Narudia tena, sio kwamba ww ni limbukeni tu, bali pia ni bendera fuata upepo. Mradi wa SGR ni wa kilomita 1,450, na kila kitu kilishakamilika wakati wa JK, na mradi ungegarimu $7.5b kwa mkopo toka EXIM Bank ya China. Sikatai kujengwa kwa awamu, bali uongo uliopo kwenye ujenzi huo. Tuliambiwa huo mradi mpaka Morogoro utagharimu 1t, na fedha zitakuwa ni za ndani. Ila mpaka sasa Dar-moro imekula 2.t na bado haijakamilika, na hakuna uhakika kuwa bado ni fedha za ndani, maana awamu hii inapikwa data vibaya.
Nasema hivi, huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani. Ngoja nikupe ukweli ww limbukeni. Kipande cha Moro-Makutopora hakijafika hata 30% tena kwa taarifa zenye utata. Na mkopo hautokei Turkey bali unatoka Exim bank ya China kiasi cha 3.1t zilizokopwa hivi juzi. Huyo mturuki unayemtaja ww ni mkandarasi lakini sio mtoa mkopo. Sina popote ninapokiri ujenzi wa hivyo vituo, maana sina ushahidi zaidi ya kutajiwa idadi na nyie waabudu sanamu. Nimekuwa nikiwaambia malimbukeni wenzako, waweke list ya hivyo vituo kwa kuweka jedwali kuonyesha kituo kiko wapi, na kimegharimu shilingi ngapi, hakuna anayefanya hivyo. Huenda ww ukafanya hivyo kama sio mpiga siasa mfu hapa jukwaani. Halafu mimi wala familia yangu, hatutibiwi kwenye hospitali za serikali, ni faida kwa hao wanaohitaji, ila sio mimi maana namudu gharama za hospitali binafsi.
Tuache hayo, huo mradi enzi za JK gharama ilikuwa $7.5b kwa mkopo toka Exim Bank ya China. Ni kipi kilimfanya Magufuli akaacha utaratibu ule akaamua kutuambia kuwa tulikuwa tumepigwa sana, halafu akasema tutajenga kwa fedha za ndani, huku ikionyesha chini yake kwenye mradi huu, sio kwamba tu anaweza asiumalize kwenye utawala wake, lakini ni dhahiri yeye atavuka hizo $7.5b, tena kwa mkopo, halafu ni kutoka huko huko exim bank ya China! ambayo mwanzo alituaminishwa tumepigwa? Kama una uwezo wa kujadili nadhani utajikita kwenye paragraph hii ya mwisho maana ndio nitajua unajua lolote, na sio bendera fuata upepo, kwani zile paragraph za juu umeonyesha una uelewa mdogo nazo.