Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Rais hajiingilii Ikulu kiholela, anapigiwa kura na watu, kwa hiyo hata ikiwa miaka 18 poa tu as long as majority ya wapiga kura wataamini kuwa ndiye mtu anayefaa kuongoza nchi.
 
zitto atuambie ni kigezo gani alichutmia kuset umri wa chini kuwa miaka 35? au kwa kuwa yeye yuko above 35? kuna watu wana miaka 30 nao wanautaka Urais!


UBINAFSI BWANA!

chuki mbaya sana,kwann unamwandama zitto wakati waliotoa maoni hayo ni wengi.acha ukasuku
 

mtu akikusaidia,haimaanishi akiwa anaharibu unamwangalia tu!
 

kwani we ni nani?hii nchi ni huru na kuna uhuru wa kutoa maoni pia,zitto kama watanzania wengine ana uhuru huo na anatumia haki yake ya kikatiba we jifiche chumbani jidanganye,ila zitto ni maji marefu
 
Kwanza nataka kujua kama kuna ukweli ktk habari hii maana Wabunge wetu watakuwa wamefanya dharau kubwa sana kwa rais na wananchi wa Jamhuri ya Tanzania. Hoja hiyo Spika wa bunge hakutakiwa hata kuipa nafasi..

nasema hivi kwa sababu wananchi hawakuwatuma wabunge wao kwenda kuzungumzia haya bungeni, maana tayari tunayo Tume ya kukusanya maoni na tayari inaifanya kazi hiyo. Maoni yetu yanakusanywa na wao wabunge kama wananchi wanatakiwa kutoa maoni yao kwa tume hiyo na sio kuyapeleka Bungeni yajadiliwe.

Ifike wakati na mahala maamuzi ya kitaifa yaheshimiwe. Hatufanyi kurekebisha katiba iliyopo bali tunaandika katiba mpya na uamuzi umeshafikiwa kwamba kufikia mwaka 2014 katiba mpya itakuwa tayari..Mwisho wa yote haya mapendekezo yote yaloorodheshwa hapo juu ni kuhusu maslahi yao tu viongozi ktk ngazi zao hakuna mapendekezo yoyote yanayowahusu wananchi iwe vyombo vya kulinda na kusimamia maswala ya Wakulima, wafanyakazi, maliasili na rasilimali zetu - It's all about THEM.
 
nilimuona j.f.kenedy

 


Ingeanza miaka 20 kabisa? au unasemaje ben wa saanane
 
Last edited by a moderator:
40 years is okay, kama vipi usogezwe hadi 50 years ili kupata watu wenye busara zaidi!!
 
Hiyo ndiyo shida ya warundi kupenda makuu, kama vile shehe ponda anataka kutawala dunia kwa itikadi zake za kidini, Zitto haya naye anaamini yeye tu ndo anafaa kuwa rais, Kigwangala hivyo hivyo, ogopa wenye asili ya kirundi.
 

duh!umeongea kitu cha maana kweli kweli.nashangaa hata jambo moja la mwananchi halikuongelewa isipokua nyazifa za wakubwa tu na kujipatia post nyeti ili kujijenga kimahela.tanzania bwana.jamani kutokana na hayo.tanzania bila ya umasikiniiiiii!.....
 
na akiwa rais atasema kukaa madarakani vipindi viwil 2 vya miaka kumi ni ushamba, mbona zimbabwe, uganda, rwanda hakuna kikomo.... so selfish bouy! nguvu iyo iyo unayotafutia urais na ccm yako ndo nguvu iyo iyo itakayokunyima ukubwa.... im sincerely nt knwn to such a selfish presdent!!
 
