Wabunge wa CHADEMA kurejea Bungeni kuanzia leo

Wabunge wa CHADEMA kurejea Bungeni kuanzia leo

kama umesoma epidemiology usingeliandika hivyo. Pale kulikuwa ni hotspot ya coronavirus. It was right ku pa lock from everybody to enter. Hivyo what they did is what is expected of a sensible man
Tangu walivyoanza karantini waseme walikufa wangapi pale bungeni kwa sababu yoyote ile!
 
Katika hili Hao wabunge wamedhihirisha Ubinafsi, Ulafi wa Pessa, Ujinga, Kukurupuka na sasa AIBU IMEJAA NYUSO ZAO yaaani kwakweli hadi naona aibu walichofanya sijui huko majimboni wakati wa Kampeni watajiteteaje shame on them.
 
Wabunge wote wa Chadema ambao hatimae wamehitimisha siku 14 za kujitenga (self isolation) kwa kukaa nyumbani na kutohudhuria shughuli za Bunge, vikiwemo vikao vya Bunge, ndani ya ukumbi na kamati zake katika maeneo mengine ya mhimili huo, leo Ijumaa, wanatarajiwa kurejea bungeni kuendelea na majukumu yao, baada ya kuwa na uhakika kuwa hawana maambukizi ya Ugonjwa wa COVID19.

Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. John Mnyika (Mb) amesema kuwa Wabunge wa Chadema waliotekeleza uamuzi wa makubaliano ya Chama na wabunge, ya kujitenga kwa kutofika maeneo yote ya Bunge, walitekeleza masharti na ushauri unaotolewa na wataalam wa masuala ya afya kuhusu namna bora ya kujikinga au kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona, miongoni mwa watu hasa inapotokea mahali walipo zipo taarifa kuwa kati yao kuna maambukizi ya virusi hivyo vinavyosababisha Ugonjwa wa COVID19.

"Wabunge wetu wote waliotekeleza makubaliano na uamuzi wa Chama na Wabunge wa kujitenga kwa siku 14, ambayo yanatokana na maelekezo na ushauri wa wataalam wa afya, likiwemo Shirika la Afya Duniani, kwa sasa, kuanzia leo, watarejea bungeni kuendelea na shughuli za kuwawakilisha wananchi, huku wakiendelea kuzingatia tahadhari zote za kujikinga wao na kuwakinga wengine wakiwemo wabunge wengine, Watumishi wa Bunge na wananchi wetu," amesema Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. Mnyika.

Itakumbukwa kuwa Wabunge wa Chadema walianza kutekeleza makubaliano hayo tarehe 1 Mei, mwaka huu, baada ya kuwepo kwa taarifa za maambukizi ya Ugonjwa wa COVID19 katika maeneo ya Bunge, hususan miongoni mwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo siku hizo 14 zinazoelekezwa na wataalam wa afya zimemalizika jana na sasa wana uhakika na afya zao dhidi ya maambukizi ya COVID19.

Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. Mnyika ameongeza kusema kuwa msingi wa makubaliano hayo, unatokana na maelekezo na ushauri wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ambayo yamethibitisha kuwa, kujitenga (self isolation) ni mojawapo ya njia muhimu zilizothibitishwa kisayansi katika kuzuia au kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona, kwa sababu inasaidia kuvunja au kupunguza muingiliano wa watu.

Imetolewa leo Ijumaa, Mei 15, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema


View attachment 1450788
View attachment 1450789
Awo niwakupigwa kwenzi mojamoja ndo wakakae.

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
shida sio wao kupambana na corona,shida ni wao kutumia mapambano kama kick ya kisiasa.halafu wananchi nao wakawaacha peke yao.

yaani ukisoma mitazamo ya wananchi nje ya jf utagundua hakuna aliyekuwa upande wa chadema,wakagundua hiyo gia haikuwa fasaha mlimani[emoji23][emoji23][emoji23],sasa wanarudi moja na wese mdogo mdogo.
 
Back
Top Bottom