Nimejaribu kujiuliza maswali haya mara kadhaa;
1. Kwamba, vikao vya Bunge vikisimama kwa muda kama tulivyofanya kwenye maeneo mengine kama vile elimu (kufunga shule na vyuo vyote) nchi itasimama na serikali kushindwa kutekeleza wajibu wake?
2. Katiba inasemaje nchi inapokuwa kwenye dharura kama hii na mambo kama vile vita?
3. Mfano tungekuwa tuko vitani nchi inapigana na nchi nyingine (na ofcoz wao wenyewe serikali wameshasema nchi na dunia kwa ujumla iko vitani) japo adui huyu tunayepambana naye si wa kawaida, Bunge lingeendelea tu na kuwa target kwa adui?
4. Kingeweza kufanyika kitu gani kwa mujibu wa katiba ya 1977? Na kwa nini hili lisifanyike sasa?