Wachambuzi wa siasa za kimataifa naomba mnijibu maswali yangu haya kuhusu taifa la USA

Wachambuzi wa siasa za kimataifa naomba mnijibu maswali yangu haya kuhusu taifa la USA

kendy

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2015
Posts
296
Reaction score
564
Mnafahamu kuwa kwa Sasa mgogoro baina ya Ukraine na Urusi ,unaonekana kuwa Kati ya Urusi na Marekani? Yaani sasa hivi ni majibizano kati ya Joe Biden na Vladimir Putin?

Kwanini Marekani kashikia bango mgogoro huu?

Kwanini Urusi anashauri NATO isiiunge Ukraine? Lakini kwa Nini Marekani analazimisha ijiunge au kwa nini Marekani ndio inakataa matakwa ya Urusi na sio nchi za Ulaya?

Kwa sababu gani Marekani Ana majeshi Ulaya lakini hataki Urusi awe na majeshi north America au south America?

kwa sababu gani Marekani hataki nchi nyingine zinunue baadhi ya silaha kutoka Urusi,mfano hataki uturuki ama India, Indonesia, Misri, Iran ama hata China zinunue silaha toka Urusi na hata ikibidi anatishia kuziwekea vikwazo?

Kwanini Marekani hapendi nchi fulanifulani ziwe na silaha kalikali mfano Iran, Korea kaskazini na baadhi ya nchi, ama hata kufanya majaribio tu.

wakati huohuo Kuna nchi zinamiliki silaha Kama hizo nchi ambazo Marekani hataki zimiliki silaha hizo.

kwa Nini Marekani inapinga Sana mradi wa Bomba la kupeleka gesi ulaya kupitia ujerumani?

Je, haiwezekani mgogoro huu Bina ya Ukraine na Urusi kuwa umeratibiwa kwa ustadi mkubwa Sana ili kupeleka Urusi kuzozana na Ukraine I'll kupata sababu ya kuiwekea ngumu Urusi katika mradi was Bomba la gesi na hasa iwekewe vikwazo? Nia ni kuidhoofisha kiuchumi na kutengwa?

Kwanini Marekani haifurahii Urusi kufanya mazoezi ya Kijeshi ndani ya mipaka yake hata Kama ni jirani na nchi nyingine hasa zilizo magharibi mwa Urusi?

wakati yenyewe Marekani inaweza kufanya mazoezi na nchi yoyote? Hata zilizo karibu kabisa na Urusi?

Unajua kuwa Marekani Ina pitisha meli zake kalikali kabisa za kivita katika maeneo ya karibu kabisa na Urusi,mfano black sea?

Marekani ni muumini mkubwa Sana wa demokrasia? Lakini kwa Nini yenyewe haitoi demokrasia kwa nchi nyingine kujiamulia Mambo yao kwa mfano haki ya kujilinda? Mfano haruhusu Iran na Korea kaskazini kuwa na silaha za nyukilia?

Haruhusu demokrasia ya kujiamulia baadhi ya Mambo ya nchi. Mfano, kuna nchi kimila na kitamaduni zao hawaruhusu ndoa za jinsia moja, lakini Marekani hulazimisha na kuzitisha nchi hizo ziruhusu Mambo hayo?

Hayo ni machache, naomba wataalamu was siasa za kimataifa mnipe majibu ya maswali yangu
 
Hapa sioni Swali hata moja,zaidi zaidi unatema nyongo tu. Hata hivyo hujaleta hoja kitaalamu ili ijadiliwe badala yake umeonesha kuifagilia Urus huku ukiilamu Marekani. Hujataja baya hata moja la Urusi. Kiufupi wewe ni timu Putin kwahiyo utajibiwa kitimu Biden tu.
 
Kwa sababu kwa sasa ivi yeye ndio superpower simple tu na akija superpower mwingine na yeye ataanza kupuyanga tu
 
Kuna mambo hujui; Biden hajalazimisha Ukraine ijiunge na NATO, na in fact Georgia na Ukraine ziliwahi kuomba kuingia NATO zikakataliwa.

