Wabunge wanne - Anthony Komu, Joseph Selasini, David Silinde na Wilfred Lwakatare wafutwa uanachama wa CHADEMA

Wabunge wanne - Anthony Komu, Joseph Selasini, David Silinde na Wilfred Lwakatare wafutwa uanachama wa CHADEMA

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema Kamati Kuu CHADEMA imefikia uamuzi wa kuwafuta uanachama Mbunge David Silinde na Wilfred Rwakatare baada ya Wabunge hao kukiuka agizo la Chama na kukijitokeza kwenye vyombo vya habari kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya maagizo ya Chama na Viongozi wa Chama

Aidha, amesema Kamati Kuu chama hicho imeazimia Wabunge Anthony Komu na Joseph Selasini pamoja na kuwa wamejipotezea sifa ya uanachama wa CHADEMA, wameendelea kutoka kauli za kejeli, kashfa na kukiuka maagizo ya Chama, hivyo Chama kimeazimia kuwafukuza uanachama

Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Mariamu Msabaha, ameshiriki kukiuka maagizo ya Chama, ilitakiwa awe mfano na kwakuwa amekwenda kinyume, amevuliwa nafasi zake zote ndani ya Chama na kubaki na Ubunge na atatakiwa ajieleze kwanini asichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka maagizo”-MNYIKA
 
Hii habari ya uongo, Chadema hawahawa wanaopigania Uhuru wa kujieleza, Uhuru wa kuwa na maoni tofauti leo wamfukuze mtu kisa wamaeleza maoni yao kuhusu korona
 
Nawapongeza Chadema kwa hatua walioifikia, Kwani wamefanya kwa kufuata Katiba na sheria za Chama chao kinavyowataka
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema Kamati Kuu CHADEMA imefikia uamuzi wa kuwafuta uanachama Mbunge David Silinde na Wilfred Rwakatare baada ya Wabunge hao kukiuka agizo la Chama na kukijitokeza kwenye vyombo vya habari kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya maagizo ya Chama na Viongozi wa Chama...
Ni sawa lakini hawa watu automatically kwa matendo yao hawakuonekana kutaka kuendelea kuwa wanachama wa Chadema.

Nadhani ni wakati sasa wa CHADEMA ku review tena Intelligence Unit yake na kuchukua hatua kwa wakati dhidi ya watu kama hawa, hakuna sababu ya watu kuachiwa kufika mbali kiasi hiki, walitakiwa kutemwa mapema asubuhi sana kabla Jogoo halijawika maana mienendo yao ilishajulikana.

Enheee Peter Lijualikali yeye kaachwa au...
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema Kamati Kuu CHADEMA imefikia uamuzi wa kuwafuta uanachama Mbunge David Silinde na Wilfred Rwakatare baada ya Wabunge hao kukiuka agizo la Chama na kukijitokeza kwenye vyombo vya habari kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya maagizo ya Chama na Viongozi wa Chama...
Safi sana JJM, yaani Silinde ni Mpumbavu sana!! Mwache aende NCCR,wakati Kigogo alivyosema Jamaa kanunuliwa watu walikuwa hawajamuelewa kigogo na ndio hivyo yupo kwenye wabunge 20 wa NCCR.
 
Wakati mwingine ni busara kukaa kimya kuliko kuchukua hatua ambazo zinazidi kudhoufisha chama sioni sababu za msingi za kufukuza wabunge wakati kila siku wananunuliwa kama ndugu
Kama una taasisi inayoheshimika, huwezi kukaa na watu kama hao ambao wanadharau maagizo ya taasisi. Jaribu kwa Jiwe kama utafika saa moja subuhi! Watakaobaki CDM wanatosha sana!
 
Back
Top Bottom