Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Umri wa Urais unatakiwa uongeze hadi iwe miaka 45; Ubunge kweli uwe na kikomo na kusiwe na mbunge anayepita bila kupingwa lazima wote wagombee (viti maalum vifutwe of course)....

Kuna hoja dhaifu hapa juu ya umri wa 35 eti watu walioko kati ya 35 na 40 wamekuwa ni wapiga kura tu! Je wale wa chini ya 35 wakija na hoja kama hiyo itakuwaje? Hivi ni kwanini umri wa Uraisi unapunguzwa kisa mtu fulani anataka kugombea? Nadhani hili la umri libaki kama lilivyo tu. Huyu anayetaka kubadilisha umri ili agombee anaonyesha anaweza hata kukatalia kwenye Urais hata muda wake ukiisha maana mapenzi yake ni Uraisi na si kuongoza!

Anayeweza kutuwekea poll ya umri wa Uraisi atuwekee tupige kura hapahapa wenye nia na Uraisi kwa kutaka kubadilisha umri wajue mapema kama matamanio yao yatatimia au laB
 
IKo siku akiwa madarakani, atakuja na uko wa kuwa rausi iwe vipindi vitatu, sio viwili tena


Hili nalo neno..huyu dogo ni sumu mbaya sana katika siasa za nchi yetu,ngoja tujiandae na maziwa endapo tu tutaimeza,ili tuitapike.
 
kwani tenga,ustaadh wa ngumi rais wa masharobaro umri wao ni miaka mingapi.
zitto anastahili kuwa rais na ni haki yake.
leka tutigite mpaka sasa haina rais where are u zitto.
 
Mimi nisingekuwa na Shida kama Zitto angevalia njuga suala hili huku yeye akiwa na miaka zaidi ya 40.Kinachonikera ni pale anapokuwa mpiga debe mkuu huku yeye ndiyo akiwa anautaka huo urais.Ni aibu sana unapopigia debe kitu fulani kwa maslahi yako.
Kuna maneno yameenea sana mitaani kwamba lengo la wanaomtuma Zitto ni ili aje agawe kura za CDM.Lililo wazi ni kwamba Zitto kamwe hawezi kupitishwa kugombea Urais kupitia CDM kutokana na historia isiyoridhisha ndani ya CDM.Siri zimevuja kwamba ama Zitto atagombea kama mgombea binafsi ama kupitia CHAUMA chama cha rafiki yake Kafulila.CCM wanajua kwa kufanya hivi atagawa kura za CDM.Ndiyo maana hapa bungeni jana haikushangaza hoja yake hii ya kichovu iliungwa mkono na wabunge wengi wa CCM huku wakimshangilia kwa nguvu.Wabunge wengine wote wa CDM waliipuuza hoja hii na kusema ina agenda ya siri.
 
Tatizo huyu mkuu wetu dhaifu kafanya kila mtu anauona uraisi kama ndala mbovu
 
Miaka ibaki 40 hakuna sababu kupunguza umri.kama anataka urais si atafika huko umri utamkuta.urais ni tofauti na ubunge asifikiri ameweza ubunge ataweza na urajis kulahisi hivyo.
 
zitto atuambie ni kigezo gani alichutmia kuset umri wa chini kuwa miaka 35? au kwa kuwa yeye yuko above 35? kuna watu wana miaka 30 nao wanautaka Urais!


UBINAFSI BWANA!

hata wakishusha poa,kwani binadamu gani mwenye akili timamu amchague ZZK? Si ni bora awe lowasa? Napenda CDM ichukue nchi 2015,lakin sitaki zitto awe ndo mgombea urais,pia hata akiwa mgombea mwenza (running mate) ataharibu mambo ndani ya chama!!IKITOKEA, kura yangu ya Rais naipa CCM
 
Zito kama mchuzi kioo usio na nyanya wala viungo ...ur good 4nothing,unakuwa cheap ka mwanamke malaya
 
Watu wanalalamika ukomo wa uraisi wa miaka saba kwa hoja ya itakuwaje kama raisi ni incompetent muda wote huo...!Tulipewa Jakaya 2005 tukagundua ni incompentent lakini tukampa tena 2010!Kama ingekuwa ukomo miaka 7 basi huyu Jakaya mwezi uliopita tungekuwa tumeshaachana nae.

