Wabunge wa CHADEMA wamekengeuka, wanajifanya hawaoni kazi nzuri ya uletaji maendeleo ndani ya miaka minne

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,746
Reaction score
5,772
Hii ni kwa sababu uchaguzi umekaribia na mwezi Juni tarehe 31 Bunge litavunjwa. Sasa wabunge wa Chadema wamekumbwa na kiholo. Wanajiuliza wataenda kuwaambia nini wananchi? Maana walizoea siasa za kupakana matope, na wananchi wamebadilika wanataka siasa za kuletewa maendeleo.

Muda wote wamekuwa wanashinda mahakamani wakijifanya wanaharakati na kusahau kuwa wananchi wao wanahitaji maendeleo badala ya harakati zilizopitwa na wakati.

Cha kushangaza anasimama mbunge wa Chadema anabeza eti vimejengwa vituo vya afya mia nne thelathini na tatu kwenye kila tarafa, wakati kuna kata nyingi hapa nchini. Anashindwa kutambua hivi vituo vya afya vimejengwa vina hadhi ya kuwa hospital ya wilaya. Maana vina kila jengo ambalo linakidhi kuwa hospital ya wilaya. Alafu kuwekwa katika kila tarafa ni kuwasogezea wananchi huduma ambazo walitakiwa wazipate mpaka waende hospital ya wilaya.

Haya majengo 433 ni majengo ya kisasa na yatatumika kwa manufaa ya watanzania wote na tena hata kwa kizazi kijacho.
Pia kujenga vituo vya afya 433 na hospital za wilaya 67 ndani ya miaka minne sio kazi ndogo.

Unaposimama na kubeza hili jambo ni kupata kiwewe na kiholo. Na October inafika sijui mtasema nini kwa wananchi! Najua kujua umeshashindwa kabla mechi haijaanza ni jambo baya sana kisaikolojia ila ndio hivyo kubalini matokeo.
 
Mami naona unakereka uwepo wa Cdm !! Why Ngalu ?.

Cdm ni chama cha upinzani na wanaunda kambi rasmi ya upinzani kikatiba. Na kazi yao ni pamoja na kuikosoa serikali , kuonyesha madhaifu na mapungufu ya serikali inayotawala. (NDIYO KAZI YAO )[emoji120]. Pili serikali inayoongozwa na Maghufuli siyo perfect kama unavyojithidi kuamini. Ni serikali ya dunia ya tatu ipo chini ya matarajio.

Mwisho uamini usiamini bwana mkubwa aliingia kwa 58% . Hawa 42% hawawezi kumpenda overnight . Kubwa aridhike kufanya kazi aliyoiomba na wakati utahukumu. Huhitaji kushupaza shingo kuiaminisha watu.

Odhis *
 
Siku zote kazi nzuri ni ile unayofaidika nayo, kujenga barabara kwa kodi zetu ni wajibu wa serikali, kununua ndege kwa kodi zetu wakati tuna vipaumbele ambavyo havijatekelezwa ni kutunyima haki wanyonge wengi ambao hatutazipanda daima. Ukiwa baba mlevi mwenye umaarufu wa kutoa ofa baa lazima familia yako itakulaumu.
 
Kuna mambo ya kukosoa na kweli mtu anaweza kukuunnga mkono. Lakini ndani ya miaka minne vinajengwa vituo vya afya 433 na hospital za wilaya 67. Anasimama mbunge anabeza hii haijaa sawa alipaswa apongeze.
Upinzani sio kupinga kila jambo.
Omera tuwe wazalendo.
 
Mmesahau miaka ile watu walikuwa wanazipiga na hakuna kulichokuwa kinafanyika?
 
Kuna mambo ya kukosoa na kweli mtu anaweza kukuunnga mkono. Lakini ndani ya miaka minne vinajengwa vituo vya afya 433 na hospital za wilaya 67. Anasimama mbunge anabeza hii haijaa sawa alipaswa apongeze.
Upinzani sio kupinga kila jambo.
Omera tuwe wazalendo.
Uzalendo ni pamoja na kupinga matumizi ya hovyo yasio na faida kwa wananchi. Kwa mfano wewe sijakuona ukikemea matumizi mabaya ya hazina kutaka ku eliminate upinzani .

Panapohitaji pongezi utapongezwa, lakini panapohitaji kuhoji mapungufu wacha watu wahoji hizo weakness

Odhis *
 
Hii ni kwa sababu uchaguzi umekaribia na mwezi Juni tarehe 31 Bunge litavunjwa. Sasa wabunge wa Chadema wamekumbwa na kiholo. Wanajiuliza wataenda kuwaambia nini wananchi? Maana walizoea siasa za kupakana matope, na wananchi wamebadilika wanataka siasa za kuletewa maendeleo.

