Wachambuzi "Bingwa wa Kombe la Dunia Argentina aliandaliwa Mapema na Makusudi Kabisa ili Messi Ashinde"

Acha niwe wa mwisho kuamini huu upuluzi.
 
Acheni nongwa, kwahiyo ufaransa alikuwa amesimama tu kipindi argentina anashambulia? Tatizo lenu matokeo yamekuja tofauti na fikra zenu ndio maana mnaumia
 
Yaani nilikuja kujua Argentina anabebwa na kuandaliwa ubingwa ile mechi ya Netherlands ile penalty ilikuwa nje ya box na jana refa kazima shambulizi la goli kwa France
 
Haya bas mwambieni Ronaldo akachukue kikombe cha kahawa anyanyue juu ntamlipia
 
Huu ni umbumbumbu, yaani kwa mpura ule uliopigwa bado kuna watu wanaleta doubt,? Kama penalty ndani ya mchezo mbona kila timu ilipata ?,kipindi cha kwanza pande zote
 
Kwamba Argentina kabebwa fainali? Hivi kweli Kati ya aliyepewa penati moja na mwingine mbili nani kapendelewa? Wenzetu waliofungwa hata hawalalamiki wamekubali yaishe. Asiyekubali kushindwa si mshindani.
 
Umewaambia ukwel usio na shaka,hizo penati za jana zilipindiswha na FIFA?,maumivu yakizidi mwone daktari
 
sasa ulitegemea mashabiki wa ronaldo wangesemaje? we hukumsikia pepe na bruno wanatolewa na moroco ila wanamlaumu messi!

kwan nan aliwazuia ufaransa kufunga? kuna goli la ufaransa lililokataliwa? mbona nao wamepata penat 2 na refa wala haja review kwenye VAR, swala la kubebwa ni mtazamo tu, ukishaamini unaonewa hata nzi akikugusa utasema uonevu unaendelea, hvi ,mtu asiye na uwezo ana bebwaje?, watu wanapambana unaona kipa anaokoa mpaka penat halafu unasema imepangwa? ingekuwa rahisi hvyo na ronaldo angekuwa fainali.

recently argentina ndo timu best timu, walikuwa na unbeaten run ndefu , waliwakalisha mpaka brazil fainal copa america, tukubali tu uwezo wanao na wamesatahili, pia bahati imekuwa upande wao maana 2014 walikosa tu bahat wangebeba, pia wameingia fainali 3 za copa america kabla ya kushinda. RESPECT THEIR STRUGGLE, hizo cheap evidence hazibadilishi chochote, ARGENTINA ARE WORLD CHAMPIONS. let that SINK in
 

timu gani ya ulaya imewafunga argentina world cup hii? na ulaya pangekuwa pagumu hvyo italy asingekuwa na unbeaten run 37 kati ya 2018 mpaka 2021. Pia ukumbuke hao brazil walipigwa fainal na argentina tena wakiwa maracana, walikuwa full kikosi na hakuna kitu walifanya. astahiliye heshima apewe tu
 
Ninachokijua ata sh mia mbili inatosha kununua kamba ujinyonge kama Argentina kuwa bingwa unaumia
 
kama kweli fifa au refa angekuwa anawabeba argentina, ile penati ya mwisho asingetoa.. maana muda ulikuwa umeisha na argentina wangebeba ndoo, wanaongelea kubebwa kupi hawa
 
Acheni nongwa, kwahiyo ufaransa alikuwa amesimama tu kipindi argentina anashambulia? Tatizo lenu matokeo yamekuja tofauti na fikra zenu ndio maana mnaumia
Wapumbavu hao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…