Mi sioni sababu ya kuangaika na miaka ya ukomo wa uraisi kama raisi ataendelea kuwa mfalme asiyeweza kupigiwa vote of no confidence au kushtakiwa mahakamani during his presidence.Kikubwa ni kuwa na mianya mingine ya kuondokana na raisi kilaza bila kusubiri uchaguzi mkuu kwani wapiga kura wengi pia bado ni "vilaza" wa kudanganyika na vitu vya mpito.

Hoja ya raisi kuwa na 35+ yrs pia halina ubaya kama raisi huyu atakuwa competent.Kulikataa hili kwa sababu ya kumkataa Zitto Kabwe ni kutowatendea haki wengine ambao wana uwezo kuliko yeye na hawautolei macho uraisi kama yeye(nawafahamu wengi).Kwangu mimi naona raisi awe na umri wowote kuanzia miaka 35 ili mradi kuwe na mianya mingine ya kikatiba ya kumuondoa kama ataunderperform bila kusubiri uchaguzi ambao most likely anaweza kusurvive(kama Kikwete) pamoja na ubovu wake.

Suala la muungano wa mkataba siliafiki hata kidogo ila napendekeza muungano huu ufe tu.Kama ni ujirani tukutane kwenye EAC au jumuiya zingine huku kila nchi ikiwa kivyake.Muungano wowote ule utaendelea kuwa na mawaa kama wananchi wenyewe hawapendi kuungana.

Viti maalum kweli vifutwe kwani vingi hugeuzwa kuwa ni vitu maalum na ukiti wote hupotea na kuwa ni ukitu.

Hakuna haja ya kuwa na ofisi ya makamu wa raisi kabisa na raisi asiwe na mgombea mwenza wakati wa uchaguzi.

Wabunge wasiwe na wagombea wenza na idadi yao ipunguzwe.At least kila wilaya itoe mbunge mmoja na at most wawili huku wakuu wa wilaya wakifutwa kabisa.Wakuu wa mikoa pia wafutwe na majukumu yao yarasimishwe kwa maRAS.
 
In short.......zitto you are not a presindency material even after 10 years!
 
hata wakishusha poa,kwani binadamu gani mwenye akili timamu amchague ZZK? Si ni bora awe lowasa? Napenda CDM ichukue nchi 2015,lakin sitaki zitto awe ndo mgombea urais,pia hata akiwa mgombea mwenza (running mate) ataharibu mambo ndani ya chama!!IKITOKEA, kura yangu ya Rais naipa CCM

Natamani viongozi wa CDM wawe wanachukua haya maoni ya wanachama vinginevyo itakula kwao.
 
Huyu kijana ni mroho sana wa madaraka lakn pia mkoa anaotoka umekua na sifa ya Usaliti mfano yuko wapi yule Kaburu alowika akiwa NCCR ya kipandi kile? zaidi tutegemee usaliti ule ule.
 
Mkuu umekuwa na jazba sana.

vitu vingine vinaudhi sana.anataka apunguze umri ili agombee,aliyemwambia achelewe kuzaliwa nani?anatutafutia BAN huyu,bora alijitoa JF,anasoma kama guest,msidhani hapitii humu,jazba ndizo zilimtoa humu..hapendi kukosolewa
 
Nakubaliana na wewe kabisa mku Zitto na shibuda ni majanga ndani ya Chdm na wanakera sana!
 
kwa nini 35 na siyo 18?hoja yake ina mashiko lakini kwa kipindi hiki ataonekana ni mroho wa urais sababu ashatangaza nia...akae kimya
 
Mods unganisheni na uzi huu hapa

www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/152109-jk-ataka-rais-ajaye-asiwe-wa-rika-lake-5.html

NB:Msimamo wangu uko pale pale sababu ya umri kuwa 40+ and above haielezwi

Tusiwazuie vijana kwa kutumia nguvu.Kama katiba inamtambua mtu mwenye miaka 18-35 kama kijana,ni kwa nini mwenye umri wa kati from35-40 usipewe uwezo wa kuongoza taasisi ya urais?Pia kwa nini tusiweke ukomo mwisho miaka 80 kwa sababu za kibaiolojia na kisaikolojia?