Muda wote wamekuwa wanashinda mahakamani wakijifanya wanaharakati na kusahau kuwa wananchi wao wanahitaji maendeleo badala ya harakati zilizopitwa na wakati.

Cha kushangaza anasimama mbunge wa Chadema anabeza eti vimejengwa vituo vya afya mia nne thelathini na tatu kwenye kila tarafa, wakati kuna kata nyingi hapa nchini. Anashindwa kutambua hivi vituo vya afya vimejengwa vina hadhi ya kuwa hospital ya wilaya. Maana vina kila jengo ambalo linakidhi kuwa hospital ya wilaya. Alafu kuwekwa katika kila tarafa ni kuwasogezea wananchi huduma ambazo walitakiwa wazipate mpaka waende hospital ya wilaya.

Haya majengo 433 ni majengo ya kisasa na yatatumika kwa manufaa ya watanzania wote na tena hata kwa kizazi kijacho.
Pia kujenga vituo vya afya 433 na hospital za wilaya 67 ndani ya miaka minne sio kazi ndogo.

Unaposimama na kubeza hili jambo ni kupata kiwewe na kiholo. Na October inafika sijui mtasema nini kwa wananchi! Najua kujua umeshashindwa kabla mechi haijaanza ni jambo baya sana kisaikolojia ila ndio hivyo kubalini matokeo.

Mkuu ujasiri huu wa kuongelea haya mnaupata wapi wakati Corona imetuinamia hivi?

Jamani eeh au nyie mwaishi sayari nyingine?
 
Hata Usa ambako janga ni kubwa kuliko sehemu yoyote siasa zinaendelea. Jana umemsikia Obama akiunga mkono Joe Biden awe mgombea urais. Kwa hiyo tunaguswa na haya yote kwa ujumla. Hasa mtu anapobeza mambo makubwa yaliyofanyika kwa muda mfupi.
 
Uzalendo ni pamoja na kupinga matumizi ya hovyo yasio na faida kwa wananchi. Kwa mfano wewe sijakuona ukikemea matumizi mabaya ya hazina kutaka ku eliminate upinzani .

Panapohitaji pongezi utapongezwa, lakini panapohitaji kuhoji mapungufu wacha watu wahoji hizo weakness

Odhis *
Nitakemea vipi matumizi mabaya ya hazina tena ku eliminate upinzani! Bila ushahidi?
 
Kila awamu imefanya yake. Usifikiri hawa wanafanya ambayo hayajawahi kufanywa. Bahati nzuri mimi nimekuepo awamu zote 5 nazijua zote ipi was the best .

Odhis *
Niambie ni awamu gani ambayo imefanya makubwa katika hizi awamu tano? Nakubaliana na wewe kila awamu imefanya kazi, ila ipi ni bora?
 
Kila awamu imefanya yake. Usifikiri hawa wanafanya ambayo hayajawahi kufanywa. Bahati nzuri mimi nimekuepo awamu zote 5 nazijua zote ipi was the best .

Odhis *
Watu hawajui - gharama ya kujenga hivyo vituo vyote na hospitali za wilaya, zikiwekwa pamoja, hazifikii gharama ya kujenga na kuwekea vifaa hospitali 3 tu za awamu iliyopita - Mloganzila, Taasisi ya Moyo ya JK na Hospitali na Benjamin Mkapa.

Kujenga vituo na hospitali za Wilaya ni jambo jema, lakini siyo maajabu. Maana hata hizo awamu nyingine zilizopita kuna mambo mazuri yalifanyika, na mengine awamu hii haijayafikia.
 
Kuna mambo ya kukosoa na kweli mtu anaweza kukuunnga mkono. Lakini ndani ya miaka minne vinajengwa vituo vya afya 433 na hospital za wilaya 67. Anasimama mbunge anabeza hii haijaa sawa alipaswa apongeze.
Upinzani sio kupinga kila jambo.
Omera tuwe wazalendo.
Watanzania wamelipa kodi na kuwezesha kujenga hivyo vituo mkuu.Hao wasimamizi tu na tunawalipa kutoka kwenye kodi zetu. Ajajenga CCM,CUF ,CHADEMA etc
Vituo hivyo ni mali ya umma maana umma ndiyo umefanya hayo
 
Back
Top Bottom