Wabunge wa CHADEMA waliohudhuria Bungeni, watakiwa kujiuzulu nafasi za uongozi Bungeni

Wabunge wa CHADEMA waliohudhuria Bungeni, watakiwa kujiuzulu nafasi za uongozi Bungeni

Watabakia kuwa historia!
Wassira alisema hivyo hiyvo, yeye sasa ndiye amebaki historia. CDM siyo mtu, ni chama, wataingia na kutoka kama ilivyo CCM, Wanatoka na kuingia. Nani angedhani kuwa NCCR ingekuwepo leo? Wewe una umri wako wa kutosha kufahamu haya mambo tena kwa undani sana, lakini unaleta ushabiki wa kitoto mtu mzima wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wabunge ni wawakilishi wa wanachi wenye vyama na wasio na vyama

Hakuna kujiuzulu kwani walipigiwa kura na chadema tu? Spika hata wakileta barua ya kuwafukuza kaitupe vyoo vya bunge
Lkn kumbuka pia mgogoro wa DED wa Ubungo dhidi ya Meya Jacob. Kama huoni ya huko Bungeni basi tazama hata sakata la Ubungo ili kupima hoja yako.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema Wapigwee!!!

Ni sauti ya Mch Gwajima siku ya Jumapili, Je, maombi hayo yameanza kufanya kazi?

Yetu macho
 
Zitto hakuwahi kupewa nafasi hiyo.

Ukisharuhusu demokrasia manake anaruhusu mawazo ya wengi ktk kufanya maamuzi,huu mchakato haukuhusisha mawazo ya baadhi ya watu na wana haki kuupinga.
Huu usaliti uliofanywa Na hawa wabunge wangeufanya ccm ingekula kwao
 
niliandika hapa siku si nyingi kwamba chama hakiwezi kuendeshwa kwa mawazo ya mwenyekiti tu na nilisisitiza hapa kua wapo wabunge watakaidi hilo agizo, nikaishiwa kuitwa lumumba buku Saba. Ukweli ni kua wabunge wengi wa chadema hawapendezwi na 'amri' za mwenyekiti.

Leo hii wabunge wanashindwa kuwawakilisha wananchi eti kisa korona. Yaani kiongozi unakimbia majukumu unategemea utaaminiwa tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu waungwana wanachofanya Ni kujiuzulu uwanachama Na kujiunga Na chama ukipendacho.usaliti haukubaliki kokote.kutii maelekezo ya viongozi Wa chama chao Ni lazima.waliopo ccm wanajua.wanaowashabikia hawa wabunge wanawadanganya.
 
Hao wabunge ni wawakilishi wa wanachi wenye vyama na wasio na vyama

Hakuna kujiuzulu kwani walipigiwa kura na chadema tu? Spika hata wakileta barua ya kuwafukuza kaitupe vyoo vya bunge
Spika akiikata hiyo barua atakuwa anavunja katiba.Nchi yetu haina mgombea huru
 
Hao vijana wanamgwaya Mbowe sababu ya kesho yao tu (Nidhamu ya uwoga) lakini wasiokuwa na cha kupoteza kwenye chama wameshampuuza.

Kila mtu mzima anajua namna ya ku-deal na afya yake na akifa atazikwa pekee yake.
 

Wabunge wa Chadema kwa kauli moja wamependekeza kwamba Wabunge wasaliti walioamua kuhudhuria bunge la corona na kupuuza msimamo wa chama chao wa kujitenga na bunge hilo kwa wiki mbili kama mwongozo wa WHO unavyoelekeza ili kuzuia maambukizi ya Virus hatari vya corona , wametakiwa kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama ukiwemo ujumbe wa kamati kuu

Kauli hiyo imetolewa na Mnadhimu wa Kambi rasmi bungeni Mh Ester Bulaya , amesema kwamba ni aibu kwa kiongozi anayeshiriki vikao vya maamuzi vya chama kwa nafasi yake ya uongozi halafu baada ya muda mfupi anapuuza mambo aliyoshiriki kuyaamua .

Ikumbukwe kwamba Chadema haihangaiki na Ubunge wa mtu yeyote , bali wasaliti wanatakiwa kuachia nafasi za uongozi ndani ya chama , ndio maana mpaka sasa Anthony Komu na Joseph Selasini bado ni wabunge .

Mnadhimu wa Kambi rasmi bungeni Mh Ester Bulaya ameandika hivi kwenye mtandao wa Twitter.





=====

UPDATES:

DAVID Silinde, Mbunge wa Momba, Songwe kupitia Chadema ametangaza kujizulu nafasi ya katibu wa wabunge wa chama hicho kuanzia jana Jumatatu tarehe 4 Mei 2020

Silinde ambaye amekuwa mbunge kwa miaka kumi mfululizo amesema amechukua hatua hiyo ya kujiuzulu na tayari barua yake ya imemfikia Freema Mbowe.

Amesema, licha ya barua hiyo kumpelekea Mbowe, pia nakala yake ameipeleka kwa John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho.

“Nilijiuzulu jana nafasi ya Katibu wa Wabunge wa Chadema, kwa sababu nimeshindwa kusimamia maagizo ya chama ya kutohudhuria bungeni,” amesema Silinde. Hata hivyo, Silinde hajaweka wazi kama atakihama chama hicho au la.

Wabunge wengine walioingia bungeni jana ni; Joseph Selasini (Rombo), Anthony Komu (Moshi Vijijini), Peter Lijualikali (Kilombero), Jafary Michael (Moshi Mjini) na wabunge viti maalumu, Ratifa Chande, Mariam Msabaha na Sabrina Sungura.

Baada ya Silinde kuchukua uamuzi huo, wabunge wa Chadema wamemtaka Mariam Sabaha kujiuzulu nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, kufuatia hatua yake ya kukiuka maagizo ya chama.


Ndio mafuta yanaendelea kujitenga na maji hivyo.

Chama kinapita kwenye tanuri la moto kuelekea GE 2020.

Only the fittest of the fittest shall survive.
 
Ni mpuuzi tu ndo anaweza amini kuwa CHADEMA ni chama cha siasa, hili ni genge la wachumia matumbo chini ya kiongozi mkuu sana DJ Mbowe, chama hiki hakiheshimu kauli ya mwenyekiti wala ya katibu wewe unategemea nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hapa Tanzania hakuna chama kilichofikia level hyo.hakipo, mengi Ni magenge ya watu.ukiungana Nayo yaheshimu.muulize membe
 
Back
Top Bottom