comson
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 288
- 41
i think huyu jamaa ni very pathetic na mwenye uchu wa madaraka,anayependa umaarufu usio na msingi wala tija kwa taifa letu... nikijaribu kuangalia historia yake pindi anaposoma pale UDSM alimuhama mgombea mwenzake na kwenda kuungana na mtu mwingine akiwa na ambition za kuwa president na matokeo yake akaukosa.... kujitangaza kwamba yeye ni mmoja kati ya wanachadema wanaoutaka URAIS ni makosa kwa sababu chama kina taratibu zake na wewe kuwa na ushabiki usio na tija kwa wenzako ambao wanategemea kuwa na wewe utakuwa na msimamo kama wao (upande wao) ni UNAFIKI.... kwa muonekano wa haraka ulio wazi kijana kama ZITTO kupewa urais ni sawa na kuipeleka hii nchi mahala ambapo tutakuja kujuta zaidi ya tunavyojuta sasa ambapo tunaweza kuirekebisha kwa kumpa mtu anayefaa nyadhifa ngumu na sio rahisi kama walivyoiona wanaCCM.... kuwa Rais sio kukaa ikulu,kutoa picha nzuri zenye tabasamu kwa ajili ya kuziweka kwenye ofisi za serikali au za umma au kufurahi na kuchekacheka kwenye halaiki ya watu ukitoa maneno matupu ambayo hayana effect, URAIS ni zaidi ya hapo..... watanzania inabidi tukae tufikirie ili kuweza kupata mtu anayefaa kwa ajilki ya manufaa na mustakabali wa taifa letu lenye miaka 50 lakini bado linaonekana changa katika macho ya mataifa mengine.... "....mungu ibariki tanzania mungu wajalie watanzania waweze kuipata ile nchi yao ya ahadi ambayo wameisubiri kwa miaka mingi pasipo kuwa na mafanikio kutoka kwa wale wanaoiongoza safari ya kufika huko..."