Wabunge wa CHADEMA waliohudhuria Bungeni, watakiwa kujiuzulu nafasi za uongozi Bungeni

Udikteta Ni nn? Kutii maagizo ya wakubwa Ni utawala bora pia
Kuwa mkubwa haina maana kila mda upo sawa,CHADEMA ni chama siasa na si taasisi binafsi ya mtu,ambaye anayeweza akaamua chochote wengine mnafuata.

Udikteta ni kulazimisha vitu atakavyo mtu mmoja bila kuwa shirikisha na kuheshimu mawazo ya wengine,kisa yeye ni mkubwa kinyazifa.
 
Ni vema Chadema wakatupa taarifa kamili kama wabunge wao wako kwenye karantini hawa tunaowaona bungeni kulikoni?

Sasa hivi mbunge wa Bukoba Mh Lwakatare ndio anachangia hotuba ya wizara ya viwanda na biashara na yuko mubashara TBC, Channel ten na Star.

Nyuma ya mh Lwakatare nawaona wabunge wa " kutosha" tu wa Chadema wakimshangilia mwenzao.

Ama Chadema imegawanyika au ndio imeishiwa pumzi!

Maendeleo hayana vyama!
Endelea kuangalia TBCCM
 
Hao vijana wanamgwaya Mbowe sababu ya kesho yao tu (Nidhamu ya uwoga) lakini wasiokuwa na cha kupoteza kwenye chama wameshampuuza.

Kila mtu mzima anajua namna ya ku-deal na afya yake na akifa atazikwa pekee yake.
Nakubaliana Na we we, nakuhakikishia 80% ya wabunge Wa chama vyote wanawaogopa viongozi wao, sio ccm wala upinzani.Mifano IPO, fikiria Nape Na makamba yaliyowakuta ndani ya ccm.
 
Hakika na bila mashaka viongozi wa CHADEMA ni genge la wachumia tumbo na kwa kujua hilo, Mbowe anawachezesha kama vikaragosi.

Sakata la Diwani/Meya Jacob kuvuliwa madaraka yake kisheria ni moja ya mifano iliyo hai. Tawi la chama chake CHADEMA, lilimfukuza kwenye chama na kumwandikia barua Mkurugenzi wa Halmashauri. Akajitokeza kwa vyombo vya habari kumlalamikia Mkurugenzi badala ya kuchukua hatua kwenye vyombo husika Kikatiba na kisheria. Mnyika, Katibu Mkuu wa CHADEMA, naye akalivalia njuga na kutumia vyombo vya habari kukanusha kwa kumtukana na kumtishia Mkurugenzi. Ni mambo ya kustaajabisha, aibu na utoto.

Hongera kwa viongozi wachache wanaotambua ubabe wa Mbowe. Wengi wao wameondoka kwenye chama maana wangejaribu kushindana Mwamba wangegonga ukuta na kuumia.

UDUMU UBABE WA M/KITI CHADEMA
 
Kuwa mkubwa haina maana kila mda upo sawa,CHADEMA ni chama siasa na si taasisi binafsi ya mtu,ambaye anayeweza akaamua chochote wengine mnafuata.

Udikteta ni kulazimisha vitu atakavyo mtu mmoja bila kuwa shirikisha na kuheshimu mawazo ya wengine,kisa yeye ni mkubwa kinyazifa.
Mkuu huenda uko sawa, lakini hakuna chama ambacho kinatoa hyo nafasi uliyosema.sio ccm wala upinzani.hawa wabunge walichofanya wangekuwa ccm, muda huu tungesema mengine, muulize nape Na makamba January.
 
Hakika na bila mashaka viongozi wa CHADEMA ni genge la wachumia tumbo na kwa kujua hilo, Mbowe anawachezesha kama vikaragosi.

Sakata la Diwani/Meya Jacob kuvuliwa madaraka yake kisheria ni moja ya mifano iliyo hai. Tawi la chama chake CHADEMA, lilimfukuza kwenye chama na kumwandikia barua Mkurugenzi wa Halmashauri. Akajitokeza kwa vyombo vya habari kumlalamikia Mkurugenzi badala ya kuchukua hatua kwenye vyombo husika Kikatiba na kisheria. Mnyika, Katibu Mkuu wa CHADEMA, naye akalivalia njuga na kutumia vyombo vya habari kukanusha kwa kumtukana na kumtishia Mkurugenzi. Ni mambo ya kustaajabisha, aibu na utoto.

