Acha kukopa China, hata US wanakopa, je umesikia wanalazimisha wananchi wao kusifia hiyo mikopo?
Kumbe wamebeza kwa kusema kuwa hospitali ni chache kulingana na idadi ya kata. Huo ndio maana ya upinzani, ulitaka wasifie hilo ni jukumu lao? Kazi ya wapinzani wa kweli ni kuikosoa na kuibeza serikali iliyopo madarakani, ili isilale kwa kubweteka, na bado ikilala inaitoa madarakani. Inaonekana ww ni mzee aliyethirika na siasa za ujamaa za chama kimoja, hivyo unapokutana na siasa za kweli za ushindani, unaanza kujiliza kama mwanamke aliyekimbiwa na mumewe. Kutokuwepo kwa idadi hiyo ya vituo vya afya kabla ya uhuru, hiyo sio tiketi ya kusifiwa na wapinzani. Ilitakiwa viwe vituo vingi zaidi ya hivyo, hivyo wapinzani wanawashangaa nyie kuamka mkiwa mmechelewa na kuona ni bonge ya mafanikio. Mnataka msifiwe kwa mambo ya kawaida sana kwakuwa nyie ni malimbukeni wa maendeleo. Ulimbukeni wenu isiwe tatizo kwa wenye uelewa wa mambo.