalifahamu lakini kwa hali ya Marekani ni nchi iliyoendelea tulitegemea angalau wawe na maisha ya kuridhisha!
Kitu Kimoja watu hamfahamu ni kwamba gharama za maisha zinaendana na Maendelea,Nchi inavyozidi kuendelea na gharama za maisha zinapanda,hili ndio la msingi.
 
Umeshawahi kufika huko? Siyo kila mtu ana maisha ya kuridhisha. Na siyo kila anayeishi nchi yenye maisha mazuri naye anakuwa na maisha mazuri. Mawazo yako ni kama yale ya wazee wa vijijini wanaodhani kila mtu aliye jijini Dar ana maisha mazuri.
Ndio ukweli huu
 
Tv kubwa nchi 65 .Umenichekesha.Mimi nikajua labda una kiwanda hata cha kutengeneza vifungashio na umeajiri watu 30.Sasa TV nayo ya kulingia jamani.
Hao Jamaa ndio wabebela mabangi siku akina Mbowe au Lisu wakienda huko unategemea mtu anaejitambua na ana maisha atakuja kubeba bango eti anahutubiwa na Mbowe? Mpaka hapo unajua kabisa hao ni chokambaya wabangaizaji tuu 😁😁

Ndio maana wale wengine wanakomaa na Urais pacha huko waliko hakuna maisha 😂😂

Mwisho bongo hapa sio pa kuhama ,Ukiwa na mil.5 unapata Ardhiaekari ya kutosha.
 
Hakuna Cha inferiority bwana kama huna huna tuu,Sasa wewe unaishi ughaibuni watu wanayarajia ulikimbia Hali ngumu Bongo unarudi huna tofauti na wao Sasa Kwa nini wasikuzodoe hata kama maisha ni Yako?
 
Mipango imegoma nini ya kufika ulipopataka ??...hii ukandiaji ni wa chuki 🤣
 
Huu ujinga ndio Huwa naukataa,Nchi hizo ziko very exhausted kwenye Kila nyanja ya uchumi.

Afrika ndio Kuna fursa ingawa Changamoto ya Afrika ni mtaji na sio fursa.Binafsi uniambie nichague kazi Ulaya na Afrika nachagua Afrika
 
Mipango imegoma nini ya kufika ulipopataka ??...hii ukandiaji ni wa chuki 🤣
Kufika wapi ambako mipango imegoma? Mimi huko kwenu ntakuja kutalii mambo ikikaa sawa sio kuishi ,siwezi ishi sehemu ambayo Kila mtu ana habari zake no social cohesion kama ya Bongo.

Kiufupi sijawahi tamani kuishi Nje ya Nchi ila natamani kufika kuona kulivyo.
 
Napenda sana asili yangu na nchi yangu ila kama unajua maana ya maisha mazuri Tanzania wanayaishi viongozi tu tena wale wa ngazi za juu.
Wewe una matatizo,maisha Yako ya Daraja 3 Kwa Kila Nchi ,Sasa ukifika Marekani utaishia Daraja lipi? Hata Tanzania hapa wapo wa Maisha ya Juu,ya kati na chini kama kwingine Sasa unaposena viongozi tuu ndio wanaishi maisha mazuri kisa viongozi sio kweli,hao viongozi ni wachache kuliko wengine.

Kinachonikera hapa Tanzania ni kwamba Ukiwa na vihela Ili uwe salama inatakiwa uwe Chana tawala hata kama hutaki hii ndio kero kubwa Sasa kiasi kwamba huna uhuru wa Mali Yako.
 
Napenda sana asili yangu na nchi yangu ila kama unajua maana ya maisha mazuri Tanzania wanayaishi viongozi tu tena wale wa ngazi za juu.
Wewe una matatizo,maisha Yako ya Daraja 3 Kwa Kila Nchi ,Sasa ukifika Marekani utaishia Daraja lipi? Hata Tanzania hapa wapo wa Maisha ya Juu,ya kati na chini kama kwingine Sasa unaposena viongozi
Itapendeza zaidi HUENDA ikakuongezea kitu vile ufkiriavyo au kupunguza yale ufkiriayo/tofauti.
Nimefika Nchi za Africa kadhaa ila Nje ya Nchi Bado na Africa yote Kwa sehemu kubwa inafanana.

Huko Ulaya nk nakuona kwenye picha,video nk na pia nasoma Hali ya maisha, biashara na Uchumi lakini siwezi kutamani.kuishi huko ila kufika na ntafika before 2030 nikiwa mzima.

Nitapata exposure na experience Mpya ila siwezi tamani kuishi Kwa sababu tayari ntakuwa nimejiwekeza Afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…