Wabunge wa CHADEMA waliohudhuria Bungeni, watakiwa kujiuzulu nafasi za uongozi Bungeni

Wabunge wa CHADEMA waliohudhuria Bungeni, watakiwa kujiuzulu nafasi za uongozi Bungeni

Kwa haya yanayotokea Bungeni ambapo wabunge wa Chadema wanafanya uasi dhidi ya chama chao, soon bunge litaanza kurushwa live. Hao wabunge wanaoasi msimamo wa chama chao wameshakubali matokeo kuwa wanahamia kambi nyingine, na Watanzania tulivyo bado watawapa kura kwenye uchaguzi ujao.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
Wasiwasi wangu huko waendako sijui hali itakuwaje, hata chain of command hawaijui.Ni bora kubaki bila vyama
 
Wabunge wote wa JMT wanawakilisha vyama vyao, hakuna mbunge binafsi, sasa ninyi ambao kutwa ni siasa za CCM vs Chadema sasa mpate akili ma kuona umuhimu wa katiba mpya ambayo uwakilishi binafsi utambuliwe.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
Safety First, hao wabunge licha ya kukiuka amri ya chama chao,pia wanahatarisha afya zao na watu wengine bungeni.

Wabunge wote walitakiwa kufanyiwa mandatory testing.Baada ya kupata matokeo ya kubaini nani ana maabukizi,na ni nani safi.
Baada ya hapo spika angeamua utaratibu upi wa kuendesha shughuli za bunge.
 
Kumbe, kwahiyo Komu bado yuko Chadema au Nccr mageuzi?

Officialy kwa spika ni Mbunge wa CDM, akiandika barua kwa spika either yeye au CDM inayohusu kuhama chama basi officially haqualify kuwa mbunge na spika haraka ataijulisha tume ili kuitisha uchaguzi mwingine...Analipwa posho kama mbunge wa CDM na CDM wanalipwa kwa idadi hiyohiyo na Komu akiwemo....
 
Mtumishi wa umma hauwezi kufanyia kazi barua inayosema kuwa kikao fulani kimemfukuza uanachama mtu fulani bila kutaka kuona minutes za kikao hicho na zenye sahihi ya waliohudhuria na kufanya uamuzi huo. Kwa kilichofanyika ni kuwa alijiridhisha kuwa aliyeandika barua hiyo ndie pekee mwenye mamlaka ya kumvua uanachama diwani wa chama chake. Alitakiwa kufanya due diligence kwa kuuliza uongozi wa kata husika kuhusu uhalali wa barua hiyo. Na kwa mtu mwenye nyadhfa ya umeya angemuuliza Katibu wa Chama husika kama hilo jambo ni sahihi. Inaelekea badala ya kutaka uthibitisho kutoka kwenye Chama husika yeye aliwauliza viongozi wake wa kisiasa. Huo ni uzembe wa wazi na umemuacha wazi wa kufunguliwa mashtaka yeye mwenyewe. Na tofauti na alivyosema Waziri wake, ni kawaida kabisa mwandishi kubadilisha uamuzi wake kama atagundua kuwa taarifa alizotumia kufikia uamuzi zilikuwa na dosari.

Amandla.....
Nakuunga mkono 105%, yule mkurugenzi tungekuwa Na utawala bora alipaswa kufukuzwa kazi 100%.jambo LA watu kufukuzwa chama sio siri.mambo mengine siasa tuweke pembeni
 
Wabunge wengi wa Chadema hawakubaliani na zidumu fikra za Mwenyekiti. Kinachofanyika, wanapata courage ya kusimamia mawazo yao kwa nyakati tofauti. Naamin wako wengine wengi wasiokubaliana na misimamo ya chair, wakiongozwa na Kubenea. Ni suala la muda tuu, tutasikia Mengi.
 
Wabunge wengi wa Chadema hawakubaliani na zidumu fikra za Mwenyekiti. Kinachofanyika, wanapata courage ya kusimamia mawazo yao kwa nyakati tofauti. Naamin wako wengine wengi wasiokubaliana na misimamo ya chair, wakiongozwa na Kubenea. Ni suala la muda tuu, tutasikia Mengi.
Kwa Tanzania usipokubaliana Na misimamo ya viongozi Wa chama chao Ni bora kujiuzulu uwanachama, nje ya hapo usaliti.Hats ccm wabunge wengi hawakubaliana Na mwenyekiti wao katika mambo mengine ila tu inawabidi.asikudanganye MTU mkuu
 
Wanasiasa (siyo wote) ni watu hatari sana.Akili zao zote sasa hivi zipo Oct 2020,kila mtu anafanya pemutations na combinations zake.
 