Hii age 35-40 imenyimwa baadhi ya haki za kuchaguliwa.Nyerere na Akina Lumumba walikua katika group hii walipochukua uongozi.Kwa nini tuwazuie ikiwa tunakubali wameshavuka ujana.Si wananchi wakiona hawafai wataamua wenyewe?tusitumie udikteta wa kisiasa kuhalalisha uhaini wa kidemokrasia kupitia mchakato wa kisheria kwa ghiliba

Zaidi ya vigezo vya umri tuangalie uadilifu na dira sahihi kwa Taifa.

Kwanza hao wabunge nao mbona walikomaa sana na umri wa urais?kuna suala la code of conduct,moral standard n.k

Unaposema wenye umri wa 35-40 wamenyimwa fursa ya kuchaguliwa je wa umri wa chini ya 35 wao watasemaje? Ukitaka haki kwa wote basi umri wowote una haki ya kuwania Uraisi. Vigezo vinavyotumika kuwaacha waliochini ya 35 ndiyo hivyo hivyo vinavyotumika kuwaacha walio chini ya 40 pia.
Huwezi kusema eti walioweka umri wa 40+ walikuwa washamba eti sisi leo ni welevu sana! Huyu huyu anayepambana umri ushushwe ili kukidhi matakwa yake siku atakapofika 40+ hutamsikia tena anatetea hii hoja maana haitakuwa na manufaa kwake! Huu ni ubinafisi wa kutaka kutimiza malengo machafu ya majitu yanayotaka nchi hii iendelee kubaki hivi ilivyo ili yaendelee kuwanyonya watz. Huu jamaa sijui ameahidiwa nini akitimiza haya malengo ngoja tusubiri lakini wenye kuipenda nchi hii tutaendelea kumwomba Mungu na Mungu ni mwaminifu ataiponya hii nchi dhidi ya hii dhuluma inayoendelea.

Tumwombeni sana Mungu maana kuna giza nene limeghubika huko tuendako!
 
Personally, sina matatizo na kigezo cha umri kwenye urais. Umri unaweza kuwa hata miaka isiyo chini ya 18 pale ambapo mtu anaweza kupiga kura. Tuna mifano, japo sio mingi sana ambapo kijana alichukua nchi na kuiendeleza vizuri tu, kama Thomas Sankara (Burkina Faso - the land of a standing man); Meles Zenawi (alikuwa dikteta lakini nchi yake imepiga hatua kubwa sana chini yake).

Ningependa kuona vigezo vinapatikana ambavyo kwavyo, anayevifikia ni lazima atakuwa amefikia umri fulani na kupata busara za kuhimili uzito wa Taifa nyuma yake. Kama wewe utakuwa na umri wa miaka 18 na ukawa na vigezo hivyo utaruhusiwa kugombea. Halafu tukumbuke kuwa kugombea sio kupata. Haki ya kugombea ni ya kila Mtanzania anayefikiria na kujipima kwamba ataweza mzigo huo, kwa hiyo kila mtu awe nayo.

Ningeshauri kuwa hivyo vigezo vitengenezwe (Elimu, uongozi, weledi, uelewa wa masuala ya kitaifa na kimataifa, etc) halafu kuwe na jopo huru la wataalamu watakaowasaili wagombea wa urais walioteuliwa kutoka vyama vya siasa na wagombea huru na ku=short list wale wote watakaovifikia viwango. Hao ndio wapitishwe kugombea.

Kama utakuwa na miaka 18 ukapitishwa, hakutakuwa na wa kukuzuia kugombea. Utapelekwa kwa WaTZ waamue hatma yako.
 
Huyu jamaa siku akiingia ikulu atabadiri hadi tarehe ya kuzaliwa mgombea urais iwe sawa na ya kwake! Anachefua na hata angejaribu hayo madoido yake kamwe CDM hawatompa nafasi ya kugombea am sure watamuengua wala asipoteze muda,labda kama ataendelea na mpango wake na Kafulira wa kuhamia NCCR!
 
PRESIDENCY MADE EASY!!!
-from college
-join opp politics
-Critic and radical member of paliamentary committe.
-Quick school on hot mineral issues.
-mix with bongoflavor celebrities
-fix age issue.
-Tayari urais unapatikana!!!!

BIG NOOOO......ZITTO

USHAURI:
Tumikia wananchi ktk ngazi ulionayo tikuone hadi tuyakaporidhika unafaa. Tena huna haja ya kujinadi, tutkuambia. At least 25 years

It takes more than what you think to be a true predident!!!
 
Back
Top Bottom