Huyu Zito Zuberi Kabwe anatoa maoni haya kwa maslahi binafsi. Ukichanganua vizuri hoja hii, utakuta inakazia matamanio yake ya kutaka urais akiwa bado kufikia umri unaokubalika kikatiba kwa katiba ya sasa. Ingalikuwa ni tenda, basi yeye tungesema atoke nje ya mjadala kwa kuwa ana maslahi binafsi au conflict of interest.
Anataka katiba ibadilishwe kulenga matarajio yake.
Waingereza wana usemi unaosema " Life begins at 40s. Mtu akifikia umri huu akili yake inakuwa imekomaa na inakuwa na hekima. Hulka za papara kama za Zito zinakuwa zimetulia. Kwa mtu mwenye hekima kosa moja haliachi mke, lakini kwa umri chini ya miaka 40 one mistake one goal. Kwa maana hiyo kijana akiwa rais baraza la mwaziri litabadilishwa kila siku pengine hata kwa mambo ya mitaani tu.
Vijana hupenda kujionyesha ili kila mtu amtambue yeye nani. Atajitutumua hata pasiposthili na kujifanya anajua kila kitu. Tutakapotaka kumrekebisha maji yatakuwa yamemwagika.
Kwa kufuata hoja zake kama vile: Ruanda Afrika kusini..........wanafanya kadha wa kadha inaonyesha hawezi kubuni mawazo yake au hata kujivunia mambo yake bali ana hulka ya kuona jambo linalofanywa na jirani ni bora zaidi kuliko la Tanzania. Kuna hatari hata Wakenya, jirani zetu wakatuona sisi ni watu wa kuiga kila jambo kutoka kwao.
Tunataka vijana wanaoielewa siasa/ utamaduni wa nchi yetu, wanaweza kueleza tulifikaje hapo tulipo na kwa nini tunaona ni bora kuendelea na utamaduni tulionao. Sio kukopi na kupest kila kitu. Anapozungumzia mikataba ya madini anasema Botswana, Zimbambwe nk. hatoi mawazo yake kulingana na mazingira na hali halisi ya Tanzania.Akiona kijana wa Uigereza amelegaza suruali naye kesho atalegeza, akiona ndoa za jinsia moja zimeruhusiwa na Tanzania turuhusu bila kwanza kupima umuhimu wa kuruhusu au kutoruhusu ndoa za jinsia moja. Wenzetu Korea kusini tulipata uhuru pamoja walitoa mawazo yao pasipo kutegemea ya taifa lingine mpaka sasa wanatupita kimaendeleo
Kenya wananchi wake wanawekza katika nchi yao hawapeleki mitaji Uswiss. Fedha zinazopatikana zinainua uchumi wao. Wakati wa vurugu za uchaguzi mataifa ya nje walishindwa kuwawekea vikwazo vya uchumi kwa sababu bajeti yao haitegemei misaada toka nje, Tanzania ni siasa kila siku toka uchaguzi hadi uchaguzi mnang'ang'ania umri wa urais bila output yoyote ya maana. Hakuna link yoyote kati ya maendeleo na umri inayotolewa ili mradi tu agombee kijana. Kijana wa umri huo ana features zipi tunazotaka kuexploit?
 
Nakubaliana nawe labda Rais wawe wanaruhusiwa kuwa na awamu mbili tu za miaka minne minne badala ya mitano, hilo la Rais kijana kustaafu na umri mdogo ni vyema kukawa na utaratibu wa kutochukua pensions zao mpaka watakapofikisha umri wa miaka 60 vingnevyo wanaweza wakaifilisi hazina ambayo tayari imeshafilisika.

 

Why 35 and not 18? Maana chini ya 18-35 nao wananyimwa haki ya kuchaguliwa...
 

Mkuu Mkandara,
Haya mambo hayajajadiliwa Bungeni bali tume ya kukusanya maoni kwa ajili ya katiba mpya ilikutana na wabunge ili kupata maoni yao!
 
Hawa jamaa kweli wana funza vichwani. Kweli hayo ni maoni ya watu wenye kuipenda Tanzania?
Ndio maana nimekuwa nikiamini kuwa kwa mazingira yalivyo sasa nchini katu hatutapata Katiba yenye kukidhi matakwa mtambuka.

Bado nasisitiza CHADEMA wakichukua nchi 2015, moja ya vipaumbele katika muhula wa kwanza ni LAZIMA kuandika upya Katiba ya nchi hii ktk mazingira huru, ya haki na ya usawa.
 
Eti wabunge kama Lusinde, Nchemba, Chiligati, Shibuda, Wassira,Meghji, Kilango, Zungu na watu wa sampuli hiyo wapitishe Katiba kwa ajili ya maslahi ya Tanzania na/au Mtanzania wa kawaida? Ni afadhali kuamini hekaya za Abunuwasi kuliko hilo kutokea!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…