Uchaguzi wa 2020 ulikuwa wa kughushi-forgeries, kwa vigezo vyote.
Hata CCM wanalijua hilo.
Mazingira na mipango yote ya serikali ilitayarishwa ili mtu mmoja aamue, na ni kwa matakwa yake tu, nani anaingia bungeni.
Kuanzia tume ya uchaguzi, wasimamizi hadi kura za mabegi za kughushi.
Watanzania wanalijua hilo.
Kuna wakati Magufuli alisema hadharani, siwezi kumpa DED kazi na akampitisha mpinzani kuwa mbunge ati kisingizio uchaguzi!
Aliyetayarisha huo ughushi hakuwa na akili sana, matokeo yake yakawa predictable. Nchi nzima mpinzani aliyepata kura ni mmoja tu!
Naye sijui alipitaje!
Kwa viongozi wa kughushi wakawa wamejipatia tatizo jingine kubwa.
Kuna nafasi za kamati bungeni Kikatiba lazima ziongozwe na kambi ya upinzani! Sasa ilibidi Forgerer-in-Chief aagize forgery na kuwaingiza tume ya uchaguzi kughushi namna ya kuwaingiza hao wajumbe 19 toka upinzani kwa nafasi ya wanawake.
Mchezo ulichezwa na Spika Ndugai na tume ya uchaguzi.
Hapo ndipo tulipo-wabunge 19 wa CHADEMA wa kughushi, na wengine wengi tu wa CCM.
UPDATE
Wabunge 19 wa kughushi kupitia uchochoro wa Spika Ndugai ndio wameenguliwa rasmi ufadhili wa chama chao CHADEMA.
Wale 19 hawakuwahi kuwa chagup la chama chao.
Ni muhimu sasa kuwa na tume ya kuchunguza walifika fikaje kuwa wabunge.Heads must roll Tume ya Uchaguzi.