Wabunge Wote Wasiotaka Kura za Wazi are Cowards ni wakati Muafaka Wakajitoa huko Dodoma Haraka Sana!

Wabunge Wote Wasiotaka Kura za Wazi are Cowards ni wakati Muafaka Wakajitoa huko Dodoma Haraka Sana!

- Kaka Museveni ameweka standard Sheria mpya inaandikwa hadharani sio kwa siri, ha1 ha! ha!

Le Mutuz

Hopeless, tunaongelea katiba ya Tanzania kisha unaleta mifano ya Museveni hapa, kwa hiyo alichofanya Museveni ni katiba mpya ya Uganda? Kimepitia mchakato kama huu tunaoendelea nao sisi?

Jibu kwanza swali langu, una uhakika haijawahi kutokea duniani kote kura ya siri kama unavyodai?
 
Ahaaa huyuuu mutuz msengeremaaa kweliii we mbo wenywe wameteuliwa kwa siriii na rais au kulikuwa na kura ya wazi uteuzii wao


Sent from my iPhone 5 using JamiiForums

- Kaka ongea hoja sio maneno ya mtaani huu uwanja wa kimataifa kinachotakiwa ni hoja kaka, sema tena hoja yako ni nini hasa?

- Mimi nasema hivi Kiongozi wa umma kulilia kupiga kura kwa siri kisa anaoogopa viongozi wengine ina maana hafai na aondoke mara moja kwenye uongozi wa umma, wewe unasema nini kaka?

Le Mutuz
 
Hopeless, tunaongelea katiba ya Tanzania kisha unaleta mifano ya Museveni hapa, kwa hiyo alichofanya Museveni ni katiba mpya ya Uganda? Kimepitia mchakato kama huu tunaoendelea nao sisi?

Jibu kwanza swali langu, una uhakika haijawahi kutokea duniani kote kura ya siri kama unavyodai?

- So na wewe unatetea wanaume wazima kulia lia kuogopa kupiga kura ya wazi? ha! ha! ha!

Le Mutuz
 
Kweli mkuu, hata Mwalimu alikuja na sera ya chama iitwayo TUJISAHIHISHE.
CCM isipofanya hivyo haitweza kuwaunganisha wanachama wake kwa woga tu wa kuchukuliwa hatua za ku vote nje ya matakwa ya viongozi wao.

Na wala kumkosoa au kumsahihisha mtu haimaanishi unamchukia au haumpendi ila ni kuonyesha kwamba unamjali na lengo ni kutaka ajirekebishe.
 
Hii misukule ya CCM inakazi mno!! mbona kura za uraisi....tusichague kwa uwazi? kulakulala bana!!
 
- Coward that is what you are unfit to lead, ondoka kama upo huko Dodoma hufai simply hufai toka huko Dodoma waachie wanaume wanaoweza kusimama na kuhesabiwa, wewe unatetea mediocre ya kupiga kura kwa siri ili iwe nini? Utaandika katiba mpya kwa siri?

- Kaka kasome Founding Fathers wa Amerika kama walipiga kura kwa siri, infact Madison alitishia kuvunja process nzima iwapo hoja yake ya kuimarisha mahakama ingekataliwa na alismama na kusema wazi sio kwa siri, wale wote huko Dodoma ambao hamuwezi kusimama kuhesabiwa wakati muafaka sasa ondokeni huko you cowards!!

Le Mutuz
Wewe hata uandikacho hujui,wenye kutaka kura ya wazi ni wale makuwadi wa MEMBE and co ambao ni anti-lowassa ndani ya magamba,SO WEWE UMEANDIKA KUTETEA TUMBO LAKO.TAFUTA AJIRA WILLY..JINA LA MALICELA LIPO MAKUMBUSHO.
 
Nimependezawa na hayo mabadiliko yake.

CCM haijawahi kuwa na nia njema kuhusu watz.

CCM ni taasisi inayoundwa na watu wenye fikra na mitazamo yao binafsi. Haimaanishi kila mwana CCM akubaliane na kila jambo la CCM.
 
usituletee misimamo ya chama chako hapa,kura yoyote ni ya siri ili kuondoa chuk baada ya hapo
 
- Kaka ungeanza na Zitto na Kitila kufukuzwa chama na Migamba kupigwa ngumi hivi ilikuwa ni kwa sababuy ya nini kaka?

Le Mutuz
Ndio hapo sasa nataka ufikirie kama mwenye akili timamu, acha kujifanya hamnazo.
Kama na wewe unajua watu wamepigwa ngumi na kufukuzwa kwa kwenda kinyume na matakwa ya chama kwa nini unataka tena wapige kura ya wazi inayoweza kuwa ni kinyume na matakwa ya vyama vyao!?, Unataka tena wapigwe ngumi na kufukuzwa!??

Kinachotakiwa ni kujua tu wengi wameamuaje, na sio kujua kila mtu amepiga kura gani.
 
CCM wanapotaka kutetea kitu wakitakacho watatumia mbinu za kila aina, nakumbuka kuna kipindi walikuwa wanafanya uchaguzi kule Dodoma kwa kuogopa Mwenyekiti atapata kura za hapana basi Mjuaji mmoja akabuni mbinu ya kupiga kura kimkoa ili wajue ni mkoa gani wamempinga Mheshimiwa, hapo kila mtu akaufyata na wote wakapiga kura za ndio kwa Mwenyekiti.......sasa huko bungeni wameibuka na staili nyingine utadhani 2005 na 2010 tulipiga kura za uwazi..........CCM acheni kujitetea kwa kura za uwazi muone Bendera ya Tanganyika itakavyopepea kwa fujo mitaani.
 
