Ngoja nikumegee kidogo....mchaga wa kibosho.
Ardhi moshi ni garama sana na haina cha maana inachozalisha, baada ya anguko la kilimo cha zao la kahawa ambalo wazee walitegemea km chanzo cha fedha ya kujikimu. Zao la ndizi likageuka ndio dili na kilimo cha mbogamboga, ili ulime unahitaji ardhi.
Elimu ilikuwa kipaumbele kwa watoto kwa sababu ardhi ni finyu na hakuna urithi "soma mwanangu hapa hakuna urithi, hichi kiamba (shamba) ni cha mimi na mama yako". Hiyo ni kauli kutoka kwa wazee tumekua tukiisikia kila siku ukizingua shule au ukileta ujuaji home.
Mila za kichaga ni noma kuliko hata ushirikina, kwa sababu zinahusisha kuchinja myama kwa style ya aina yake na manuizi ya kutumia maziwa. Tunaamini katika kuendelea kuwapa chakula wazee waliotangualia ili watuombee baraka. Desemba lazima tukumbuke ndugu walio hai na wafu kwa kuwapa chakula. Wewe ulishawahi kwenda kwenu kutoa shukrani, ukakunjua nafsi za nduguzo kwa chakula na kinywaji kizuri wakaachilia neno la baraka?!
Wivu wa maendeleo, disemba wakati unachinja na kunywa angalau mafundi wawe wanapandisha room nne ili wazazi wapate pazuri pa kulala na pia nikifa nitarudishwa hapo. "Wewe mushi huko dar unafanya nini hata kitenge umeshindwa kuninunulia, unaona mtoto wa mzee masawe nyumba anayojenga" Hiyo ni kauli ya mzazi akikupandisha hasira ya kutafuta hela, ukirudi mjini unapambana ili mzazi asiende kukusimanga tena.
Jua kilinge chako cha kutolea sadaka, kama hauko kwa Mungu tafuta mahali pa kutolea sadaka. Mafanikio hutekwa kwenye ulimwengu wa rohoni kwanza ndipo unayaona kwenye ulimwengu wa nyama.