Mengine ya "kwa nini Marekani haitaki hiki wala kile" ni innuendo tupu za mitaani tu. Ungekuwa makini ukatazama historia ya miaka 30 iliyopita tangu USSR ilipoanguka, ungeweza kuandika na mada nzuri kuliko hii ya kuungaunga maneno ya hisia za kutoka mitaani tu.
 
Da ila waswahili bana Huwa wajinga sana ,Sasa jamaa kauliza vitu ambavyo yeye anaona havijui,anaomba maomi yenu,badala ya kumfahamisha unshambulia.
 
Da ila waswahili bana Huwa wajinga sana ,Sasa jamaa kauliza vitu ambavyo yeye anaona havijui,anaomba maomi yenu,badala ya kumfahamisha unshambulia.
Huyu utamjibu nini sasa wakati ameuliza maswali kwa kuonyesha kabisa kwamba ni timu Putin na anaichukia Marekani
 
Da ila waswahili bana Huwa wajinga sana ,Sasa jamaa kauliza vitu ambavyo yeye anaona havijui,anaomba maomi yenu,badala ya kumfahamisha unshambulia.
nadhani na wewe huenda ni mjinga unadakia mambo usiyoelewa.

Ukisoma hapo utaona premise aliyotumia kujenga maswali yake ina makosa, na ndiyo ninayokosa kuwa hajui analosema. Lakini wewe kwa kutokuelewa hilo, unadhani kuwa mtu aliyekosoa swali hilo ni mjinga kumbe wewe mwenyewe ndiye una upungufu.

Angalia: Ukiuliza swali kwamba kwa nini mtu fulani anakuchukia, premise yako ni kuwa unajua kweli anakuchukia ila unachotaka kueleweshwa ni kwa nini anakuchukia. Sasa iwapo itajulikana kuwa mtu huyo hakuchukii, basi utajibiwa kuwa huelewi unachouliza, na jibu la namna hiyo siyo ujinga.
 
Huyu utamjibu nini sasa wakati ameuliza maswali kwa kuonyesha kabisa kwamba ni timu Putin na anaichukia Marekani
Putin ana matatizo sana. Anataka nchi za eneo hilo zote ziwe mikononi mwake kama ilivyokuwa USSR, na viongozi watawale milele kama yeye. Angalia marais wa nchi marafiki zake wa Beralus, Azerbaijan, Turkmenstan, Tajikistan, Uzbekistan, Krygyzstan, Kazakhstan. Hapendi demokrasi ya Magharabi ambamo mto yeyote anaweza kuwa kiongozi, hivyo wale wansiasa wa ncho zote za Magharibibi waliosmea Ulaya na Marekani ni maadui zake: Georgia, Ukraine, Estonia, Moldova, Latvia, na Lithuania. Amekuwa anadai kuwa wakati wa USSR kuangua, NATO iliahdi kuwa haichukua nchi yoyote iliyokuwa chini ya USSR. Lakini huo wote ni uwongo tu kwani hakukuwa na makubaliano ya na,mna hiyo kabisa. Wakati huo Russia ikiwa katika hali ngumu sana BYelstin alikuwa anaitegemea sana Marekani. Kuna wakati alitoa ombi kwa Clinton kuwa NATO isizipokee nchi zilizokuwa za USSR, hasa wakati Poland inaomba hivyo, lakini Clinton alikataa. Transcript za maongezi yao yaliyofanyika March 21, 1997 ziko hapa kuanzia ukurasa wa 105.

Leo hii anavumidsha uwongo kuwa NATO ilivunja makubalianao ambayo hayakuwapo kabisa; anaogopa nchi zenye demokrais ya kweli kuwa jirani yake. Kuna mama mmoja wa Ukraine alikuwa anasema kuwa sisi hatuji nani rais ajaye, lakini Urusi wanjua kuwa rais ni Putin tu.
 
Attachments

demoghasia sio mfumo pekee wakiutawala duniani
kama ukiona wewe unaupenda wenzio hawaupendi nahakuna shida
kama wewe unapenda ndoa zajinsia moja wenzio hawapendi hakuna shida nakinyume chake kipo sahihi pia
UKRAINE.anatakiwa akijiunga na NATO apewe kichapo kizito tena kizito mnooooooo
 
Back
Top Bottom