Wabunge wa Kagera wapinga Mkoa wao kumegwa na kupelekwa Chato

Hujui hata kulikua na mkoa unaitwa West Lake Region (Mkoa wa Ziwa Magharibi)na ndio ukamegwa ukazaa Kagera na wilaya za Misenyi na Kyerwa zimejimegua Humo humo Kagera leo unabetua Midomo hamtaki kumegwa mmkea akina nani nyie.

Ukimega au kumegewa jua kuna siku utamegwaaaa tu Utake Usitake Upende Usipende. Ni hayo tu.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Na huo ndiyo ukweli, Chato iliendelezwa kwa maandalizi ya kuwa makao makuu ya "mkoa" na sasa wanataka kutimiza ahadi ya JPM aliyosema yule mzee msibani Chato. Kama Chato ipo juu kimaendeleo kwa Geita mjini ni vema rais akabadili makao makuu ya mkoa wa Geita yakawa Chato ili adhima ya wana Chato itimie.
 
Sikuzote unapoanzishwa mkoa lazima kuna sehemu fulan ya mikoa jiran itamegwa, kataeni kwenye vikao vyenu rasmi kuhusu jambo ilo Samia hatomega ila mkikubali huko alafu mkasema Samia akatae mtakuwa wanafiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko juu kuliko Geita ? Umefika Geita lini ? Pole sana. Usiwe unalinganisha mji wa Geita na hicho kijiji cha Chato. Chato hata hiyo Katoro haoni ndani
 
Haya ni madhara ya ubinafsi na udikteta. Kama sio kupeleka mamiradi makubwa nani angehangaika na kuunda mkoa
 
Nimesema "kama" Chato ipo juu ya Geita, sijasema ipo juu. Lakini msingi wa hoja ni hao waliopanga kuiendeleza Chato ili baadaye watengeneze mkoa na kuifanya Chato makao makuu. Nia ilikuwa ya kibinafsi zaidi kuliko uhalisia. Tazama jinsi walivyojitoa Kagera kwa sababu za mtu binafsi na sasa wakaamua kutengeneza mkoa kwa sababu za mtu huyohuyo binafsi. Tazama majengo makubwa yametangulia kujengwa kabla ya kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi na kijamii kwanza, ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa pasipo kuwa na shughuli za kupeleka ndege huko, na hiyo ni mifano michache ya hasara za uamuzi wa mtu mmoja.
 
Kabisa ndg yangu,unajengaje uwanja chato unaacha O'mukajunguti ambao unatakiwa uwe wa Africa mashariki lkn akajenga Kwa pembeni ya mwanza airport! Wenyeji wa Mushasha O'mukajunguti walishakatazwa mda mlefu wasifanye shughuli yoyote ya aridhi pale,inatia hasila na majonzi
 
Hata wapinge hadi asubuhi, atakayeamua mkoa wao umegwe ama uachwe na Chato iwe mkoa ama ibakie ilivyo ni Rais wa nchi, hizi zingine ni pre justification tu.
 
Hilo ndio tatizo. Hakuna namna njia pekee ni Mkuu wa nchi kuidhisha ili Chato iwe mkoa
 
Sisi tulio vijijini tunaamini maendeleo yetu yapo kwenye Kata, kijiji na kitongoji.
Mahitaji yetu wilayani ni kidogo sana.

2020 vitongoji viliungwa na kufanya kitongoji kuwa kikubwa zaidi.
Kuna sehemu vitongoji vitatu viliungwa kuwa kitongoji.kimoja.
Iwapo nia ni kusogeza huduma kwa mwananchi, hapa ziisogezwa?

Baadhi ya vitongoji hivyo wakati huu haiwezekani kufanya mkutano mmoja kwa kitongoji.kizima.
Inabidi kufanya mikutano miwili hadi mitatu.
Mfano ni kitongoji cha Rwenjojo katika.kata ya Ihanda wilaya ya Karagwe au kitongoji cha Kigando kwenye kata ya Kasulo wilayani Ngara.
Mifano.ipo mingi.

Serikali haina gharama za moja kwa moja za uendeshaji wa kitongoji lakini ina gharama za uendeshaji wa wilaya na mkoa.
Tena gharama kubwa.

Naipongeza.sana.serikali.kwa kuwapa pikipiki watendaji wa.kata, maafisaelimu kata na wataalamu wa.kilimo.
Hii ina tija kubwa kwa wananchi kuliko kuunda wilaya au mkoa.

Mungu ibariki Tanzania.
 

Kumega mega mikoa sio solution ya kuleta MAENDELEO.
Ila uwajibikaji +uzalendo ndio vitaleta maendeleo
 
kumega mega mikoa sijui wilaya ilikuwa upuuzi wa malaika wa chattle maana fikra zake zilikuwa kama za jibwa tu, akili ndogo nguvu nyingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…