Wabunge wa Kagera wapinga Mkoa wao kumegwa na kupelekwa Chato

Wangepinga na uchaguzi fake uliowapa ubunge.

Maadamu walimpenda Jiwe, wapende na makandokando yake yaliyotufikisha hapa leo hii.

Na hapa CCM ndio mjue madhara ya hii katiba mbovu si kwa wapinzani tu.
Wanalialia wakati nyoka anaingia ndani ya blanketi walikuwa wanachekelea? Wanaangalia wana.tiwa vidole halafu wanajifanya kuruka. Wavumilie sindano iingie. Bia tamu
 
Chato lazima iwe mkoa.Ni ukweli lakini mchungu
 
Kama Chato inakuwa mkoa kwanini Machame, Marangu, Mamba, Mwika, Kirua na Rombo zisiwe mikoa?
Hayo maeneo ukiyajumlisha yote mzunguko wa pesa wa Katoro hawafiki hata robo kwa siku
 
Mkuu kuna mtu (Sukumagang) nilimuuliza ni kwanini adhimisho ni la JK Nyerere lakini mashada yaliwekwa Chato akaniambie kule ndo kuna "kaburi la taifa".
Ujue tatizo ni kuwa nchi yetu ina maskini wengi wa akili na kipato.
Wanajidanganya sana hao na kamwe hawawezi kutundolea fikra zetu .

Tunaamini kabisa kuwa mwl JK Nyerere ndiye baba wa taifa letu na hakuna mwingine awaye.

Legacy za mwl JK Nyerere hazitakuja kubadilishwa kwa mtu yeyote.
 
Hakuna dr hapo nawapongeza wahaya halisi wamejitambua
Yaani kati ya wabunge mazuzu ni pamoja na haya matatu maana yanashindwa kutetea majimbo yao kama huko Bukoba vijijini kwa Rweikiza maji ni yeye yuko bize na vitu ambavyo wanajimbo wenzake hawana manufaa. Biharamulo na ngara zimekubali kwenda chato na wabunge wao wamekubali alafu mijitu hii inayopiga sijui imekerwa na nini
 
Biharamulo na Ngara wote ni wanyangara na wahangaza wacha waungane na wahangaza wa chato
 
Watu kama hawa wenye roho mbaya ndo wamekuwa wakikwamisha miradi mingi mkoani Kagera kwa kupinga kila kitu. Sasa wewe mbunge wa muleba mambo ya biharamulo yanakuhusu nini.

Hizi ni roho mbaya hazijengi na zinaukwamisha mkoa wa Kagera tumewachoka watu kama hawa, ni bora waende kutatua changamoto majimboni kwao
 
Nilikuwa napinga Chatto kuwa Mkoa, ila kwa hoja za kipuuzi za hawa Wabunge naunga mkono Chato uwe mkoa...

Hawa wabunge ni wakabila sana, ili kumaliza hili huo mkoa umegwe, wanalalamika atafikiri huo mkoa ni Nchi washenzi kabisa hawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…