Wabunge walihongwa na DP World; ushahidi huu hapa!

Bhangosha!
EeeenHeeeee!

Mkuu 'Chinga' ule mradi wa Bagamoyo ndio umezaa huu wa DP World?

Wanufaika ni walewale, au hawa ni kundi jingine?

Isije ikawa kuna "uliyembebea mikoba" mwingine safari hii?

Hebu tupe habari mpya!

Anyway, vyovyote na iwavyo, maumivu yetu (Tanzania) ni yale yale.
 
Kifupi ni kwamba nchi hii tuna bahati mbaya ya kupata viongozi wasio na "akili".
 
Magufuli alaumiwe vipi 100% kwasababu aliamua kuchezea uchaguzi??

How?

- Kwani kuchezea uchaguzi ndio kuliwafanya hao wabunge wakachukue rushwa Dubai?

- Kuchezea uchaguzi ndio kulimfanya Samia akatoe bandari zetu kwa wajomba zake huku akiungwa mkono na hao wabunge?

- Kuchezea uchaguzi ndio kuliwafanya kina Mbarawa watie saini zao kwenye ule mkataba wa hovyo?

Kwa mantiki hiyo, kama kwako unaona Magufuli anastahili kulaumiwa 100%, hebu tuambie, Samia yeye aliyesimamia huo uozo chini ya serikali yake alaumiwe kwa asilimia ngapi?
 
With all due respect to Prof. Anna Tibaijuka. Nilitarajia angetoa maoni yenye mashiko lakini nimemsikiliza mbona anababaisha tu kama vile siyo mtu wa hadhi yake? Labda ana ajenda nyingine. Vifungu anavyosema vina matatizo mbona havina matatizo yo yote. Anashindwa hata kujibu maswali ya waandishi wa habari. Kwa kweli sikutarajia kuwa angekuwa mbabaishaji tu kwa hadhi yake. Kwa maoni yangu bora hata angekaa kimya tu. Labda kuna "interest" zake ambazo anazilinda halafu anataka kutuaminisha kuwa mkataba una shida kubwa sana. Nilitamani kama msomi wa hadhi yake angewasaidia watanzania kuuelewa mkataba na kutoa mapendekezo mahsusi ya namna ya kuuboresha maana ameanza kwa kusema kuwa kuingia mkataba ni jambo zuri. Au anatetea TICS? Labda alikuwa na hisa huko.
 
Ningekuona wa maana na hiki ulichoandika hapa, kama ungepinga hoja za Prof. Tibaijuka ili tufanye mlinganisho, sio kuja na maneno matupu chini ya kivuli "with all due respect" ili upate attention yetu!.

JF sio ya kutafuta respect za wajinga, weka hoja upate respect.
 
"JF sio ya kutafuta respect za wajinga, weka hoja upate respect". Naiheshimu JF na sitarajii JF kuwa kijiwe cha matusi. Namheshimu Prof. Tibaijuka.
 
CCM ya sasa huwa inatengeneza matatizo, ili baadaye ije iyatumie hayo matatizo kutengeneza suluhi zenye kuwapatia ugali wakati wa uchaguzi...

Mgombea ajaye baada ya Samia, atatumia headlines hizi hizi sijui za mikatapa ya DP world n.k kuombea kura na atapata...
 
Kama hakutakuwa na katiba mpya mambo haya haya ya kijinga yataendelea
 
Prof Tibaijuka katuambia UBAYA wa mkataba. Wewe na mafisadi wenzako hebu tuambie UZURI wa mkataba ni upi.
 
"JF sio ya kutafuta respect za wajinga, weka hoja upate respect". Naiheshimu JF na sitarajii JF kuwa kijiwe cha matusi. Namheshimu Prof. Tibaijuka.
Ujinga sio tusi myfriend, ni kutojua, ndio maana nikakwambia, kwako kumlaumu Prof. Tibaijuka kwa maneno matupu pekee, bila kuonesha udhaifu wa hoja zake, umekosea, na hilo kosa ndio ujinga wenyewe.

So, if you want to prove me wrong, kwamba wewe sio mjinga, unajua tuwekee hapa hoja za Prof. Tibaijuka, uweke na hoja zako za kumpinga, kisha tulimganishe.

Karibu..
 
Umeamua kujitoa akili naona, record za wapinzani walipokuwa bungeni zinaonyesha tofauti lakini
 
Kweli kuna connection hapa.

Wakati nikimsikiliza Dr. Slaa alipokuwa anaupinga mkataba wa DPW, kuna mahali alitoa mfano kwamba, hata serikali ya awamu ya nne ilitaka kuiuza bandari, bahati nzuri kwetu, yule aliyewapa hiyo taarifa upinzani wakati ule, alifukuzwa kazi.

Kitendo cha kumfukuza kazi yule whistleblower tayari kinaonesha nia ovu iliyokuwepo wakati wa awamu ya nne kwa rasilimali zetu, sasa nikiunganisha na hicho alichoandika Chinga One, nikiongezea na kelele zilizokuwepo kwenye mkataba wa Bandari ya Bagamoyo, naona kabisa, jamaa inawezekana wameamua kuwapa waarabu wakijua ule wa Bandari ya Bagamoyo kwao umeshakuwa mgumu.
 
Akileta hoja za kumpinga Prof Tibaijuka nitag, nimekaa paleee.

Tatizo mafisadi wameajiri watu wa kuwatetea humu mitandaoni bila kuwapa hoja zozote zaidi ya kupayuka tu pasipo kutoa hoja watu tuwaeewe. Inasikitisha sana😢😮
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…