Wabunge wengi wa Chadema hawakubaliani na zidumu fikra za Mwenyekiti. Kinachofanyika, wanapata courage ya kusimamia mawazo yao kwa nyakati tofauti. Naamin wako wengine wengi wasiokubaliana na misimamo ya chair, wakiongozwa na Kubenea. Ni suala la muda tuu, tutasikia Mengi.
Hawakubaliani vipi wakati amechaguliwa mwaka jana tu? Wangefanya uasi baada ya uchaguzi tungewaelewa, wanachofanya sasa ni uasi tu.

JPM amezichanga karata zake vizuri sana kwa kuingia urafiki na Mbatia na kuiibua NCCR, kwa kufanya hivyo amefanikiwa kuibomoa Chadema na kujikinga na uasi wa wana CCM. CCM wakimfanyia zengwe bado ataibukia NCCR kwa Mbatia na CCM kitakufa rasmi kitu ambacho wana CCM na bodi ya wadhamini ya chama hawatakubali hilo litokee.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huenda uko sawa, lakini hakuna chama ambacho kinatoa hyo nafasi uliyosema.sio ccm wala upinzani.hawa wabunge walichofanya wangekuwa ccm, muda huu tungesema mengine, muulize nape Na makamba January.
Zitto kwani naye alifanywa nini? Dk Kitila nae alifanywa nini?

Liondoe kwanza boriti la jicho lako kisha ulisafishe jicho la mwenzio.

Unahubiri demokrasia kila siku lakini ndani ya chama chako hureflect unacho kuhubiri.
 
Demokrasia ngumu sana jamani

Wabunge wa Chadema kwa kauli moja wamependekeza kwamba Wabunge wasaliti walioamua kuhudhuria bunge la corona na kupuuza msimamo wa chama chao wa kujitenga na bunge hilo kwa wiki mbili kama mwongozo wa WHO unavyoelekeza ili kuzuia maambukizi ya Virus hatari vya corona , wametakiwa kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama ukiwemo ujumbe wa kamati kuu

Kauli hiyo imetolewa na Mnadhimu wa Kambi rasmi bungeni Mh Ester Bulaya , amesema kwamba ni aibu kwa kiongozi anayeshiriki vikao vya maamuzi vya chama kwa nafasi yake ya uongozi halafu baada ya muda mfupi anapuuza mambo aliyoshiriki kuyaamua .

Ikumbukwe kwamba Chadema haihangaiki na Ubunge wa mtu yeyote , bali wasaliti wanatakiwa kuachia nafasi za uongozi ndani ya chama , ndio maana mpaka sasa Anthony Komu na Joseph Selasini bado ni wabunge .

Mnadhimu wa Kambi rasmi bungeni Mh Ester Bulaya ameandika hivi kwenye mtandao wa Twitter.





=====

UPDATES:

DAVID Silinde, Mbunge wa Momba, Songwe kupitia Chadema ametangaza kujizulu nafasi ya katibu wa wabunge wa chama hicho kuanzia jana Jumatatu tarehe 4 Mei 2020

Silinde ambaye amekuwa mbunge kwa miaka kumi mfululizo amesema amechukua hatua hiyo ya kujiuzulu na tayari barua yake ya imemfikia Freema Mbowe.

Amesema, licha ya barua hiyo kumpelekea Mbowe, pia nakala yake ameipeleka kwa John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho.

“Nilijiuzulu jana nafasi ya Katibu wa Wabunge wa Chadema, kwa sababu nimeshindwa kusimamia maagizo ya chama ya kutohudhuria bungeni,” amesema Silinde. Hata hivyo, Silinde hajaweka wazi kama atakihama chama hicho au la.

Wabunge wengine walioingia bungeni jana ni; Joseph Selasini (Rombo), Anthony Komu (Moshi Vijijini), Peter Lijualikali (Kilombero), Jafary Michael (Moshi Mjini) na wabunge viti maalumu, Ratifa Chande, Mariam Msabaha na Sabrina Sungura.

Baada ya Silinde kuchukua uamuzi huo, wabunge wa Chadema wamemtaka Mariam Sabaha kujiuzulu nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, kufuatia hatua yake ya kukiuka maagizo ya chama.
 
M
Zitto kwani naye alifanywa nini? Dk Kitila nae alifanywa nini?

Liondoe kwanza boriti la jicho lako kisha ulisafishe jicho la mwenzio.

Unahubiri demokrasia kila siku lakini ndani ya chama chako hureflect unacho kuhubiri.
Mbowe ni kama Mchungaji anayewahubiria watu waache uzinzi Wakati yeye anatafuna waumini.Je, ndo kusema kilichotangazwa na Mbowe ulikuwa msimamo wake tuu? Kama ndivyo, Chadema ni chama Cha kidemokrasia?
 
Chadema imesambaratika. Imebaki na Mbowe, Mnyika, Bulaya, Heche, Matiko na Sugu pekee!!
Mbona wanatosha sana. Wacha majoka yote yaondoke yenye price tags wanaonunuliwa na CCM kwa pesa zetu za kodi; masaliti hayo!
 
Back
Top Bottom