Sishawishiki saana kuamini mchango wako ingawa pia nashindwa kukupinga at the same time, najiuliza; hivi kwa mazingira yale enzi za mwendazake, hao wapinzani wa kweli (ambao wewe unasema hawapo ) hivi wangefanyaje ili tujue kwamba tunao wapinzani wa kweli? Mtu kabomolewa jengo lake la biashara (Bilcanas club ), kafungiwa chombo chake cha habari (Tanzania Daima ), kang'olewa green gaden yake, mbomoaji ambaye alikua DC kapandishwa cheo hadi kua mkuu wa mkoa baadae kapewa UBUNGE, kavunjwa miguu yake muda mfupi kabla ya uchaguzi, halafu accounts zake zote (za biashara na hata ya mshahara wake wa ubunge ) zikafungwa, hachukui hata mshahara cause account imefungwa, wabunge wake wametongozwa almost wote ili "waunge mkono juhudi" hivi mtu wa namna hiyo alitakiwa kufanya nini zaidi ili tujue kama ni MPINZANI!? Tumejaribu kuvaa viatu vyake kweli?