Hongera kwa viongozi wachache wanaotambua ubabe wa Mbowe. Wengi wao wameondoka kwenye chama maana wangejaribu kushindana Mwamba wangegonga ukuta na kuumia.

UDUMU UBABE WA M/KITI CHADEMA
Mkuu usifanye siasa uchwara, yule mkurugenzi Wa ubungo mpaka Leo ameshindwa kumtaja MTU aliyepeleka ile barua, swala LA hawa wabunge Ni usaliti.usizunguke.
 
Ukishachaguliwa wewe ni mali ya wananchi...... Waendesheni hao wa viti maalumu!

Ni mali ya wananchi kupitia chama A.
Chama A kikikufukuza uanachama huna tena sifa yakuwa Mbunge na lazima watu warudi kwenye uchaguzi au Katiba imebadirika..?
 
Ni vema Chadema wakatupa taarifa kamili kama wabunge wao wako kwenye karantini hawa tunaowaona bungeni kulikoni?

Sasa hivi mbunge wa Bukoba Mh Lwakatare ndio anachangia hotuba ya wizara ya viwanda na biashara na yuko mubashara TBC, Channel ten na Star.

Nyuma ya mh Lwakatare nawaona wabunge wa " kutosha" tu wa Chadema wakimshangilia mwenzao.

Ama Chadema imegawanyika au ndio imeishiwa pumzi!

Maendeleo hayana vyama!
how many threads do you make a day?
 
Kwa haya yanayotokea Bungeni ambapo wabunge wa Chadema wanafanya uasi dhidi ya chama chao, soon bunge litaanza kurushwa live. Hao wabunge wanaoasi msimamo wa chama chao wameshakubali matokeo kuwa wanahamia kambi nyingine, na Watanzania tulivyo bado watawapa kura kwenye uchaguzi ujao.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mali ya wananchi kupitia chama A.
Chama A kikikufukuza uanachama huna tena sifa yakuwa Mbunge na lazima watu warudi kwenye uchaguzi au Katiba imebadirika..?
Kumbe, kwahiyo Komu bado yuko Chadema au Nccr mageuzi?
 
Hakika na bila mashaka viongozi wa CHADEMA ni genge la wachumia tumbo na kwa kujua hilo, Mbowe anawachezesha kama vikaragosi.

Sakata la Diwani/Meya Jacob kuvuliwa madaraka yake kisheria ni moja ya mifano iliyo hai. Tawi la chama chake CHADEMA, lilimfukuza kwenye chama na kumwandikia barua Mkurugenzi wa Halmashauri. Akajitokeza kwa vyombo vya habari kumlalamikia Mkurugenzi badala ya kuchukua hatua kwenye vyombo husika Kikatiba na kisheria. Mnyika, Katibu Mkuu wa CHADEMA, naye akalivalia njuga na kutumia vyombo vya habari kukanusha kwa kumtukana na kumtishia Mkurugenzi. Ni mambo ya kustaajabisha, aibu na utoto.

Hongera kwa viongozi wachache wanaotambua ubabe wa Mbowe. Wengi wao wameondoka kwenye chama maana wangejaribu kushindana Mwamba wangegonga ukuta na kuumia.

UDUMU UBABE WA M/KITI CHADEMA
Mtumishi wa umma hauwezi kufanyia kazi barua inayosema kuwa kikao fulani kimemfukuza uanachama mtu fulani bila kutaka kuona minutes za kikao hicho na zenye sahihi ya waliohudhuria na kufanya uamuzi huo. Kwa kilichofanyika ni kuwa alijiridhisha kuwa aliyeandika barua hiyo ndie pekee mwenye mamlaka ya kumvua uanachama diwani wa chama chake. Alitakiwa kufanya due diligence kwa kuuliza uongozi wa kata husika kuhusu uhalali wa barua hiyo. Na kwa mtu mwenye nyadhfa ya umeya angemuuliza Katibu wa Chama husika kama hilo jambo ni sahihi. Inaelekea badala ya kutaka uthibitisho kutoka kwenye Chama husika yeye aliwauliza viongozi wake wa kisiasa. Huo ni uzembe wa wazi na umemuacha wazi wa kufunguliwa mashtaka yeye mwenyewe. Na tofauti na alivyosema Waziri wake, ni kawaida kabisa mwandishi kubadilisha uamuzi wake kama atagundua kuwa taarifa alizotumia kufikia uamuzi zilikuwa na dosari.

Amandla.....
 
Back
Top Bottom