Wachaga zindukeni, VICOBA vya kuzikana ni Umaskini!

Mimi sijasema kama waanzishe vikundi vya uchumi mkuu mimi nimeandika observation yangu tu kuchangia mada.
Labda umequote kitu tofauti ?
 
Huyo achana naye na wasiojitambua ety umaskini atutajie kikundi chao kilicho Jenga hata choo ?

Kamwe ukitaka kufanya chochote kile hasa kinachoshabihiana na pesa, jipime/jiulize unamudu ? Chungulia pato lako, ukiona huwezi kaa mbali !!!! Ndo inavyokuwa !

Hii ndio kanuni yangu, kuna mambo nikiona ni kina kirefu napiga chini mara moja
 
Kamwe ukitaka kufanya chochote kile hasa kinachoshabihiana na pesa, jipime/jiulize unamudu ? Chungulia pato lako, ukiona huwezi kaa mbali !!!! Ndo inavyokuwa !

Hii ndio kanuni yangu, kuna mambo nikiona ni kina kirefu napiga chini mara moja
Me nachoona mtu anauwezo acha afanye kama haimuumizi ni yeye,

Ila mtu kuumia kisa fulani kafanya hiki kwa pesa yake naona ni ujinga mwingine

akihusisha na mambo kama ya msiba kwamba yanachangia vipi umaskini yaani ??
 
Huwezi ingizwa huko na wewe sio mchagga. Na siku mchagga akifa wewe usio mchagga huwezi kuchangia lolote, utaenda tuu msibani.
Huwezi kuja sikia mchagga amekufa bakuri limepitishwa kuomba sukari, sanduku wala sanda. Wanandugu hamtoi hata mia mbovu hapo, mnaachwa muomboleze mpendwa wenu huku taratibu zote zikiratibiwa vizuri.
Utaenda msibani utakuta chakula kipo full time, haiazimwi tents wala kiti cha kukalia yote yatakodiwa. Sana sana utakuta landcruiser mbili tatu zipo fulu tenki na zipo silencer kwa kazi moja tuu, nyote mnaijua. Uchagga ni urithi na ufahari.

Upotoshaji: Umoja wa kuzika na kuzikana hasa kwa Wachagga, hauna lengo moja tuu la kuzikana. Humo ndani kuna mambo mengi ya kijamii kama magonjwa, kuugua, matatizo mengi ya kijamii.

Ukiona mtu hawezi kuchangia laki moja kwa mwaka kwenye vitu kama hivi, huyo ndio masikini mwenyewe sasa. 😊
 
Imagine hayo makundi leo yangeitwa, "kundi la michango na kutafutiana Fursa" mnachagua watu kila mwezi wa kuwanzishia biashara na wanalipa deni kidogo kidogo, ukifika mwaka kila mtu ama ni mkulima ama mfanyi biashara!

Tukalogwa na mamisiba!

Wabongo niliwahi kuwashauri hivyo kwenye harusi moja ya jamaa wa mtaani😄😄😄

Wabongo waliniona mchawi, niliwauliza hivi ni akili au matope mnachangisha mchango wa millioni 25 alafu yote mnaogaragaza kwa siku moja.

Kwanini msimpe kijana kama mtaji let say millioni 15 alafu hiyo 10 kijana na mkewe wakatafutiwa viwanja.

Nikawaambia tungekuwa na huo utaratibu tanzania ya leo isingekuwa na vijana walialia maisha magumu, wengine wanaoa baada ya miezi sita wanakimbia ndoa😄😄😄.

Yaani jamii hii ilivyo masikini wa akili na mawazo.Wanaona ni bora watoe hiyo michango ya laki au laki mbili wakale sahani ya pilau,nusu kuku na kipande cha tango na vibia chupa nne.Hapo nafsi inasuuzika sana.

📌UMASKINI NI MENTALITY❗❗

HATA BILA MKOLONI MUAFRIKA NI MBINAFSI NA NDO UMASKINI UPO HAPO HII IPO KWENYE DNA.
 
Hakuna tatizo kuzikwa na Halmashauri au na familia yako tu kama huko US na Ulaya wanavyozikana, nafikiri ni suala la utamaduni tu na kutambiana wabongo hasa Wagalatia kupenda mazishi ya kifahari yenye watu wengi na mbwembe nyingi.
 
Tufikirie je ya boksi, tuanzish makunddi ya kujadili biashara na fursa, saya nsi na technology.
 
Nina cha kwetu hapa tulipo kina piga mult purpose,kuzikana ipo,kukopeshana ipo,yaani kinapiga kote kote,dadeki.
 
Vikundi vinasaidia sana Kukuondoa kwenye aibu ndogo ndogo especially kama umefiwa na Mpendwa wako wa karibu, Vikundi vyenyewe unakuta Kwa Mwaka mzima unachangia total 120k na ukipata janga wanakushika Mkono Kwa 1M
 
Nina cha kwetu hapa tulipo kina piga mult purpose,kuzikana ipo,kukopeshana ipo,yaani kinapiga kote kote,dadeki.
Lazma kuna mmoja wenu kasoma nje ya nchi, mawao ya kwetu ndani ni kuzikana tu!
Naomba niunge huk, kama hakina wachawi.
 
Vikundi vinasaidia sana Kukuondoa kwenye aibu ndogo ndogo especially kama umefiwa na Mpendwa wako wa karibu, Vikundi vyenyewe unakuta Kwa Mwaka mzima unachangia total 120k na ukipata janga wanakushika Mkono Kwa 1M
Cha kwetu tumeweka mkazo kwenye kukusanya faini,kwa kosa lolote kwa mujibu wa kanuni zilizopo,hivyo hizo faini ndizo zinahusika zaidi na misiba,hazina kuu haiguswi,na endapo kama faini zitakuwa pungugu basi, fedha hukopwa kutoka hazina kuu,na baadae faini zikitimia hurejeshwa katika mfuko mkuu.
(Najaribu kutoa format ili wengine waige utaratibu huu mzuri sana,hukwami hufi njaa)
Ili ukope itabidi udhaminiwe na wanachama 3, wasiodaiwa monthly fee, dhamana za hao watatu waliokudhamini ndani ya kikundi,ndiyo fedha itakoyotumika incase hukulipa!
( Kuhakikisha kikundi kinakuwa salama)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…