Baada ya kafulila,masha na Patrobas Katambi na wengine wengi kuhama chadema.
Kumekuwepo na tetesi na habari za chini chini kuna
Vigogo zaidi wanatarajia kuhama chadema kwenda chama tawala.
Kitu kikubwa watu ambacho wanajidanganya wanadhani chadema akiondoka mtu flani au akihama mtu flani basi chama ndo kimekufa au kitapoteza mwelekeo kisiasa
Kitu ambacho sio kweli
Chadema ni taasisi na chama cha watanzania hivyo kama kuna mtu ana mipango ya kuhama ahame tuu chama kitaendelea kuwepo.
Ikumbukwe ya kwamba ndani ya chadema walikuwepo watu kama akina kaburu, jerry muro, kitila mkumbo Zitto, machali, juliana shonza,mpendazoe,slaa shibuda waliondoka chadema lakini chama bado kipoo hivyo hata mbowe, mnyika, msigwa, kubenea, mdee,sugu na wengine wengi wahamie CCM chama kitaendelea kuwepo na chama kipo kitaendelea kuwepo.
Ingekuwa chama ni mtu basi hata leo dini zisingekuwepo maana walikuwepo watu kama akina yesu na mtume muhamad leo hii hawapo duniani lakini usilamu na ukristo usingekuwepo.
Kama ukristo ungekuwa ni yesu tuu au usilamu ungekuwa ni mohamad tuu
Basi leo hii usilamu na ukristo usingekuwepo kwa maana wenye dini zao washaondoka nazo