- Nimeshitushwa sana na habari za mzozo wa Kupiga kura huko Dodoma kwenye bunge la Katiba, siamini kwamba leo 2014 Tanzania tuna viongozi watuwazima na akili timamu wanalia lia kama watoto wadogo eti wanaogopa kupiga kura za wazi are you kidding me or what? Katika kuishi kwangu nje miaka mingi sana sijawahi kusikia Viongozi wanaume wakililia kupiga kura za siri on anything, sasa sisi Tanzania tumemkosea nini Mungu mpaka kuweza kuwa na Viongozi wa Taifa waoga waoga mpaka kuogopa kupiga kura ya wazi?

- Mimi nilidhani Wanasiasa wote Duniani huwa wanalilia kazi zao kuonekana wazi kwa wananchi na hizi kura ndio haswa ilikuwa nafasi za wanasiasa wetu kuonyesha misimamo yao wazi kwenye kura na kuweza kusimama kuitetea kwa nini wamepiga kura kama walizopiga, badala yake naona wanaume watuwazima wakilia lia kila siku kuomba wapige kura za siri kusudi wasijulikane na wananchi wanaowaongoza wamepigaje kura zao, Really?

- Naomba wale Viongozi wote huko bungeni Dodoma wanaolilia kama watoto habari za kupiga kura za siri waondoke huko mara moja, cause hawafai, ni kiongozi gani Duniani leo anayeogopa kupiga kura ya wazi na kusimama mbele ya Taifa kutoa sababu za kwa nini amepiga kura yake kama alivyopiga? Ukweli ni kwamba hawafai kuwa Viongozi na hata kuwa wawakilishi wa wengine, wananchi wa Tanzania hatujawatuma viongozi waoga na cowards huko Dodoma ni simply kwamba hawawezi na hawatufai, waondoke mara moja na wawaachie wananchi wengine nafazi zao, wananchi wasio ogopa kuhesabiwa na umma!!, Wananchi tunataka katiba mpya na inatakiwa kuandikwa na wananchi walio tayari kufa kwa kusimamia misimamo yao, sio waoga waoga kama fisi fukuza wote huko Dodoma waoga waoga!!

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA

Le Mutuz Big Show

acha ujinga wako.kura ni siri ya mtu. kabebe mabox huko.nadhani umetumwa kwa akili zako huwezi kuandika upuuzi huu.
 
- Katiba ya Taifa haiwezi kuandikwa kwa kura za siri wale wote wanaolilia kura za siri waondoke huko now hawafai ni cowards, waondoke now!!

Le Mutuz
Huna uhalisia ndugu yangu. Jaribu kuwa mtafiti. Aondoke familia yake ife njaa? Sikuelewi ingawa juzi sred yako ilionekana umeanza kuona uhalisia
 
- So na wewe unatetea wanaume wazima kulia lia kuogopa kupiga kura ya wazi? ha! ha! ha!

Le Mutuz

Yaani hata hujui kutofautisha mifumo iliyotumika kwa Museveni kupitisha sheria yake na kinachoendelea Tanzania kuhusu katiba mpya na unataka kubeza mfumo wa kura ya siri.

Kwa taarifa yako nchi nyingi zimepitisha katiba za nchi zao kwa kura ya siri japo unasema hujawahi kusikia. Kutokusikia kwako haimaanishi haijawahi kutokea.

Uwazi unaotetea hapa umeanza lini? na utaenda ndani kiutendaji kwa kiwango gani? Hatutaki uwazi unaoishia tu kwenye kura ya kupitisha katiba. Kama umekua muumini wa siasa za uwajibikaji wa uwazi, mfumo huo uendelee kwenye mambo yote.

Suala la kiinua nyongeza ya kiinua mgongo cha waheshimiwa wabunge bado ni kitendawili hadi sasa hivi, ikulu ikitoa tamko lake, wizara ya fedha ikitoa tamko lake, katibu wa bunge na spika wakitoa kauli zinazotofautiana kuhusu jambo moja, kuna uwazi hapo?
 
Huna uhalisia ndugu yangu. Jaribu kuwa mtafiti. Aondoke familia yake ife njaa? Sikuelewi ingawa juzi sred yako ilionekana umeanza kuona uhalisia

Unafikiri haelewi uhalisia wa mambo? anajitoa ufahamu tu!
 
- Katiba ya Taifa haiwezi kuandikwa kwa kura za siri wale wote wanaolilia kura za siri waondoke huko now hawafai ni cowards, waondoke now!!

Le Mutuz
Willy, hivi ni chama gani cha siasa hapa nchini ambacho hupigiana kura za wazi? Nijuavyo mimi, hata ktk chaguzi za vyama za kura zq maoni tu ili kupata mgombea hata wa Udiwani, hupiga kura za siri. Rejea uteuzi wa wagombea wa Ubunge uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga juzi; ni mfumo wa kura gani ulitumika kumpata Mgimwa Jr na Tendega wa CCM na Chadema?
 
kaanze kwanza kumwambia mama ako wa kambo nae si yuko dodoma. au unamuexclude ndio maana unasema wanaume? au mama ako wa kambo nae mwanaume?
acha ubaguzi wa kijinsia wewe
babu zima, mwili kuuubwa akili kisoda.
ovyo
 
nashangaa sana wanasisiem wanaojifanya kwamba kura hupigwa wazi? rais na vibaraka wake huchaguliwa kwa siri.
 
Back
Top Bottom