Wabunge wa CHADEMA wakubaliana kutohudhuria tena vikao vya Bunge kutokana na janga la COVID-9, Kujiweka Karantini kwa wiki 2

Wabunge wa CHADEMA wakubaliana kutohudhuria tena vikao vya Bunge kutokana na janga la COVID-9, Kujiweka Karantini kwa wiki 2

toughlendon_1, Ameondoka rafiki yangu Mzee Abdulhaik Mulla( Kaka ya Mh. Mulla) kwa Covid 19,nimesikitika sana na kwa kifo cha Dr. Mahiga, kwa kweli nina hasira na hawa viumbe vifananavyo na binadamu.
 
Shabbash upande wa pili sasa mavi kitambaani watatamani na wao kujitenga lakini watachelewa amri mpaka itoke juu
 
Wabunge ni watu wanaoongoza kwa ubinafsi sana nchi hii. Walishinikiza yote yafanyike ilà wao hawakujigusa, wanatamani posho ya makalio utadhani hawana hela. Bora hao chadema wamejitambua...
Siasa siasani

Kwaiyo unaona wamefanya uamuzi mzuri? kumbuka bunge la KATIBA ilikuwa hivi hivi
 
denooJ,
Ni hatua nzito, uamuzi mgumu, kisiasa. Lakini nawapongeza CHADEMA. Simameni imara. Tunahitaji Leadership, uongozi thabiti, sio viongozi wababaishaji.
 
Safi sana akili kubwa.....acha yabaki mambwa hayo hayana huruma na watz kazi yao kufikilia posho na kumsifia rais etu wapate vyeo......

HONGERA SANA CHADEMA KWA UKOMAVU HUU MNAZIDI KUONYESHA NJIA FOR THE LAST 15 YEARS TUNAWAKUBALI SANA ILA TUME YA UCHAGUZI NA DOLA NDIO TATIZO
KUNA MAISHA BAADA YA COVID19 TUTUNZE AKIBA YA MANENO, HAKUNA ANAYEPENDA WATU WAFE, HATA HUKO WALIKOLOCKDOWN WATU WAMEKUFA.
 
Nimejaribu kujiuliza maswali haya mara kadhaa;

1. Kwamba, vikao vya Bunge vikisimama kwa muda kama tulivyofanya kwenye maeneo mengine kama vile elimu (kufunga shule na vyuo vyote) nchi itasimama na serikali kushindwa kutekeleza wajibu wake?

2. Katiba inasemaje nchi inapokuwa kwenye dharura kama hii na mambo kama vile vita?

3. Mfano tungekuwa tuko vitani nchi inapigana na nchi nyingine (na ofcoz wao wenyewe serikali wameshasema nchi na dunia kwa ujumla iko vitani) japo adui huyu tunayepambana naye si wa kawaida, Bunge lingeendelea tu na kuwa target kwa adui?

4. Kingeweza kufanyika kitu gani kwa mujibu wa katiba ya 1977? Na kwa nini hili lisifanyike sasa?
 
Wabunge wa CCM nao wasione Aibu Kuiiga hatua hii ya Wabunge wa CHADEMA, kwani hadi sasa Matokeo baina yao ni 3 bila!!!
 
KUNA MAISHA BAADA YA COVID19 TUTUNZE AKIBA YA MANENO, HAKUNA ANAYEPENDA WATU WAFE, HATA HUKO WALIKOLOCKDOWN WATU WAMEKUFA.
Unaonge kirahisi sana.....huoni viongozi wako wanavyofanya utani na huu ugonjwa.....
Mara hii umesahau kua walisema ni kaugonjwa kadogo?
Mara hii umesahau viongozi wako wamesema wao ni wanaume waliokamilika hawaogopi corona?

Hizi akili za kutokufuatilia misimamo ya viongozi wenu mnazitoa wapi nyie jamaa?
 
Back
Top Bottom