Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

Wacha sifa we mshamba, wenye hela hawajinadi namna hiyo.

Humu kuna kina Ridhwaan kikwete, kina Bashungwa, kina Bakhresa Jr's, wajukuu wa Asas, kina Abdiel Mengi na vigogo kibao! Ila hawajishaui kama wewe mpumbavu na kiakaunti chako cha salary account cha CRDB... au unajisemesha uwaoshee majimama humu?! Huna lolote mwanetu we ni KENGE tu!
Achana na huyo poyoyo shamba ukute linafanya kazi halmashauri ya chato au kilwa linajiona limemaliza Kila kitu.

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 
Kama umegoma kuzoa taka kwa PM basi Njoo inbox nikupe nambari za balozi mmoja hivi kaoa ila hajaoa kiviilee😂🤣
Balozi wa wapi tena huyo? Me nataka kwa PM bhana me team NABAKI AFRICA km shemeji yangu tukana. Sitaki kuwa diaspora nianze kuzurura ulaya km yatima 🤣🤣🤣🤣
Si eti shem TUKANA UONE
 
Mtu wa miaka 25 sio mwanafunzi huyo? Ugenini ni ugenini tu sio kwao na kama ulivyosema wengine hawana uhalali wa kuishi huko, basi hata kujikimu itakuwa ni kwa kuunga unga.
Na mipango ya mtu huwezi ijua, kama ameamua maisha yake yote yawe huko, Tz atakuja kuwekeza nini? Itamlazimu awekeze sehemu mbili, na hapo maisha yatakuwa magumu.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
Hili ni tatizo jingine ambalo sisi tunalo kama taifa.

Wazungu wengi ughaibuni humaliza vyuo vikuu wakiwa na wastani wa miaka 23.

Hapo ni kuondoa zile gap years ambazi ni 18-19

Yaani A level miaka 17/18 na kijana aanza uni akiwa na miaka 18

Vijana wa mwaka wa kwanza vyuo vikuu kule mwaka huu waloanza september wana miaka 18.

Hivyo ukienda na umri wa kuanzia miaka tuseme 20, weye unakuwa upo nyuma sana kwa kila kitu na kama umeenda kishule basi utapata mtikisiko.
 
Afrika ukikomaa hauchelewi kupata mtaji wa kuwa na boda boda tuu Nje kuna mitaji na unakuja kuwekeza Afrika mtu mwenye Njaa ya mafanikio Nchi zilizoendelea ni sahihi kwake kwa kuchanga...
Zile bodaboda weye wazikabidhi kwa vijana na wao wakuletea kiasi fulani mtachokubaliana kila mwezi.
 
Kuna Handymen ,wale wanaofanya kazi za repair ndogo ndogo wanatembea na trucks zao kwa shughuli hizo ,wake hawana kampuni ,wale ni independent single people , hata kwenye Craig list wapo wengi mno na kazi ni nyingi ,mfano kufix heating and air conditioning , indoor plumbing , Electrical systems , carpentry nk
Si lazima uwe na kampuni kama unavyodai .
Kuna single independent contractor au Handymen kama hao ,na bado wanapata pesa ndefu tu .
 
Ukihitaji salamu nenda pwani kwa waswahili,kwangu utaambulia chuya ukalishie kuku!

Bado sijafahamu ni kwanini watanzania wengi wanaoishi nchi za Marekani,Canada na Uk huwa wanamaisha magumu kupita kiasi tofauti kabisa na wale wanaoishi nchi za Scandinavian na Germany!.

Ninawafahamu jamaa kadhaa wanaoishi huko tangu zamani na hakuna walichofanya cha maana kwenye familia zao(Wazazi) hapa Tanzania,wengi huwa wanarudishwa kipindi cha matatizo tu lakini huwezi kuwaona wakiwa wanarudi kipindi cha furaha kuwasalimia ndugu zao.

Watanzania wengi wanaoishi nchi za Scandinavian huwa wamerekebisha makazi ya wazazi wao na pia huwa wamejenga nyumba za kifahari ili wanapokuwa wanakuja likizo basi hufikia huko,siyo nyumba tu bali huwa na usafiri mzuri!.

Hii ni tofauti kabisa na wabongo wanaoishi Marekani,Canada na UK,hawa huwa wanarudi makwao endapo Baba au Mama ni mgonjwa au amefariki kabisa,na huwa wakija hata vaa yao inatia mashaka!.

Huwa wanapenda kuvaa miwani mikubwa kama wachomelea welding na kujifanya kuishangaa Tanzania kana kwamba ni chooni!,Unakuta hata hela ya kuwatoa marafiki zake tu Out hawana zaidi ya kujiongelesha blah blah na masifa kibao!.Wengi wamechoka kimuonekano,Sura hazina nuru na mionekano yao imefubaa!.

Ukiwauliza wanabaki kusingizia Marekani Kodi ni kubwa na Ishu za Bills zinabana kila kona,Unabaki kumshangaa kana kwamba huko Marekani ni yeye tu ndiye Bills hupewa kubwa!.

Wabongo wengi wanaoishi Marekani na Canada waliofanikiwa huwa ni kuanzia Umri wa Miaka 50 - na Kuendelea,hawa ndiyo angalau huwa wamejenga makwao na hata hujitahidi kuprovide kwenye familia zao.

Ila hawa wenzangu na mie kuanzia miaka 25 - 45 huwa hawana cha maana zaidi ya blah blah na ngonjera kibao huku kila muda wakipiga simu na kusimanga serikali na kuwakashifu ndugu kana kwamba wanaishi kwenye vyoo!.


Wengine tunawafahamu wamekwenda huko miaka ya 90 lakini hadi leo ni kuzurura tu hawana paper!.

Any way:

Ukitaka kuona walivyo na hasira,wewe soma comments!
Wao wamekwenda kutafuta Umarekani hawakwenda kutafuta maisha hiyo ndio shida ya bongo kwa hivyo wacha wakule unyamwezi .
 
Back
Top Bottom